Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
FaizaFoxy anachungulia tu huu uzi hata hachangii
Kama hilo llilikuwa shirika la umma vipi msishangae mashirika ya umma yote yaliyokufa mshangae hilo tu?
Ni nini kinatafutwa? Tanganyika Packers vipi?
Viwanda vimeuliwa na serekali ya ccm full stop!
Adhabu yenu ni October!!!
Viwanda vimeuliwa na wale waliokuwa wanachaguliwa kuendelea na masomo bila kufaulu. Unawajuwa ni akina nani.
Viwanda vimeuliwa na wale waliokuwa wanachaguliwa kuendelea na masomo bila kufaulu. Unawajuwa ni akina nani.
Mkuu FaizaFoxy nchi hii nyie ndo mmeiangamiza kweli angalia tatizo la ajira kwa vijana wetu, mimi sijui hawa vijana wengi wanaomaliza vyuo wataajiriwa vipi wakati hivi viwanda vingekuwepo leo tungekua mbali saana. Maana tusingweza kutumia bidhaa za kichina wakati sisi wenyewe tunaweza zalisha. Na hata hao wachina wasingetuletea bidhaa feki kama wafanyavyo sasa.
Wanaposema miaka 50 na mafanikio makubwa hua najiuliza saana. Mnakodisha majengo ya viwanda kwa ajili ya makanisa na magodown wakati vijana kibao wanazurula.
Ni bora sasa CCM iachie madaraka kwa chama kingine walau hata miaka 5 tuone tofauti maana hakuna tunachofanya zaidi ya siasa tu, mikataba mibovu. Sisi huku kwenye makampuni binafsi ndo usiseme tunavyonyanyasika halafu ni hao viongozi wanaosimamia mikataba ya kutuangamiza wananchi wakati watoto wao wanawapeleka mashirika ya serikali ili tuibiwe zaidi. Ila Mungu yupo pamoja na sisi tutashinda tu. We must do changes wana JF popote ulipo tubadilike sasa. KATAA CCM 2016 TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA
Waseme ama unaogopa kupigwa ban lumumba
Nakumbuka miaka ya 85 hadi 95 tulikuwa tukipeleka kuuza kahawa KNCU tunapeleka kama ni gunia 20. Unapewa dawa bure na magunia mapya toka kiwanda cha moshi bure
Hiyo imebaki history
Dah mchozi unanitiririka.Kwa anaye fahamu sababu ya kuiba vinu vya kutengeneza matairi ya ubora wa hali ya juu kutoka kiwanda maarufu Nchini na Duniani kilichokuwepo Arusha juzi juzi tu cha General tyres na kuvihamishia Kenya ambapo wanavitumia kutengenezea matairi ya Yana tyres then wanakuja kutuuzia hayo matairi huku Tanzania, nini chanzo?
============================
==========================================
==================================
=====================================
nakubaliana na hoja zako hapo juu kutokana na hilo mwenyekiti wa bodi ambaye ni shelukindo ,anatusikia haoni kuwa amelitia hasara taifa ya kutosha kwa kukubali kiwanda kimfie mikononi mwake ,je kwanini asifunguliwe mashtaka ya kuhujumu kiwanda cha general tyre kutokana na serikali kukosa kodi kubwa kutoka kwa wafanyakazi pia.nawakilishaSababu za kufa General Tyre ni kama ifuatavyo.
Mosi,Bodi ya wakurugenzi ilikuwa ya kisiasa zaidi badala ya kuzingatia utaalamu.
Wajumbe wengi wa bodi walikuwa ni wabunge wa JMT ambao walitakiwa kuyasimamia mashirika ya umma kupitia kamati kama PAC.Madudu yaliyokuwa yakifanywa na management yalikuwa yakipata baraka za bodi kupitia vikao na posho mbali mbali.Wabunge waliokuwa wakiisumbua serekali kupitia hoja mbali mbali walikuwa wakitupwa kwenye hizi bodi za ulaji bila pasipo uwajibikaji.Kamati za kusimamia mashirika ya umma mara nyingi zilijikuta zikishindwa kufanya kazi ipasavyo kwasababu ya kuwa wajumbe wa bodi za mashirika hayo na wakati huo huo wajumbe wa kamati za bunge.Hili Zitto kalisema sana lakini watawala wetu wametia pamba kwenye masikio.
Laiti wanyama pori wangekuwa wanazalishwa kama bidhaa nyingine mashirika kama TANAPA & Ngorongoro Conservation Area Authority yangeshafungwa siku nyingi.Mashirka kama NSSF,PPF.... tungeshayasahau kama yalishakuwepo.
Pili,Ikumbukwe General Tyre ilianzishwa na Mwl Nyerere ambaye alitembelea USA miaka ya sabini mwanzoni akakuta General Tyre Amerika wana modernise kiwanda chao so mitambo ya zamani haikuwa na kazi kwao wakati huo.Mwl Nyerere akawaomba General Tyre wailete mitambo ya zamani Tanzania jambo ambalo walilikubali.General Tyre USA wakapewa 26% na serekali ikamiliki 74%.Mwl Nyerere angekuwa mlaku kama wanasiasa wengine pengine 74% share zingekuwa zake na familia yake lakini hakufanya hivyo.Katika makubaliano hayo Tanzania ilikubaliwa kuunda bodi na baadhi ya manager hasa HRM na maeneo mengine hasa ya technical wakaachiwa wamarekani.Kwenye bodi aliingia Mkurugenzi mkuu,mkurugenz wa fedha na mkurugenzi wa uzalishaji wote hawa wamarekani watanzania badala ya kuingiza vichwa vya ukweli tukawapa ujumbe wa bodi akina Gullamal,Shellukindo na wabunge wengine wengi kwaajili ya kulipana posho.
Kwakuwa General Tyre ilianzishwa na technoligia ya zamani kama nilivyoonysha hapo juu.Kati ya mwaka 2003 - 2005 sikumbuki vizuri ilikubaliwa kununua mitambo mipya ya kisasa kwaajili ya kuendana na kasi kubwa ya maendeleo ya uzalishaji wa tyre.NSSF ikatoa mkopo wa dola 10 milion serekali ikiwa mdhamini wa mkopo huo.Badala ya kununua mitambo mipya mitambo ya zamani ikapakwa rangi na fedha zote zikatokomea.Utashangaa leo unaambiwa deni la taifa linazidi kuongezeka ukichunguza utakuta linaongezeka kwa mambo kama haya.
Hii fedha ya NSSF naambiwa ilitumika kujenga hotel ya waziri aliyepitisha udhamini wa serekali baada ya msukoko wa kuoneeana wivu akauza hiyo hotel kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Tutakutana October, lazima kieleweke!!!!
Kulikuwa na Coffee Curing pale Moshi na Tanalec kule Arusha, hivi navyo vinajikongoja au vilishakufa?
Kibo Match pale Moshi kipo mochwari sasa hivi.
Breweries aahh inauma ...
***2015 operation Delete CCM*** basi
Mkuu TANELEC bado kipo ila kinasuasua sana. Kimechukuliwa na Jamaa toka Kenya Baada ya Wanorway waliokianzisha kuondoka.
Ila ninasikia hali yao ya uzalishaji imeshuka mno baada ya Tanesco kuacha kununua Transformer zao jambo lililosababisha mwaka huu kiwanda hicho kupunguza wafanyakazi zaidi ya hamsini.
Tanesco wananunua Transformer nje.(China na India)na kuacha kununua nyumbani.