General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

Kwa Mara ya kwanza naomba nikukosee heshima Leo wewe ni mchawi aiseee
Jamaa na kuelezea kote juu ya kifo cha General tyre wewe unapinga tu

Kuniita "mchawi" ni heshima kubwa sana kwangu.

Hata Pele aliitwa mchawi wa soka duniani.
 
inaiuma sana kuona kuna watu wanatetea ujinga wa serikali yetu.
alioyasema ngongo yamenichoma roho.mwenyekiti wa bodi alikuwa ni mccm
 
....Wakiristooooo ! Ngongo
 
Last edited by a moderator:

tusipochukua hatua hawa watu watataka mpaka tuvuje damu....... inasikitisha hawaoni pa kutafuta mapato zaid ya udhalimu kwa ela za watu!!!
 
Licha ya viwanda kufa, mashamba ya ngano ya Basutu yaliyokuwa makubwa sana leo ni vichaka vya swala. Yaani inaniuma sana kwa viongozi wetu kukosa uzalendo. Nchi yetu ni tajiri sana kilichokosekana ni uongozi bora basi.
 
Ngongo

Samahani kaka mkubwa naomba unijuze tu!! Hivi kiwanda kilichokuwa jirani wa kiwanda cha General Tyre cha KILITEX kilichokuwa kinatengeneza nguo kipo au nacho ndo tumeshakula mtaji??
hichi kiwanda juzijuzi kinana alienda kukitembelea akakuta ni ghala tu siku hizi....ukipita pale ni kama gofu tu
 
Upuuzi wa kufilisi viwanda umetufikisha pabaya kiasi cha kuwa wayegemezi wa kila kitu toka tyres hadi njiti za kuchonoa kwenye meno. Mambo kama haya huyapati China
 
Watanzania waliokosa uzalendo wamelaghaiwa na wahindi na Waarab kulifilisi hili taifa chunguza viwanda mfu vyote vimenunuliwa na wahindi na Waarab then wakawa ma supplier na wagavi wa bidhaa zilizokuwa zikizalishwa na viwanda hivyo kutoka nje.
Wahindi sio watu wema kabisa na uchumi wa nchi yetu.
 
siyo kweli.Yana ni one of the sameer group of companies ya kenya.Taarifa za sembe hizo.
 

Umenena vema hapo
 
.. ndugu yangu Ngongo, unashangaza sana kama ambavyo watanzania wengi wamekuwa wakishangaza, mnamsifia Nyerere upande mmoja halafu hapo hapo mnamkosoa upande pili. Umesema Nyerere alianzisha General tyre kwa makubaliano ya umiliki wa 74% kwa TZ na 26% USA, lakini hapo hapo, nanukuu kauli yako: “WATANZANIA BADALA YA KUINGIZA VICHWA VYA UKWELI TUKAWAPA UJUMBE WA BODI AKINA GULLAMAL, SHELLUKINDO NA WABUNGE WENGINE WENGI KWA AJILI YA KULIPANA POSHO” mwishi wa kunukuu
Wajumbe wa bodi za mashirika ya umma wanateuliwa na mh rais, kwa maana hiyo hao waliokuwa wajumbe wa bodi ya General Tyre, walioua shirika hilo waliteuliwa na Nyerere kwa ajili ya kulipana posho. Halafu kumbuka kila walipoharibu hakuwawajibisha ndiyo maana mashirika yote kufa hata kabla Nyerere hajaondoka madarakani ila alikuwa anayanusuru kwa usanii wa kuyapa ruzuku ili yaonekane yapo hai.
 
Hizo takwimu za namna ya zile alizoweka hapo Ngongo, ndizo ninzotaka watangaza nia wagombea na hata ilani za vyama vya siasa wakati huu watanakiwa waziweke wazi, na watoe mapendekezo namna watakavyo wasulubu kisheria walihusika na hujuma hiyo kwa watanzania na mbinu gani watazitumia kudhibiti ama kukomesha hujuma za namna hiyo siku zijazo...!
 
Last edited by a moderator:
Kina Gulamal & co waliteuliwa enzi za Mkapa Nyerere hakuhusika kabisa.

 


naungana nawe sana. kweli unaweza enda shule na usieleimike, watu wamebaki na ushabiki wa kisiasa tu, ndio mambo machafu yametendeka ila ninauhakika karibu 90% ya wale wanaishutumu serikali nao ni mafisadi vile vile. Nina hakika ndio wa kwanza kukwepa kodi, kupokea hongo na rushwa kupitisha magendo kusoma magazeti siku nzima ofisini na kubia makampuni ila wanakaa kando na kunyoosha vidole serikali. Tunakuwaje watu tusio weza kujisimamia na kujiendesha wenyewe?!

Kuokoa taifa ni jukumu letu sote lazima kila mtanzania avae uzalendo na kusimama katika nafasi yake kuitetea nchi tuwe na uchungu basi japo kidogo tu, nakwambia hata kije chama gani kipya mambo ni yaleyale tuu maana watu waliopo kwenye system ya uchumi uwe serikalini au shirika la umma au binafsi hamweki maslahi ya taifa mbele mnasumbuliwa na ubinafi, uchoyo, ulafi na umimi tu.
Na ni vyema kumwangalia mgombea kama mgombea na kueka uchama pembeni maana sidhani kama wote wa ccm ni wachafu au wote wa upinzani ni wasafi na waadilifu.

Be wise people, it begins with you.
 

Hayo niliyafungulia nyuzi zamani sana: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...zania-msichaguwe-chama-chagueni-kiongozi.html
 
Dah.....laiti mwalimu nyerere akipewa bahati ya kufufuka akiiona Tanzania yake ilivyo na akiwaona watanzania wake walivyokata matumaini anaweza akafa tena kwa mstuko.......
 
Dah.....laiti mwalimu nyerere akipewa bahati ya kufufuka akiiona Tanzania yake ilivyo na akiwaona watanzania wake walivyokata matumaini anaweza akafa tena kwa mstuko.......
asingeamini kwamna hivi sasa nyama ya ng'ombe inauzwa 6,000/- badala ua sh.5, shillingi inaporomoka mno kwa ukosefu wa viwanda..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…