naungana nawe sana. kweli unaweza enda shule na usieleimike, watu wamebaki na ushabiki wa kisiasa tu, ndio mambo machafu yametendeka ila ninauhakika karibu 90% ya wale wanaishutumu serikali nao ni mafisadi vile vile. Nina hakika ndio wa kwanza kukwepa kodi, kupokea hongo na rushwa kupitisha magendo kusoma magazeti siku nzima ofisini na kubia makampuni ila wanakaa kando na kunyoosha vidole serikali. Tunakuwaje watu tusio weza kujisimamia na kujiendesha wenyewe?!
Kuokoa taifa ni jukumu letu sote lazima kila mtanzania avae uzalendo na kusimama katika nafasi yake kuitetea nchi tuwe na uchungu basi japo kidogo tu, nakwambia hata kije chama gani kipya mambo ni yaleyale tuu maana watu waliopo kwenye system ya uchumi uwe serikalini au shirika la umma au binafsi hamweki maslahi ya taifa mbele mnasumbuliwa na ubinafi, uchoyo, ulafi na umimi tu.
Na ni vyema kumwangalia mgombea kama mgombea na kueka uchama pembeni maana sidhani kama wote wa ccm ni wachafu au wote wa upinzani ni wasafi na waadilifu.
Be wise people, it begins with you.