Naona vijana wanaendelea nguvu ya uchawa kawa Rais maana kila kitu sasa utasikia Samia hivi na vile yani hashitag kibao kumuhusu Rais Samia.
Sasa ndiyo njia pekee ya kufanikiwa kwenye mambo yao? Hii ni to much
======================
Programu mpya ya vijana inayojulikana kama Generation Samia (Gen S) imezinduliwa rasmi, Disemba 2, 2024, jijini Dodoma, kwa lengo la kuwaunganisha vijana wa Kitanzania kutoka sekta mbalimbali na kuwajengea mtandao wa fursa za maendeleo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, msemaji wa @Gen_samia, Sonata Nduka, amesema programu hiyo inalenga kuwa chachu ya mafanikio kwa vijana, ikiwakutanisha kutoka nyanja tofauti kama wajasiriamali, wafanyabiashara, wanamichezo, wasafirishaji, na wajenzi.
Sonata amesema Gen S inalenga kufanikisha ndoto za vijana kupitia juhudi za pamoja huku ikichagiza matumizi ya mazingira rafiki yaliyowekwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uchumi wa vijana.
Katika hatua ya kuimarisha mtandao wa vijana, Gen S imeandaa tukio la mbio za pamoja lijulikanalo kama Gen S Jogging, litakalofanyika Jumamosi, Disemba 7, 2024, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mbio hizo zitaanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 3 asubuhi, zikiwaleta pamoja vijana kutoka makundi tofauti, ikiwa ni pamoja na vikundi vya jogging, wafanyabiashara, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali, pamoja na wanamichezo.
Sonata amesema tukio hilo si tu fursa ya kujenga mtandao wa kijamii na kiuchumi bali pia litakuwa sehemu ya burudani kwa vijana wa mjini.
Magufuli aliichekea hii sumu na imekuwa mbaya zaidi.
Simpatii picha raisi ajae akiwa wa type hizi, itakuwa ni balaa mpaka vyooni atataka ziwekwe picha.
Tukiwa TUNASHENYENTANA tumpongeze tunashenyentana kwa uhuru na utamu umezidi kiasi. 🤣
Mnoaratob program lukuki za samia ukweli ni kwamba mnaboa na hazina impact
Sijajua labda ni project mnapewa mafungu ya hela ila ukweli ni kwamba huku ground tunaona kama mnamchafua maana kila kitu sami..sami kwani matendo yake katijka uchumi wa Nchi na jamii si yangetosha kumtangaza. Au hayapo?.