Gentamycine kwa wewe ni mnyarwanda kweli hebu tuambie nini maana ya maneno haya

Inatosha mkuu ,usitoe sana madini
 
Naona mkuu umewatolea uvivu unawapa haki yao

Wamelilia wenyewe ' Wembe ' ngoja sasa ' uwakate ' vizuri Mkuu. Nina sifa kubwa mbili Ustaarabu sana kama nitakutana na Mstaarabu mwenzangu na Muhuni mno kama nikikutana na Mhuni mwenzangu. Na ' Principle ' yangu humu haijawahi na haitowahi kuja kubadilika ambapo nitakupokea kadri utakavyokuja ( kwa lugha iliyo nyoofu na nyepesi ni kwamba ukitishia tu Kujamba basi Mimi naharisha kabisa )
 
Hahahahaha me nakukubali
 
huko kote mlikuwa mna`guess,ila huu sasa ndio uhaya wenyewe...
 
Inatosha mkuu ,usitoe sana madini

Mkuu kuna Watu humu wanataka ' tufunguke ' zaidi kisha wajione ' takataka ' na ' waumbuke ' vilevile. Wengine hatujazoea na hatujakuzwa katika ' Kujionyesha ' Mkuu na hadi hii leo naikumbuka Kauli ya Kibusara aliyoniambia Rais Museveni mwaka 1996 mwezi September aliponipandisha katika ' Chopper ' yake nikiwa na ' First Son ' wake Muhoozi Kainerugaba huku huyu ' sacked ' IGP mwenye matatizo sasa Kale Kayihura akiwa ni mmoja wa Walinzi wake katika Kikosi chake cha PPU ( Presidential Protection Unit ) kwenda kunitembeza Kijijini Kwake Rwakitura na katika ' ranch ' yake ya Ntungamo na kunitambulisha kwa Marehemu Baba yake Mzee Amos Kaguta ambapo aliniambia namnukuu...." Nawapenda sana Watanzania na Tanzania mmebarikiwa sana kumpata Kiongozi mkarimu, mwenye huruma na asiye na makuu Babu yako Mzee Mwalimu Nyerere hivyo nakuomba na Wewe hata ukija kuwa Msomi wa aina gani au kuwa na mafanikio ya aina gani maishani usipende kuishi kwa Kujionyesha bali muige Mwalimu ambaye hakupenda makuu na aliishi maisha yake tu ya kawaida hadi hivi leo......". Na mpaka leo hii GENTAMYCINE nayaishi hayo maneno ya Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni na hata ukija kuniona au ukiambiwa huyu ndiyo GENTAMYCINE hutoamini na utabaki kushangaa.
 
Aiseeee
 
huko kote mlikuwa mna`guess,ila huu sasa ndio uhaya wenyewe...

Ukinitajia Wahaya au ukiwataja Wahaya nafurahi sana kwani hao ndiyo ' Watani ' zangu wakubwa sana halafu ninawapenda mno kutokana na umakini wao katika maisha, maaria yao makubwa na uwezo wao wa akili / upeo. Nadhani kuna ambao walikuwa ' wakinibipu ' sasa nimeamua ' kuwapigia ' kabisa hivyo nawe unaweza sasa ukajumuika nao katika kuipokea ama kuisikiliza hiyo Simu niliyowapigia.
 
Tatizo watu humu wanapenda kukuchukulia poa sana,ila kwa ufafanuzi huo ,km hawajakuelewa basi hawawezi kukuelewa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…