Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,999
- 23,540
Mara nyingi watu huchanganya kati ya masimp na ma’gentlemen kwasababu ya ufahamu finyu wa hawa watu wanawakilisha haiba gani. Simps na gentlemen ni viumbe wawili tofauti ambao hawafanani hata kidogo katika nature ya matendo yao.
Zifuatazo ni tofauti kati ya simp na gentlemen na ni vema kuzifahamu ili ziweze kusaidia watu kuwatambua na kujitathimini ili kujua yupi ni yupi;
Malengo:
Dhamira na Matendo : Simp huwa anafanya vitu kwa mwanamke au wanawake ili kupata sifa au kuonekana, ridhaa na uhalali au kupata nafasi ya kupiga show,ukarimu wake ni wa kimaslahi zaidi. Gentlemen anafanya mambo yake kwa kujiheshimu na kutenda kwa namna alivyo na sio kupretend. Ukarimu wake unalenga masilahi ya mwanamke anayekutana naye ila hatovuka mipaka yake kumsaidia ataishia pale uwezo na nia yake inapoishia bila kuwa na malengo au dhamira nyingine nyuma ya matendo yake. Mfano, anaweza mpatia pesa msichana na asiwe na haja wala sababu ya kulala nae.
Kujiheshimu: Simp anaweka rehani utu wake,jina lake,na heshima yake ili tu kumfurahisha mwanamke na kumpa anachokitaka. Gentleman anaheshimu wanawake lakini hawezi kuvuka mipaka ya kuweka rehani utu na heshima yake ili kumfurahisha mwanamke au kumridhisha.
Balance katika mahusiano: Simp anapenda kumuendekeza mwanamke na kumjengea mtazamo kuwa yupo chini yake na yupo tayari kutumika au kudhalilika ili mradi tu huyo mwanamke asimuache. Gentleman anamheshimu mwanamke kwa kiwango kile kile cha heshima na utu anachopewa. Kama ikitokea mwanamke akamkosea adabu au kumdharau hawezi ruhusu hayo mahusiano kuendelea.
Msingi wa hisia: Simp hujenga msingi wa hisia zake kwa hofu ya kuachwa,kutojiamini, kujidharau, na kujiona yeye ni second kwa mwanamke na kuwa desperate kupata mahusiano na mwanamke. Gentlemen huendesha fikra za mahusiano kwa kujiamini,kupevuka kiakili,kuheshimu na kujiheshimu, na huchagua kuwa kiongozi wa mwanamke bila kuburutwa.
Mapokezi ya wanawake: simp kwa wanawake huonekana ni dhaifu,mjinga,mzembe na kifaa au kitu cha kutumika kwaajiri ya kutatua matatizo binafsi kama za pesa au place holder wakiwa wanasubiria mtu wanaemhitaji. Gentleman huonekana ni mtu mwenye thamani na wanawanawake humheshimu kwa mipaka yake na principles zake bila kumletea michezo ya kitoto au dharau na kumjaribu kwa lolote lile ambalo wanajua halitakuwa na maslahi kwake.
Kwa kifupi, simp huweka rehani utu na heshima yake ili kupendwa wakati gentleman hukaa na utu wake na kutunza heshima yakena kupendwa kwa namna alivyo.
Vijana acheni kusimp na ujifunze kuwa gentleman.