Gentlemen na simp huchanganywa ila ni watu wawili tofauti

Umenena mkuu hata kama hujamla akileta dharau piga chini, lakini kuna watu wanakomaaga eti kisa hajamla matokeo yake kupoteza pesa na kudharaulika
 
Umesema vizuri sana.👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿
 
Mkuu kwenye usimp huko nitoe mimi mtu fulani jeuri na nina kiburi sana kwa mwanamke sijawahi kufanya kitu kwa lengo la kumridhisha mwanamke ama nipate kile ninachotaka kutoka kwake.
Na kwenye vitu siogopi na sina hofu navyo ni kuchapiwa ni kitu sipendi kutokana na kuwa na effect mbaya sana katika upande wa kiroho.

Nimechangia hayo kutokana na kile nakiona katika mazingira niliopo wapo simps wanachapiwa na wapo gentls wanachapiwa katika angle fulani tunaona wanavyokuwa na jitihada za kuyalinda na kujenga mahusiano yao but same shit every day.Kuna muda hata gentleman nae anakuwa simp akishapenda na hapa ndipo mwanamke anapotake advantage ya kuchanga karata zake vizuri shwaaaa kapita na kichwa

Mkuu kiburi na jeuri na ubinafsi umenikaa sana sasa suala la kujishusha ama kumridhisha mtu huwa sina. Sijui niko kundi gani nabadilisha wanawake tu
 
Kwa mfano unaishi na mwanamke wako saa hii. Umeshamchumbia na mlishafunga ndoa.

Unajipanga kufungua biashara yeye akasimamie na wewe utaiendesha kwa kushirikiana nae.

Anakuja siku anakwambia anataka aka apply kazi somewhere ambapo ana uhakika wa kupata.

Swali gani la kwanza utamuuliza?

Niambie pia hili swala utalichukuliaje kwa urefu na mapana yapi?
 
Sioni sababu ya kumuuliza swali ama kufikiria zaidi hapo ninacho jua hataki kusimamia hiyo biashara. Sitolifikiria kwa mapana zaidi ya kujua hivyo hataki kusimamia anataka kuajiriwa.
 
Sioni sababu ya kumuuliza swali ama kufikiria zaidi hapo ninacho jua hataki kusimamia hiyo biashara. Sitolifikiria kwa mapana zaidi ya kujua hivyo hataki kusimamia anataka kuajiriwa.
So kama mwanaume mipaka yako inasemaje?
 
HAkuna kutumia nguvu kwa mwanamke.
Okay, ipo hivi, wewe kama mwanaume ni jukumu lako pia kumuongoza mkeo kufanya maamuzi sahihi sio kumuachia afanye maamuzi binafsi then mambo ya kizorota uje kusema ni yeye alitaka iwe hivyo then nafasi yako kama kiongozi wa kaya unakuwa umeitenda katika namna gani?
 
Mkuu kumuongoza mwanamke mpaka utumie nguvu ? Ninefungua biashara nikamwambia asimame lakini yeye anataka kuajiriwa nini tena napaswa kufanya hapo na kitu kipo wazi?

Utamlazimisha kufanya tofauti na yy utayari wake haupo hapo upo kwenye kuajiriwa ninacho amini mimi kwenye vitu reasonable utayari wa mtu unakuwa ndio kitu cha kwanza kuzingatia.

Huoni kama ukitumia njia yoyote ambayo itamlazimu yeye kufanya kwa kukuridhisha hawezi akaweka mkazo halafu hapo tunazungumzia pesa mkuu Pesa mkuu nimewekeza halafu mtu asilete umakini huoni kama nitapata sababu ya kumvunja mtu taya ??
 
Naunga mkono hoja
 
Mkuu kumuongoza mwanamke mpaka utumie nguvu ? Ninefungua biashara nikamwambia asimame lakini yeye anataka kuajiriwa nini tena napaswa kufanya hapo na kitu kipo wazi?
Yeah but ni nguvu ya hekima sio ya mwili au maneno matupu yaliyojawa amri tu. Ndio maana nikauliza ili nijue kuwa ulianzaje nae mwanzo na uliweka nini kwenye akili yake awali kabla hajajiamulia yeye bila wewe?
Utamlazimisha kufanya tofauti na yy utayari wake haupo hapo upo kwenye kuajiriwa ninacho amini mimi kwenye vitu reasonable utayari wa mtu unakuwa ndio kitu cha kwanza kuzingatia.
Upo sahihi. Zingatia lakini swala la namna gani umeitroduce swala kwake na wakati gani.
Huoni kama ukitumia njia yoyote ambayo itamlazimu yeye kufanya kwa kukuridhisha hawezi akaweka mkazo halafu hapo tunazungumzia pesa mkuu Pesa mkuu nimewekeza halafu mtu asilete umakini huoni kama nitapata sababu ya kumvunja mtu taya ??
Ukiharibu mwanzoni mwisho hautakuwa mzuri. Unatakiwa kujua namna ya kumshirikisha na kumpangia majukumu na utaratibu kabla hajaona kupwaya kwenye mikakati yako.
 
hiyo ndo point, mimi pia huwa siwezi kulazimisha maamuzi ya mtu eti kisa nionyeshe ugentle
 
Hii ndo sifa ya masimp? Duh, mmewapa jina zuri sana. Hawa wanaitwa mazezeta.
 
Uyasemayo ni sahihi kabisa na ya hekima mkuu naweza kupingana nawe kidogo kutokana na nature ya wanawake kuwa loyal katika hisia zao hii imekaaje kuna muda unaweza kuona mwanamke anaflow na ww vizuri kwa kila unachomwambia ama kumuelekeza tuseme kumuongoza atafuata kutokana na level ya hisia alizonazo kwako.

Hii ndio sababu ilonifanya kuwa na kanuni za kutokutumia nguvu ya aina yoyote hata hiyo nguvu ya hekima Katika kumuongoza siku zote nakuwa natural nitanyoosha maelezo katika hali ya kawaida kabisa kwa mtu mzima haitaji mifano mingi wala maelezo mengi. Sasa utayari wake yeye mwanamke wa kufuata muongozo unajengwa na kiwango cha hisia za kukubali.

Siku zote wanaume tunakuwa kwenye mizani ya kukubalika kwa mwanamke ili aendane na muongozo wako imma uwe mzuri ama mbaya. Mkuu mwanamke akiwa na hisia kubwa kwako utamuongoza katika njia yoyote iwe nzuri ama mbaya haitojalisha ww ni gentleman au simp ataflow tu.
 
hiyo ndo point, mimi pia huwa siwezi kulazimisha maamuzi ya mtu eti kisa nionyeshe ugentle
Mkuu ukiforce mambo huwa yana haribika hasa haya mambo ya uteyari wa mtu mbaya zaidi ni kwa faida yake ama yenu ama ya mahusiano yenu. Pesa zitupe stress na mtu mzima mwenzako nae akupe stress mimi kwangu naona kama laana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…