George Mpole amka la sivyo utapotea

George Mpole amka la sivyo utapotea

Kama anawadai, basi Yuko sahihi. Ila anachokosea ni njia aliyotumia kudai hiyo haki yake,maana anajiumiza yeye. Kama ingekuwa ndio effective way ya kudai chake, basi angekuwa ashapewa.

Benchi linaua sana viwango vya wachezaji. Anaumia yeye.
Upo sahihi,
Ngoja tuone watamalizana vipi bila kuumizana
 
Upo sahihi,
Ngoja tuone watamalizana vipi bila kuumizana
Timu za kiafrica na madeni, ni kama mapacha. Yanga wenyewe kuna kipindi tulikuwa tunatembeza bakuli.

Watu wake wakaribu wamshauri arudi uwanjani
 
Nyie mdanganyeni tu George

Mtoa mada Ana points Sana tu
Amechagua njia hiyo kudai haki yake hata kama sio "star" kama alivyomwita.Mgomo nayo ni njia ya kudai haki maana mpira ni issue ya kisaikolojia hata akirudi kwenye timu hawezi ku-perform vizuri. Ukute yupo analima mananasi mida hii sie tunamwona amepotea
 
Timu za kiafrica na madeni, ni kama mapacha. Yanga wenyewe kuna kipindi tulikuwa tunatembeza bakuli.

Watu wake wakaribu wamshauri arudi uwanjani
Sio kitu cha kujivunia,
Wachezaji wakiwa hawapati stahiki zao hata Morali uwanjani inakua zero ndio maana hatufiki mbali
 
Sio kitu cha kujivunia,
Wachezaji wakiwa hawapati stahiki zao hata Morali uwanjani inakua zero ndio maana hatufiki mbali
Shida sie Waafrika wengi tunaamini zaidi kwenye utimamu wa mwili bila kuangalia upande wa kiakili aka kisaikolojia, unakuta mtu anafanya kitu kwa kuburuzwa huku moyoni ana vitu vinamsonga.

Ila wameshakaa chini na kuyamaliza na amesharudi kwenye timu (taarifa za leo leo hizi)
 
Sio kitu cha kujivunia,
Wachezaji wakiwa hawapati stahiki zao hata Morali uwanjani inakua zero ndio maana hatufiki mbali
Hatujivunii maana kinarudisha nyuma maendeleo ya mpira. Ila Bado haikwepeki uchumi wetu upo chini. Alitaka alipwe hela nyingi, itabidi aende Simba,Yanga au Azam. Ila atleast Azam anaweza akapata nafasi ya kuendeleza kipaji chake.

Ila akienda Simba au Yanga, hatopata nafasi za kucheza mara kwa mara.

Wachezaji wa kitanzania, ukimlipa hela kidogo anagoma kucheza, ukimlipa hela nyingi, anavimba makwapa, analeta ustaa, sterehe kwa wingi then kiwango kinashuka.

Huwaga Natamani pangekuwa na association ya kuwapa msaada wa kimawazo wachezaji wazawa, hii itasaidia kumaintain
 
Watu mnaongea tu humu km mmekula maharage ,hamjui mpole anapitia kitu gani? Katika nyie mnae msema ishawai kukutokea mwisho wa mwezi upate mshahara alafu inapita miezi mitatu hujapewa kitu.?? Hiyo kazi utai ona kazi au mauza uza.

Mtu kudai haki yake anaonekana anavimba kichwa ???? Mtoa mada jiangalie mara mbili

Mpole ndio alikuwa profile ya geita kwa msimu uliopita ,hawana budi kumlipa madai yake na sio kuanza kumsema vibaya

Naungana na mpole coz maisha ya mpira ni mafupi sana , baada ya kustaafu mtakuja kumcheka kwamba hakutumia hela vizuri wakati hata hizo hela alikuwa hapewi.

Tuache uzuzu

Mpole wakomalie wakupe hela zako aiseee, na ww una majukumu kama wengine

Mbona wageni wanalipwa hela zao cash kwann wenyeji tuzungushane ?
 
Suala ni kuwa George Mpole anajiumiza yeye na Wala inayoumia sio Geita..
Halafu kama wengine wanadai na hawafanyi kitu yeye peke yake akilipwa anaweza kutengwa na wenzake ikiwemo kunyimwa pasi..
Ajifunze Kwa Ronaldo
 
Safari hii mashabiki wa simba sijui wataenda na nani kwenye vita ya kugombania kiatu cha ufungaji bora!!
 
Hatujivunii maana kinarudisha nyuma maendeleo ya mpira. Ila Bado haikwepeki uchumi wetu upo chini. Alitaka alipwe hela nyingi, itabidi aende Simba,Yanga au Azam. Ila atleast Azam anaweza akapata nafasi ya kuendeleza kipaji chake.

Ila akienda Simba au Yanga, hatopata nafasi za kucheza mara kwa mara.

Wachezaji wa kitanzania, ukimlipa hela kidogo anagoma kucheza, ukimlipa hela nyingi, anavimba makwapa, analeta ustaa, sterehe kwa wingi then kiwango kinashuka.

Huwaga Natamani pangekuwa na association ya kuwapa msaada wa kimawazo wachezaji wazawa, hii itasaidia kumaintain

" Wakipewa pesa nyingi wanavimba makwapa, starehe kwa wingi, kiwango kinashuka"

Kwa usemi huu ni bora wasipewe kabisa bali wafundishwe kua wazalendo wa kulitumikia Taifa lao kama JKT, huku wageni kwa kua wao wana nidhamu ya pesa ndio walipwe.

Tanzania yangu tuna safari ndefu sana[emoji26]
 
Shida sie Waafrika wengi tunaamini zaidi kwenye utimamu wa mwili bila kuangalia upande wa kiakili aka kisaikolojia, unakuta mtu anafanya kitu kwa kuburuzwa huku moyoni ana vitu vinamsonga.

Ila wameshakaa chini na kuyamaliza na amesharudi kwenye timu (taarifa za leo leo hizi)
Alhamdulillah kama wameyamaliza, hua naumia sana nikionq Mtu anadai Haki yake na hakuna wa kumsikiliza anaishiwa kubezwa na kudhihakiwa,

Umeongelea jambo kubwa sana kuhusu Afya ya Akili wengi tulikua hatutilii maanani hii Afya ya Akili badala yake tulihimizwa Afya ya Mwili, ila sasa uelewa unakua kwa kasi na wasomi wetu wanajitahidi kutoa elimu,

Tunawalaumu wachezaji bure bila kujua mazingira mabovu waliyokua nayo yanaathiri saikolojia yao, nina imani kwenye hizo timu kuna waalimu wa saikolojia kwa wachezaji wake.
 
Tusimfokee Mpole tumuulize kwanza shida ilipo!
Tunapaswa kukumbuka kuwa kuna baadhi ya viongozi kwenye vilabu vyetu ni wadanganyifu na wababaishaji sana!
Kumbuka Mpole alitaka kusajiliwa na vilabu vya Simba, Yanga na Azam lakin kuna mbinu zilitumika pale Geita gold ikiwemo kumuahidi dau zuri, lakini walipofanikiwa kumbakisha na dirisha la usajili likafungwa tayari ahadi zikaota mbawa, mchezaji kabaki anazungushwa!
Tutambue kuwa soka ndio shughuli pekee ya kipato kwa mchezaji na muda wa kustaafu wachezaji ni mfupi sana ukivuta mpaka 38 au 40 ni bahati , hivyo wanachokipata sasa wanachokipata sasa wanawekeza kwa maisha yajayo, kwaiyo mchezaji aliye serious na maendeleo yake hawezi kuvumilia kuzungushwa haki zake!
 
Kosa lake nikudai malipo yake?
Malipo haudai kujificha umekaa kimya!au Hana mkataba? hayo mambo CAF/FIFA wanayataka,peleka kesi huko upate ruhusa ya kukaa home au cheza huku umewashtaki.aache ujinga
 
George Mpole wewe ni kijana uliyevimba kichwa baada ya kuwa mfungaji bora msimu uliopita.

Picha lilianza mechi ya kwanza ya ligi shidi ya Simba, wewe ukajificha kwa makusudi eti hautakuwepo kwa maana eti utokee dakika za mwisho kama 'suprise' kwa Simba na bado hukufanya chochote, hata :shot on target'!

Wenzako wanasafiri kimataifa wewe unajifanya unaumwa ukaacha kwenda! Haya, kwasasa nasikia umejitoa kwenye timu eti kuna pesa unadai!

Hivi hapo Geita ni wewe peke yako tu unadai? Mbona unajifanya maarufu kabla hata ya umaarufu wenyewe?

Kwa akili zako ndogo na finyu unadhani dirisha dogo unaweza kwenda Simba au Yanga? Kwa taarifa yako hata Ihefu huwezi kwenda!

Rudi ongeza bidii kwenye timu, kama ipo ipo tu lakini siyo huku kulazimisha umaarufu, utakuja kuumbuka. Au kama una pasi ya kusafiria na viza nenda Uarabuni ukacheze ligi daraja la pili huko.
Umeshiriki kumuharibu Kwa kulazimisha na kushawishi aonekane mchezaji mkuuubwa wakati wa kawaida Sana. Mpole halisi ni yule anayechezea Taifa stars, hayo mapambo mengine ni kumuongezea asichokuwa nacho.
 
Back
Top Bottom