George Simbachawene, hakupitia JKT?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Ni kweli div 1 wataapply vyuo mara baada ya depo na kuja kuwa maofisa ( maofisa hawaendi lindo kwenye mabenki). Point ya waziri iko hapa.

Nadiriki kusema heading ya huu uzi IMEPOTOSHA.View attachment 1971554
Upo sahihi sana na ndio ukweli huo kwamba Div 1 ni ngumu kuendelea kukaa naye ktk kada hiyo(lindo).

Ila kwa ninachokiona Mh Simbachawene asingetakiwa kuliongelea hili. Nadhani kuna taarifa sio lazima kuzitoa. Hiyo ni mipango ya ndani kwa taasisi au chombo husika.

Licha ya kuleta maswali ktk jamii kama hivi lakini lina kasoro mbili:

1. Ni kutoa furusa na Faida kwa wahalifu wa ndani na nje kujua uwezo wa walinzi wetu ktk sehemu nyeti ikiwa ni pamoja na Bank. Ni RAHISI kupanga namna ya kumu approach hata kwa kutumia kiingereza tatanishi nk.

2. Kwa Askari wenye viwango vya chini vya elimu watajisikia Vibaya (Inferiority) wao, ndugu na hata jamii kwani hata mtu akimuona Askari lindo atamuona ndio wale wa Div......
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
1stborn[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sijui huwa anapataje uwaziri huyu jamaa!
 
Wengi katika madaraka hawakugusa JKT , yuko mwingine kule Zanzibar , hata hivyo namtetea Simbachawene , huyu alikuwa konda wa mabasi ya mikoani pale stendi , isingekuwa rahisi kwake kupita JKT
Alikuwa konda stendi gani?

1. Fundi kutoka FTC Arusha1989-1992 (wakati anamaliza chuo cha ufundi JKT ilikuwa imesitishwa kutokana na sera ya vyama vingi)
2. LLB OUT (sijui ilikuwaje aende kusomea sheria wakati alitakiwa kufanya kazi ya ufundi au kwenda kuomba kusomea digrii ya taaluma ya uhandisi katika fani aliyochukua; lakini haioneshi kama alipitia 'school of law' na kupata leseni ya kuendesha shughuli zinazohusiana na taaluma hiyo kwa mjibu wa sheria)
3. Masters of Public Administration (hii kozi wanapenda kuchukua watu wanaoihitaji uongozi wa kisiasa au umma
4. Hakuwahi kwenda kidato cha sita hivyo kuwa na sifa ya kwenda JKT kwa mjibu wa sheria ilibidi awe ametokea chuoni au kazini. Hata hivyo wakati anamaliza chuo cha ufundi Arusha wanafunzi wote wa kidato cha sita, chuo na kazini kujiunga JKT kwa mjibu wa sheria kulisitishwa na mambi mengi kufungwa kuzuia mihemko ya kisiasa kutokana uanzishwaji wa vyama vingi vya kisiasa.
 
Mkuu umeeleza haswa wasiwasi wangu. juu ya huyu waziri wetu.
Ni wazi qualifications zake juu ya uwaziri hazijafika kiwango.
Na mbaya zaidi anaongoza wizara inayohitaji mtu ambaye toka ujanani anatakiwa awe ametayarishwa na Taifa.
Mbona vijana kama hao wako wengi tu.
Jamaa hajapitia hata JKT, na anawekwa mahali nyeti, hiyo ni dhambi!

Sisi tukia JKT tulitayarishwa kwa majukumu yoyote kitaifa, uwe una Div 1 au uwe mkulima toka kijijini wa kuingia kwa kujitole.

Waswahili husema , mtu anapofungua mdomo, anafungua na mengi yanayomhusu, hatukujua kuwa Simbachawene hapo alipo yuk chini ya viwangoo vile vilivyotarajiwa.
 
wote mnaolalama ni mapolice, kama sio basi ni mama zenu au baba zenu ndo mapolice. Hii imewachoma sana, ukweli unauma eee.

Ila kimsingi kwasasa mambo yamebadilika, simbachawene na serikali yake iache system za kizamani. Sasahivi wasomi ni wengi tunataka nchi iende kisomi.

Waachane na mambo ya la saba na form four failure kazi wapewe wasomi, nchi iende kisomi zaidi , hayo ndo maendeleo.
 
We popoma basi weka mgambo wakalinde na mipaka ya nchi yako, wasomi wale bata!
 
Mijitu mijinga sana ninyi.
Mnapobambikwa na mikesi isiyo na mbele wala nyuma mnalalamika.
Sasa mkipenda kuhudumiwa na watu wasio na akili si mfurahie tu kama ninyi wenyewe hamna akili nzuri!!
 
Mambo mengine ni aibu sana Kama Taifa.Miaka 60 ya uhuru bado tunajivunia ujinga kama sifa ya msingi kwenye kazi ambayo inahitaji weledi.Haya ni makosa makubwa sana na ni aibu kua na kiongozi mwenye mawazo yakizamani hivi.Na ata kama haya ndio mawazo yao haipendezi kuyatoa hadharani wakati kila mtu anapambana kujiendeleza sasa hivi.
 
Mijitu mijinga sana ninyi.
Mnapobambikwa na mikesi isiyo na mbele wala nyuma mnalalamika.
Sasa mkipenda kuhudumiwa na watu wasio na akili si mfurahie tu kama ninyi wenyewe hamna akili nzuri!!
yote hii ni kutokana na kukosa kazi, mnaanza kutamani mpaka na kazi za form four failure.
 
Mkuu alichemka
 
Kwahiyo hizi ndio akili za wapiga meza wote?
 
Inshu kubwa ni kwamba,ukiajili digrii utawalipa mishahara mikubwa na posho kubwa,hivyo Serikali ktk kupunguza mzigo tunaaijili f4.
Kwani tuanaajiri base on merit au expenses. Waswahili wanasema kizuri gharama yaani ili tupate polisi bora wenye weledi lazima tugharamie ivi kwanini tunazipuuza kazi za kitaalamu ie polisi wakati hapohapo hao wanasiasa wanajipa maslahi mazuri na makubwa tena wengine ni la saba kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…