Gerald Hando: Watanzania wanataka sukari, usituambie tusitumie. Asema majibu ya Janabi na Chalamila ni dharau kwa watanzania

Prof Janabi hajasema waache kutumia sukari amesema watu wapunguze kula vitu venye sukari.
It is a big difference.Huyu kajanja hajui analosema.
 
Sukari siyo hitaji muhimu kwa binadamu, bali ni bidhaa ya kawaida tu.

Unaweza usitumie sukari ya kiwandani na bado ukaipata sukari halisi kwenye matunda.

Suala la sukari linakuzwa tu bila sababu!
Wewe unaongea utafikiri huishi Tanzania..!! Wewe unafahamu kwamba watanzania wengi walivyopigika ili wale matunda lazima waandikiwe na daktari.
 
somo la lishe bora ni changamoto hata sasa ndio maana washauri wanaibuka kila siku inanikumbusha ule wimbo maarufu zamani wa mbaraka mwinshehe (Mama chakula bora)
 
Prof Janabi ameongea ukweli mchungu ambao waTanzania wengi hawataki kuusikia......ukitaka kuwateka waTanzania ongea kile wanachopenda kusikia......na ndio maana wajinga wajinga wanathaminiwa na wenye weledi wanatolewa akili........

Janabi hakuzungumza kama mwanasiasa ameongea kutokana na nafasi yake....kwa jinsi anavyoyaona mambo......

Mtu mlevi na mwenye maisha ya hovyo kama Hando hawezi kuelewa kauli za Prof Janabi.......Bali watu waliothirika na vyakula hivyo ndio mashahidi wa hayo......

Alichokiongea Janabi ni kikubwa Sana kwenye akili za mlevi kama Hando........
 
Japo mnamsifia huyo mtangazaji ila anaongea vitu asivyovijua

Swala la sukari kuwa na madhara hafahamu??


Sukari unayotakiwa mwilini ni sukari hii iliyoadimika ??


Ikiwa mgonjwa wa kisukari abatakiwa asile hadi wali au ugali, itakuwa sukari ya viwandani?

Anavyosikia mwili unahitaji sukari anadhani sukari ya Mtibwa sugar
 
somo la lishe bora ni changamoto hata sasa ndio maana washauri wanaibuka kila siku inanikumbusha ule wimbo maarufu zamani wa mbaraka mwinshehe (Mama chakula bora)
Shida tuna watu wengi vilaza

Wanajua kisukari, presha ni magonjwa ya kurithi au yanakuja tu bila sababu kumbe vyakula vya hovyo ndio sababu
 
Reactions: Tui
Hata umeme hauna maana tutumie vibatari tu na solar kupunguza gharama za maisha.- Chalamira aongezee na hili.
 
Hando naanza mfuatilia hawa ndo waandishi wa habari sasa
 
Wewe pimbi unamtukana Hando kakukosea nini?....
Unajua kuwa huyo profesa wako uchwara unaemsifia watu walikula kichwa?...kaa kwa kutulia tu tutamwaga mbigili pasikalike humu
 
"Hando amesema Janabi sio wa kutoa majibu ya sukari nchini, akae Moi apambane na Muhimbili yake.
πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†
MOI siyo MUHIMBILI
MOI sio MNH. Amekosea kidogo. Janabi abaki na MNH yake.
 
DIRA iliyopotea kuipata tena lazma uanze mwanzo. Hayo tunayaita " assistant answers " na mara nyingi utamkwa kuficha UKWELI WA TATIZO.. assistant answers nyingine ni kama kusema " tumelipokea tutalifanyia KAZI, Changamoto, MAMLAKA imesikia, nk" UGUA MAGONJWA YOTE ila sio KUKATA TAMAA.
 

Attachments

  • JamiiForums837618991.jpeg
    51.3 KB · Views: 1
Wewe pimbi unamtukana Hando kakukosea nini?....
Unajua kuwa huyo profesa wako uchwara unaemsifia watu walikula kichwa?...kaa kwa kutulia tu tutamwaga mbigili pasikalike humu
Hahahaha!!!!
Wewe mwaga mbigili Tu mimi nimevaa buti......
 
Kwami lazima kula maandazi?

Asubuhi unaweza ukanywa supu, au mchemsho wa ndizi.
Wewe na Marie - Antoinette ni mapacha.
Ni Watanzania wangapi wenye uwezo wa kunywa supu au mchemsho wa ndizi!!??
 
Mbona sigara inasababisha saratani, lakini inauzwa, ingawa kwa onyo la kiafya?

Kwanza sukari iwepo, lakini kama ina tatizo, iwekewe onyo.

Serikali isijifiche kwenye habari za afya kuhalalisha ukosefu wa sukari.
 
Mm mwenyewe asubuhi wakati naangalia cloud tv waliweka hio clip ya mkuu wa mkoa,sikumwelewa kwa kweli na cloud walivyo MACHAWA wale kina Sam Sasali wakawa kama wanasapoti kauli ya Chalamila,hakika niliwaona ni washenzi sana wale
 
Kitaalam Mimi binafsi naona Janabi yupo sawa ingawa kauli yake ameitoa kipindi ambacho mtumia sukari hawezi kukuelewa kirahisi.
Hando nae Kwa uelewa wake anaweza kuwa yupo sawa
#Mambo ni mengi muda ndio tatizo#
Janabi aliongea kitaalamu lakin mkuu wa mkoa akajibu kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…