Gerald Hando: Watanzania wanataka sukari, usituambie tusitumie. Asema majibu ya Janabi na Chalamila ni dharau kwa watanzania

Gerald Hando: Watanzania wanataka sukari, usituambie tusitumie. Asema majibu ya Janabi na Chalamila ni dharau kwa watanzania

Hando ana akili sana sema kuna muda anaziweka mahali ili tu mkono uende kinywani.

Wakati yupo EFM aliwahi kutoa kauli kuwa maisha ni magumu kwa sababu nchi inakopa sana. Uongozi wa kituo wakampumzisha zaidi ya mwezi, aliporudi akaomba radhi kwa kauli yake.
EFm ndo walikua wa kwanza kujiweka pembeni kwamba yake ni mawazo yake, mfumo wetu badobado sana
 
Kitaalam Mimi binafsi naona Janabi yupo sawa ingawa kauli yake ameitoa kipindi ambacho mtumia sukari hawezi kukuelewa kirahisi.
Hando nae Kwa uelewa wake anaweza kuwa yupo sawa
#Mambo ni mengi muda ndio tatizo#
 
Hando ana akili sana sema kuna muda anaziweka mahali ili tu mkono uende kinywani.

Wakati yupo EFM aliwahi kutoa kauli kuwa maisha ni magumu kwa sababu nchi inakopa sana. Uongozi wa kituo wakampumzisha zaidi ya mwezi, aliporudi akaomba radhi kwa kauli yake.
Nakumbuka ...baada ya hapo hakukaa muda mrefu ndipo akahamia Wasafi
 
EFm ndo walikua wa kwanza kujiweka pembeni kwamba yake ni mawazo yake, mfumo wetu badobado sana
Yote ni kujikomba. Nakumbuka hadi mstaafu akamsifia majizo kule msoga kwamba ni kiongozi mzuri, ikitokea changamoto anaishughulikia haraka.

Katika hali ya kawaida haikutakiwa media kujitenga na kauli ya Hando maana alichoongea ni ukweli kuwa maisha ni magumu na nchi inakopa kweli.

Inawezekana walipata shinikizo kutoka juu kwamba watoe taarifa kwa umma kwamba ule ni msimamo binafsi wa mtangazaji na sio kituo.
Katika hali ya kawaida wangemalizana ndani kwa ndani tu bila kudhalilishana.

Hata baada ya Hando kurudi hakukaa sana ndio akatimkia wasafi kule ana uhuru wa kuongea kiasi.
 
Sukari siyo hitaji muhimu kwa binadamu, bali ni bidhaa ya kawaida tu.

Unaweza usitumie sukari ya kiwandani na bado ukaipata sukari halisi kwenye matunda.

Suala la sukari linakuzwa tu bila sababu!
 
Back
Top Bottom