Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Mbona kadakwa kizembe sana
Haiwezekani aishi kwenye nyumba ambayo haina hata security camera.....kumbuka osama ni jasusi la kimataifa
Kuwa na ulinzi mdogo ni mbunu mojawapo ya kijasusi! Unapokuwa na ulinzi mzito una attract attention.. Just imagine kungekuwa na walinzi wenye mitutu ya bunduki getini na kwenye balcony masaa 24, kila mtu angejiuliza kuna nini humo ndani???
Pia Bin Laden hakutaka watu wengi hata makamanda wake wa ngazi za juu wa Al Qaeda wajue alipo kwani ingeongeza possibility ya taarifa kuvuja..

Mbinu hizi zimemuwezesha aishi kwenye jumba hilo takribani miaka mitano pasipo watu kutilia shaka yoyote! Inasemekana alihamia kwenye jumba hili tarehe 06 June 2006.

Lakini angehamia hapo na walinzi wenye mitutu ya bunduki isingechukua hata miezi miwili wangemshtukia.
Hii inaitwa 'hiding in plain site' (kujificha mahali kweupe). Wakati wamarekani wanahangahika kumtafuta kwenye milima na mapango hakuna ambaye angeweza kudhania bin laden anaishi katikati ya watu wa kawaida mtaani.
Hata VP Joe Biden hakuamini mpaka siku ya mwisho kuwa osama anaweza kuishi humo na aliipinga oparesheni yote kwa asilimia zote, ni mpaka pale SEALs walipoconfirm kuwa wamemdondosha bin laden ndipo VP Biden akaamini.

Kwahiyo mkuu, chagua la bin laden kuwa na ulinzi mdogo na kuishi katikati ya watu lilikuwa ni jambo la kimkakati na akili kubwa sana ya kiusalama.
 
Nimeitikia wito mkuu, wacha nisome kwanza, then ntaongea ya moyoni maana hii habari ya kifo cha osama ina mikanganyiko mingi, wamarekanj nao si wakuwaamin moja kwa moja, hawachelew kukuletea movie zao za Hollywood kwenye maisha ya kawaida..
Hahahahah! Karibu sana kiongozi
 
1473920048309.jpg

hii dunia ni zaidi ya uijuavyo
 
Hizi zinaitwa Fasihi za Kujikweza, huandikwa pote ambapo Babiloni hufanya uovu kisha kutaka kuonekana manguli...
[HASHTAG]#Vietnam[/HASHTAG], [HASHTAG]#Afrika[/HASHTAG], [HASHTAG]#Japan[/HASHTAG], [HASHTAG]#Iraki[/HASHTAG]... Na mara nyingi ni simulizi zilizotiwa chumvi na uongo wa dhati ili kuwafurahisha wasomaji.
 
Nadhani Abu Ahmed al-Kuwait ni sababu kubwa ya kuuwawa Osama.Lakini pia mataifa ya wenzetu vyombo vya usalama vipo kwaajili ya maslahi ya taifa tofauti na Afrika vyombo vya usalama vipo kwaajili ya maslahi ya watawala.
 
Nadhani Abu Ahmed al-Kuwait ni sababu kubwa ya kuuwawa Osama.Lakini pia mataifa ya wenzetu vyombo vya usalama vipo kwaajili ya maslahi ya taifa tofauti na Afrika vyombo vya usalama vipo kwaajili ya maslahi ya watawala.
Word.!! Wenzetu vyombo vya usalama wana uchungu haswa na nchi zao, sio watawala.. Watawala wanakuja na kuondoka, nchi inaishi milele
 
Back
Top Bottom