Geranimo E.K.I.A: Kutoka Makao Makuu ya CIA Langley, Oparesheni Ya Kukamatwa Osama Bin Laden

Roho yaniuma kama ni kweli huyu jamaa kafa
Nataman iwe kama db cooper
 
Na wale waliouwawa kwenye ilo jumba walipelekwa wapi
 
Nadhani Abu Ahmed al-Kuwait ni sababu kubwa ya kuuwawa Osama.Lakini pia mataifa ya wenzetu vyombo vya usalama vipo kwaajili ya maslahi ya taifa tofauti na Afrika vyombo vya usalama vipo kwaajili ya maslahi ya watawala.
Mimi napingana na wewe! Kama unatafuta sababu ya Osama kuuwawa ni yule Mtoto!
 
Na wale waliouwawa kwenye ilo jumba walipelekwa wapi
Miili ya wengine waliouawa (al-kuwait, kaka yake, mkewe na mtoto wa osama) iliachwa pale pale na ilichukuliwa na serikali ya Pakistan na waliizika wao wanadhani! Wale waliosalimika takribani watu 17 (watoto na wanawake) walishikiliwa kwa muda na vyombo vya usalama vya Pakistani lakini walikuja kuachiwa baadae..
 
Mimi napingana na wewe! Kama unatafuta sababu ya Osama kuuwawa ni yule Mtoto!

Al Kuwait asingekuwa na mawasiliano na nduguzake ndhani CIA wangekosa mahali pa kuanzia.Kumbuka Al Kuwait ndiye kamanda aliyekuwa na mawasiliano na Osama moja kwa moja hata dogo alikiri kutomfahamu Al kuwait.

Kiherehere cha kuongea na simu ni turning point.
 

The Bold Achaana na huyu Yericko aliumia sana kuumbuliwa kule Fb baada ya kuchukua andiko lako ndiomaana amekua na hasira na wewe.

tunajua wewe sio Mtumishi wa CIA wala FBI ila umepitia tu taarifa zake na wewe kutuletea kitu kizima kwa pamoja

huyu anatafuta tukuonekana nae anajua

kwa nnavyo mfahamu Yericko nisingweza kupoteza pesa yangu kununua kile kitabu chake cha ushushu na sijui na ujinga gani najua amecopy habari za kwenye movie tu.

awauzie manyum...b.u wenzake wasiomjua
 

Yericko tunaokujua wala hatukushangai hata kidogo na hizi sarakasi zako hapa
 
Nice nimeipenda hii mkuu. Ila nilidhani details za hii operesheni bado ni siri...Mfano daktari wa chanjo aliishia wapi mwisho wa siku kama identity yake ilijulikana tayari?
Daktari ambaye alitoa chanjo (Shakil Alfridi) alijulikana na alikamatwa mwaka mwaka 2012 kama sikosei, na kwa muda mrefu sana alishikiliwa na Serikali ya Pakistan katika magereza yao..
Kushilkiliwa kwake kulileta tension sana kati ya Marekani na Pakistan mpaka ikafikia hatua Marekani wakapunguza misaada ya kijeshi kwa Pakistan ili tu kuwapa presha Pakistan..

Marekani walikuwa wanadai kuwa Dk. Shakil Alfridi anapaswa kupongezwa na kupewa ulinzi kwa kuwa amesaidia kumtia nguvuni gaidi namba moja duniani na sio kuwekwa gerezani.
Lakini Pakistan walidai kuwa kitendo cha Dk. Shakil Alfridi kushirikiana na kusaidia taifa la kigeni kufanya ushushushu na oparesheni ya kijeshi ndani ya Pakistan kilikuwa ni kitendo cha Uhaini na kamwe hawawezi kumuachia.
Huu mzozo ulikuwa mkubwa sana na sijui waliumalizaje baadae..
 
Mkuu hongera sana, wewe ni bonge la muandishi naamini kuna ambao unawaita Manguli hawakufikii hata chembe. Endelea kufanya kazi nzuri kama hizi na mimi naomba usiache kunitag kila unapoweka vitu safi kama hivi.

Asante,
Kambitza.
 
Dah mkuu mimi ndio maana nimeona nikae kimya tu! Maana ameweka zaidi ya video tatu tofauti alafu kila moja anasema ndiyo hiyo imetafsiriwa 'neno kwa neno'.. Ukiifungua video si kweli.!

Nimeona nikae kimya tu!
Mkuu The Bold;

Ili kukata mzizi wa fitina safari nyingine weka na marejeo kabisa au disclaimer kidogo chini ya makala zako hizi angavu mf. Makala hii inatokana na files za FBI (declassified), habari za Wikipedia, documentaries mbalimbali hasa ****, kitabu cha **** n.k. Tuna tatizo kubwa la plagiarism katika nchi hii kwa sababu elimu yetu kimsingi imesimikwa katika kukopi kopi (kudesa) mambo ya watu bila kutoa credit sawasawa. Yote kwa yote u mwandishi mzuri sana na whether umetafsiri mahali unastahili hongera kubwa sana. Hata ile kukaa tu na kutafsiri na kupangilia lihabari refu kama hili ni kazi ngumu. Nitaanza kukufuatilia kuanzia sasa.
 
Ni sawa mkuu! Ila Dogo alikua anamjua Al Kuwait, ndo alimpa mafunzo ya mwisho! Kama Dogo asingekamatwa Al Kuwait asingejulikana, by the way Osama na watu wake walijitahidi kujificha kadri walivyoweza!
Ukiona mtu anakimbizwa usimsifie kwa mbio zake, msifie pia anayemkimbiza....Kama team imefungwa, usimlaumu kipa au beki, inawezekana walikutana na Washambuliaji bora kabisa kuliko uwezo wa Mabeki au Kipa!!!
 
Nashukuru sana mkuu! Pia ntafanyia kazi ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…