ze-dudu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 17,640
- 22,748
Roho yaniuma kama ni kweli huyu jamaa kafaKuwa na ulinzi mdogo ni mbunu mojawapo ya kijasusi! Unapokuwa na ulinzi mzito una attract attention.. Just imagine kungekuwa na walinzi wenye mitutu ya bunduki getini na kwenye balcony masaa 24, kila mtu angejiuliza kuna nini humo ndani???
Pia Bin Laden hakutaka watu wengi hata makamanda wake wa ngazi za juu wa Al Qaeda wajue alipo kwani ingeongeza possibility ya taarifa kuvuja..
Mbinu hizi zimemuwezesha aishi kwenye jumba hilo takribani miaka mitano pasipo watu kutilia shaka yoyote! Inasemekana alihamia kwenye jumba hili tarehe 06 June 2006.
Lakini angehamia hapo na walinzi wenye mitutu ya bunduki isingechukua hata miezi miwili wangemshtukia.
Hii inaitwa 'hiding in plain site' (kujificha mahali kweupe). Wakati wamarekani wanahangahika kumtafuta kwenye milima na mapango hakuna ambaye angeweza kudhania bin laden anaishi katikati ya watu wa kawaida mtaani.
Hata VP Joe Biden hakuamini mpaka siku ya mwisho kuwa osama anaweza kuishi humo na aliipinga oparesheni yote kwa asilimia zote, ni mpaka pale SEALs walipoconfirm kuwa wamemdondosha bin laden ndipo VP Biden akaamini.
Kwahiyo mkuu, chagua la bin laden kuwa na ulinzi mdogo na kuishi katikati ya watu lilikuwa ni jambo la kimkakati na akili kubwa sana ya kiusalama.
Nataman iwe kama db cooper