Gereza la Hazwa

Gereza la Hazwa

STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

UKURASA WA HAMSINI NA SABA

TULIPO ISHIA UKURASA WA HAMSINI NA SITA
"Hahahaha hahahaha hahahahahah" Kani alicheka sana tena sana, wanaume hao walipata hasira mno yule black alikishusha kibao chake ili amzabe nacho mwanaume huyo alikishusha wakati kinaelekea eneo la shavu alijikuta anapokea ngumi kama tano kwenye uso wake alishangaa kwa sababu aliambiwa Kani alikuwa dhaifu sana kweli alivyo mwangalia Kani alikuwa amesimama vile vile akiwa anavuta sigara yake kubwa huku mlinzi mmoja akiwa analifuta koti lake la suti.

ENDELEA.............................

Kilichokuwa kinatokea pale hakuna ambaye alikuwa anakiamini kilikuwa kinashangaza, yule black alipigwa bila kujua kapigwa na nani, alijipanga na kurudi tena kwa spidi pale ambapo alikuwa amesimama Kanivasi alijipinda na moja ya teke safi kuelekea kwenye shingo ya mtu ambaye yeye hakuwa na muda nae zaidi ya kuendelea kuivuta sigara yake bila pupa kabisa, black alishtuka na kuguna kwa sauti baada ya kupokea ngumi nzito ya goti kabla hajatua chini alipigwa mateke mazito na wanaume wawili kwenye kifua chake kiasi kwamba alitoa damu na kukaa chini kifua chake kilikuwa kinawaka moto kana kwamba amepigwa na nyundo hapo ndipo walipojitokeza wanaume wanne waliokuwa na asili ya kichina wakiwa kwenye suti zao nzuri sana nyeusi (code ya dunia black suit).
"Hawa watu umewatoa wapi?"
"Hahahahahah haya sio mambo ambayo yanakuhusu wewe hapo yatetee maisha yako" baada ya kuongea tu hivyo Kanivasi alienda kukaa kwenye kiti chake na kugeukia walipo wanaume hao akihitaji kuushuhudia huo mchezo, alisogea mwarabu mmoja kati ya wale watatu ambao walikuja pamoja na kuwasogelea wale wachina alidhani atapigana nao wote alishangaa kila mtu anampisha alibakia mchina mmoja tu mbele yake huyo ndiye aliyetakiwa kupigana naye na sio wote kama alivyokuwa anahisi. Alisogea kwa kasi ya ajabu huku akiirusha kadi yake uelekea kwa huyo mchina hiyo kadi ilidakwa kwa vidole viwili na kuvunjwa ulipigwa mkono wa wanaume ila hazikuisha hata dakika mbili yule mwarabu alikuwa chini uso wake ukiwa umetapakaa damu mwarabu mwenzake alitaka kuingilia hilo jambo lakini alizuiwa.
"Stooooop" yule black alitamka kwa sauti huku akicheua damu, alikuwa ameshasimama tayari, wote waligeuka kumtazama yeye alimpa ishara Kanivasi asimame.

"Hatujaja hapa kuleta ugomvi nawewe tumekuja hapa kufanya biashara nawewe"
"Hata mimi najua ni suala la biashara limekuleta na hivyo ndivyo watu tunaofanya biashara kubwa tumavyoweza kutambuana tunapokuwa tunahitaji kufanya biashara kubwa"

"Ok ila hawa watu umewatolea wapi?"
"Hiyo ndiyo biashara iliyo kuleta?"
"No nimeshangaa tu raia wa kawaida kwenye nchi yako unalindwa sana namna hii"
"Wewe hapo ndo unaniita mimi raia wa kawaida?"
"Yes, wewe ni raia wa kawaida tu kwenye nchi yako kuna viongozi wengi sana lakini hawana uwezo wa kuwa na watu wa namna hii"

"Hahahahah hahahaha sasa kama ningekuwa wa kawaida unahisi wewe ungefanikiwa kunipata?"
"Mara ya Kwanza baada ya kulisikia jina lako nilihisi itakuwa ni kijana mhuni mhuni tu mtaani cha ajabu tunafika ndani ya hili jiji tunakuta mitandao mingi ya kijamii inasifia kile ambacho umetoka kukiongea hiyo ndiyo sababu tumeweza kukupata kirahisi tu tofauti na tulivyokuwa tumefikiria"

"Wewe haujanipata kirahisi ni mimi tu nimeamua, unaweza ukaishi ndani ya nchi hii hata mwaka kama nikiamua usinipate wala kuniona basi hautaweza mpaka unakufa, nambie hiyo biashara ambayo imekuleta kwangu"

"Tunahitaji kujua taarifa za rafiki yako ambaye nadhani anaitwa Alen na wewe unamjua hivyo ila kwa sisi tunamjua kama Zakaria" hiyo sentensi ilimfanya Kanivasi atoe kitambaa chake mfukoni jasho lilikuwa limeanza kumtiririka usoni kwake ilikuwa ni mara ya pili kwa watu tofauti analisikia jina la rafiki yake ambaye alimjua kwa jina la Alen ukiwa ni muda mfupi tu tangu amsaliti rafiki yake huyo, alikumbuka siku ya mwisho ambayo alimuona rafiki yake akiwa chini ya dimbwi la damu za kutosha, kisha akakumbuka lile tukio la kumbaka mke wa Alen kisha muda mfupi baadae kuja kupata taarifa kwamba ameuawa yeye na mtoto wake, mwili ulimsisimka mno.

"Nyie ni akina nani"
"Sisi ni watu kutoka Dubai"
"Mnataka nini na unaiitaje hiyo biashara?"
"Ni biashara kwa sababu ina malipo"
"Wewe una uwezo wa kunilipa mimi?"
"Vipi unatuona wa kawaida sana?"
"Unanipotezea muda nambie huo mpango wa biashara"
"Kuna milioni miatano kwa taarifa ndogo tu ambayo utatusaidia"
"Ipi?"
"Tunahitaji taarifa chache za huyo mtu" Kanivasi aliwaza kidogo kisha akamkonyeza mlinzi wake mmoja ambaye alisogea sehemu aliyokuwepo yule black, alipewa namba za akaunti ya benki, aliinamia kwenye simu yake ya mkononi ndani ya dakika moja tu Kanivasi aliinyanyua simu yake baada ya kusikia sauti ya meseji kuingia,alitabasamu kwa mbali baada ya kuona muamala wa shilingi za kitanzania milioni miatano haikuwa pesa ndogo, ilikuwa ni pesa nyingi sana kwa taarifa chache tu ambazo zilihitajika, hakuwa na undugu na Alen tena alishamuuza na leo alikuwa anammaliza kabisa kwa kutoa taarifa zake zingine.

"Ni kipi mnataka kukijua kwake?"
"Tunataka kujua huyo mtu ulikutana naye vipi na alipotea vipi?"
"Baada ya hapo sitataka swali lingine kutoka kwenu na nitataka mnipatie taarifa huyu mtu ni nani hasa maana nahisi simjui kabisa kwa lolote lile"
"Sawa haina shida".

"Ni usiku mmoja ambao ulikuwa una baridi sana ndani ya Arusha nikiwa natoka kwenye harakati zangu za uchimbaji wa madini, nilitoka dukani kununua zangu mkate na kinywaji ili usiku wangu uishe salama wakati naanza kurudi nyumbani nilisikia kuna mtu anagugumia pembeni mwa kibanda kimoja hivi basi nikasogea karibu na pale nilimuona mtu mmoja ambaye alikuwa amekauka sana midomo yake akiwa anahitaji kama ni msaada,nilimpatia mkate na kinywaji alifakamia sana kana kwamba hakuwa amegusa kitu chochote kile kwa zaidi ya mwaka mzima. Huo ndo ulikuwa mwanzo wangu wa kukutana na yule mtu niliishi naye kama ndugu yangu nikampleka mpaka machimboni ili naye aweze kupata chochote kitu.

Ndipo siku moja alipo lalamika kwamba anaumwa wakati tupo ndani ya shimo alifanikiwa kupelekwa hospitalini ambako ndiko huko alikokuja kupotelea, kwa sababu mimi nilikuwa ndiye rafiki yake basi nilikamatwa kwa kudhaniwa kwamba nimemtorosha na madini lakini baada ya uchunguzi wa muda mrefu nilikutwa sina hatia nikatoka ndani ya jela, hapo ndipo nilipo ielewa njaa nilipigwa na njaa vibaya sana, siku moja nikiwa nimejikatia tamaa nilipigiwa simu ambayo ilinipa tumaini jipya la maisha kunihitaji nifike Dar es salaam simu ilitoka kwa Alen sikuamini kile kitu mpaka nilipokuja kukutana naye tena. Alikuwa na maisha mazuri mno nilijitahidi sana kutaka kujua huo utajiri kautolea wapi lakini hakuwahi kunipa jibu lolote lile, na huo ndio ukawa mwanzo wangu wa kuyaishi maisha mazuri sana ndani ya jiji hili, lilifanyika kosa moja tu ambalo ndilo lilisababisha mambo ya kutisha kutokea baada ya mimi kuiposti picha yake kwenye mitandao ya kijamii.

Ndani ya dakika moja tu ile picha ilifutika na muda mfupi tu nilivamiwa na watu wakiwa wanamhitaji huyo mtu na ndipo hapo nilipokuja kuambiwa kwamba huyo mtu anaitwa Zakaria Mansour nilishangaa mno kwa sababu ni miaka mitano nilikuwa namjua ila niliambiwa sijui chochote kuhusu yeye. Walikuwa wanaume 12 ndio waliokuja kumchukua baada ya kunipa taarifa kwamba ni komando wa kutisha na kiumbe cha ajabu anatafutwa kwa kuhusika na mauaji ya watu 150 zikiwemo familia mbili zenye watu 50, walimkamata na kuondoka naye sijui kama walimuua au vipi nadhani pesa yako imeishia hapo unaweza kwenda na tusitafutane tena"

"Nashukuru sana kwa maelezo yako hukutaka swali ila maelezo hayajajitosheleza hivyo ni lazima niulize swali, waliweza vipi kumkamata kiwepesi sana hivyo mtu ambaye ameua watu 150?"

"Mhhhhhhh kama sio msaada wangu sidhani Kama wangemkamata kwa sababu walikuwa wanamuogopa sana, ni wanaume wa kazi 12 hivyo mimi ndiye niliye mlegeza kwa sababu aliniamini sana, nilifanikiwa kumshuhudia kwa dakika chache tu na nilikiri wazi kwamba yule sio mwanadamu ni jini lile. Hiyo ndiyo sababu mimi kwa sasa nimewatafuta watu wa kutisha sana namna hii hata kama atafanikiwa kupona huko waliko enda naye kama akirudi basi nitammaliza mimi mwenyewe kwa sababu atakuwa na kisasi namimi hahahahahahahahahha" alijigamba sana nadhani kwa jambo ambalo hata yeye mwenyewe hakuwa anajua anacho kifanya.

"Hao walio mchukua ni akina nani?"
"Mhhhh hiyo ni taarifa ambayo siwezi kukupa kirahisi sana namna hii tafuta wakati mwingine kama tukikutana tutaongea kwa urefu mkono wako bado ni mfupi sana kwenye utoaji milioni miatano unataka kila taarifa, sasa namimi nakuuliza maswali machache kama makubaliano yetu ya mdomoni yalivyo fanyika. Huyo mtu anatafutwa kwa kuua hiyo familia, ni familia ipi hiyo na huyo Zakaria ni nani hasa mbona anaimbwa sana?" Kanivasi hakuwahi kupewa taarifa za kutosha za Zakaria hata mara ya kwanza hakupewa taarifa zozote za kumhusu huyo mtu.

"Hata sisi hapa wote watatu hatuijui historia ya huyo mtu tuna taarifa zake chache sana kwa sababu inadaiwa hata nchi yake watu wenye taarifa zake hawafiki hata watatu unahisi sisi tutazipatia wapi? Mtu anaishi kwa siri sana sehemu yoyote ile duniani utazipatia wapi taarifa zake? Sisi hapa tupo kumtafuta huyo mtu kwa namna yoyote ile tumeagizwa na mtu ambaye ndiye pekee anaye ishi kwenye hiyo familia iliyo uawa na Zakaria ilikuwa familia yake, ana uchungu sana na huyo mtu ila kwa taarifa chache ambazo zipo ni kwamba sio mwanadamu kama walivyo wengine anadaiwa kuwa mtu wa kipekee sana kwenye huu ulimwengu, anadaiwa kuwa na dunia yake kwenye ulimwengu wa watu hatari hivyo lengo la kuja Tanzania ni baada ya upatikanaji wa taarifa za uwepo wake na familia yake yeye, tunataka kujua yuko wapi kwa sasa ama familia yake baada ya hapo tufanye kazi yetu ya kumkamata" maneno ya huyo mtu yalimfanya Kanivasi ashushe pumzi kwa nguvu, alimwangalia mtu huyo hakujibu chochote aliingia kwenye gari yake na kuwaamuru watu wake waondoke ndani ya hilo eneo.

Niseme tu 57 inatia nanga hapa tukutane mpaka wakati ujao tena

Bux the story teller
Chao.

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Ndo kwanza tumefika nusu ya simulizi yetu ambayo utakuwa unaipata kwenye hii thread lakini kama utahitaji kuisona yote mpaka mwisho basi unaipata Kwa shilingi 2500 tu za kitanzania.

Unaweza kutuma Kwa namba

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA SITINI NA MOJA

TULIPO ISHIA UKURASA WA SITINI
"Ni hadithi ndefu sana na ya kutisha mno, huyo mtu ndiye pekee ambaye alikuwa anasadikika kupona kwenye familia yake, huyu pekee ndiye alisadikika kuwa masalia ya familia ya AMADOU MBAYE, huyu ndiye aliyebakia pekee yake kwa taarifa za mwanzo hata yeye anajua hivyo lakini kuna ndugu yake mwingine wa siri sana ambaye hata yeye hamjui kabisa. Hawa ndugu wawili wote kwa ujumla wanamtafuta sana Zakaria Mansour japo mmoja anajua kwamba wapo wawili na mwingine hajui kama wapo wawili anajua kama yupo pekeake. Hawa watu wote wawili mimi nimebahatika kukutana nao ni mijitu ya kutisha sana, sio binadamu kama watu wengine sina uhakika kama nao walizaliwa kawaida kama ilivyo kwa wanadamu wengine nawaogopa sana, hawa wote wanamtafuta sana Zakaria kwa sababu yeye ndiye ambaye aliua familia yao yote ya watu 50 bila kuacha mtu hata mmoja al.........."

"Whaaaaaaaaaaaaaat" mheshimiwa raisi alishangaa mno alishangaa tena, aliuliza kwa sauti kubwa sana alikuwa anapewa taarifa hizi nyeti sana kwa mara ya kwanza alikuwa anazisikia.

ENDELEA...................
Joto kali ndilo lililo muamsha kutoka usingizini, alihisi huenda kuna mtu anachoma vyuma jirani ila baadae alikuja kugundua kwamba huenda kwa nje ni jua lilikuwa limewaka hivyo alikuwa na uhakika kwamba hiyo lazima ilikuwa ni asubuhi jua limechomoza, Zakaria aliamka na kukaa chini, alivuta kumbukumbu za matukio ambayo aliyafanya kwa watu ambao aliambiwa ni waasi alitikisa kichwa chake kuonekana kwamba alikuwa anasikitika sana juu ya hilo jambo, alijilaza chini kwenye chumba hicho ambacho kilikuwa kichafu kupita maelezo akawa anaangalia juu ambako kulikuwa na zege nzito sana.

Aliamka baada ya kusikia hatua za mtu zikisogelea hilo eneo, mlango ulifunguliwa kuna mwanaume aliingia na kumpa ishara ya kumfuata kisha akafungwa macho yake, alikuwa makini sana kwenye kila eneo ambalo alikuwa anapita, alikubali kufanya kila ambacho alikuwa anaagizwa na mheshimiwa raisi kwa sababu aliambiwa kwamba yeye ni mwanajeshi wa taifa hili ni lazima alipiganie taifa lake lakini kitu ambacho kilikuwa kinamshangaza sana ni kwanini awe anafichwa asione kinacho endelea? Alikuwa na mashaka kiasi chake kwenye moyo wake sana ndiyo sababu alianza kujiongeza. Alikuwa ni msomi au injinia mkubwa sana kwenye usanifu wa majengo na uchoraji pamoja na uandishi kwake lilikuwa ni tatizo dogo sana anapokuwa kwenye eneo lenye majengo ya kutisha kama angepata bahati ya kulitazama kwa zaidi ya dakika tano alikuwa na uwezo wa kulichora lote kama lilivyo.

Alishtuka baada ya kuona anapanda kwenye ngazi eneo ambalo lilionekana kuwa wazi kabisa, hakujiuliza mara mbili kwamba alikuwa anapanda kwenye helikopita hilo alilielewa vizuri hakuwa na shida nalo.

"Tunaelekea wapi?" Aliuliza swali lakini hakuna ambaye alimjibu chochote kile, safari yao iliendelea wakiwa juu angani mpaka walipofika sehemu ambayo ilikuwa na nyumba chache za kuhesabu ambazo yalikuwa kama magofu, walimtoa kitambaa na kumshusha wakati wanatembea naye wale ambao walikuja naye walianza kupiga makelele huku wakiondoka na kukimbia lile eneo, hakuna kitu ambacho yeye aliweza kukifanya alibaki anawashangaa sana, mbele yake alitokea mwanaume mmoja ambaye alijifunika mwili mzima, kiunoni kwake alikuwa na bastola mbili pamoja na upanga kwenye mkono wake ukiwa ndani ya ala yake, alisogea eneo ambalo alikuwepo Zakaria na kumtazama juu mpaka chini.

"Nina uwezo wa kukuua kwa risasi ila baada ya kuipata historia yako nasikia wewe ni mtu hatari sana unapokuwa na upanga kwenye mkono wako au pete ambazo inadaiwa huwa unazificha sehemu yenye usalama sana sasa leo nataka nione nawewe unavyoweza kuukwepa upanga ambao umekufanya uzitoe nafsi za watu wengi sana hapa duniani, Una kazi ya kuyatetea maisha yako kuanzia muda huu tunavyo ongea hapa"

"Ndio hicho tu ambacho wale vijana wamekimbia sana namna hiyo kwamba wanakuogopa au"
"Kuna watu tunatisha na kuogopwa sanae ndio maana tunakimbiwa sana sehemu yoyote ile ambayo tutaonekana"
"Mhhhhhh unaweza ukanipa sababu ya kukufanya wewe kuvamia hili eneo maana inaonekana kama ulikuwa unanisubiri ni mimi nifike hapa?"

"Yes nimekusubiri sana tena sana kuhusu kwamba mimi ni nani hakuna anayeweza kujua, hata wewe hauna huo uwezo hahahahahahahahahha"

"Sawa, Leo ngoja nikufunze kwa kukuonyesha upande wa pili wa dunia jinsi unavyofanya kazi" Zakaria baada ya kumaliza kuongea mwanaume huyo aliuchomoa upanga kutoka kwenye ala yake alicheka mara moja tu na kuondoka kwa nguvu mno alikuwa anatembea zig zag kuelekea ile sehemu ambayo alikuwepo Zakaria alivyo karibia alidunda chini kwa mguu wake mmoja alipanda hewani kidogo na kujigeuza, upanga wake ulikuwa unaelekea usawa wa shingo ya Zakaria baada ya kufika alipo mwanaume huyo aliushusha huo upanga kwa nguvu alirusha ngumi yake ya mkono wa kushoto pamoja na huo upanga alidhamiria kufanya kitu kibaya sana, alishangaa upanga wake na ngumi vikipita kwa wepesi sana. Alikuwa amemkosa mtu huyo na kupiga hewa alihakikisha kwa kuungalia upanga wake vizuri haukuwa hata na tone la damu kwenye suruali yake hakuwa na mkanda ambao kwa mara ya kwanza ulikuwepo hapo hakuamini hicho kitu.

Aligeuka na kuona mwanaume mwenzake amesimama akiwa ameangalia upande wa pili na mkononi mwake akiwa na mkanda ambao bila shaka ulikuwa ni wake, akazirudisha kumbukumbu zake vizuri wakati anafika hilo eneo mwanaume huyo aliinama na kujiburuza chini kwa kumdaka eneo lake la kiuno hapo ndipo ulipo tolewa huo mkanda kisha alisukumizwa na ngumi nzito ya mbavu, hapo ndipo alipo elewa aliugusa ubavu wake wa kushoto ulikuwa unauma sana sasa alijipa uhakika kwamba alicho kiwaza hapo kilikuwa ni cha kweli.

"Kwa mara ya Kwanza kwenye maisha yangu nimedhalilika leo, sijawahi kutumia hili pigo nikamkosa mtu na kuishia kudhalilishwa namna hii hapana hapana" aliongea kwa sauti huku akiwa anakimbia kuelekea pale alipo Zakaria mwanaume ambaye alikuwa na spidi Kali sana linapokuja suala la urushaji wa mikono, aliruka double kick moja nzuri sana upanga ukiwa unazungushwa, alibahatika kuingiza mguu wake kwenye kifua cha mwanaume huyo ambacho kilikuwa kigumu sana lakini hata yeye alipokea ngumi nzito sana kwenye kifua chake alihisi kama Moto unawaka mateke mazito yalikuwa yanakuja kwenye uso wake alilikwepa moja lakini moja lilimpata akiwa ameufunika uso wake alidondoka chini na upanga ukamdondoka, alitaka kukimbia alihisi kama mkono umeshikwa na ganzi baada ya kujaribu kuzuia buti ambalo alilivaa mwanaume huyo alitoa miguno sana, Zakaria alizunguka kwa spidi kali akawa kama amejipiga mtama mwenyewe alikuwa anashuka na goti la shingo hakuufikisha mguu wake alipigwa na ngumi nzito kwenye goti lake mpaka yeye mwenyewe alisikilizia maumivu makali na kurudi nyuma.

Nyuma ya mheshimiwa Salem Malek walikuwa wamesimama wanaume watano wakiwa ndani ya kombati nzito za Jeshi, hata yeye Salem Malek aliwashangaa wanaume hao kati ya hao watano yeye alimjua kijana mmoja tu ambaye alikuwa ni mlinzi wake wa kawaida wa siku nyingi tu, akiwa hapo chini aliyakumbuka maneno ya Razack Hakim kwamba yeye analindwa na makomando ishirini wa siri ambao huwa wana hakikisha anakuwa salama muda wowote ule na kwa bahati nzuri huwa hawajui kama huyo mtu sio mheshimiwa raisi wanajua ndo yule raisi wao hiyo ndiyo kete ya mhimu zaidi ambayo alikuwa nayo yeye kwenye mkono wake hakuweza kuamini hicho kitu alijikuta anafurahi sana kuwa na watu wa kazi namna hii kwenye maisha yako ni kitu kikubwa sana japo alishangaa mno kwanini siri nzito kama hizo yeye anakuwa hazijui na watu kama hao wanajuaje kwamba atakuwepo eneo fulani kwa muda fulani? Na kama wapo ishirini hao wengine wako wapi na wanaishi sehemu ipi ambayo yeye haijui ndani ya nchi yake? Alijivuta na kuegemea moja ya ukuta hapo alitaka kushuhudia mchezo wa wanaume hapo akiwa zake pembeni bila wasiwasi.

Zakaria aliwaangalia kwa umakini walikuwa wanaume watano, miili ilikuwa imejaa mno hata sura zao zilisadiki kuwa ni watu wa kazi sana.

"Ni aibu sana raia wa kawaida kama wewe kumgusa kiongozi mkubwa kama huyu hilo kosa binafsi mimi kama mimi siwezi kukusamehe kabisa labda kama wengine watakusamehe ila sio mimi" hiyo kauli ilismhtua na kumshangaza sana Zakaria, hakuelewa neno kiongozi limeingiaje hapo, alitamani sana kutoa nyembe zake hadharani mbele ya hao watu ila alijionya sana kufanya hicho kitu, alijikuta yupo chini baada ya kufanikiwa kukwepa ngumi za moja ya hao wanaume ambaye alikuja kwa kushtukiza sana lakini alikutana na ngumi za mwanaume mwingine ambaye alikuwa nyuma ya huyo wa kwanza aliye mkwepa, alisimama vizuri na kujipangusa nguo zake mbaya ambazo zilikuwa kwenye mwili wake, alicheka sana Zakaria na kuikunja mikono yake vizuri, alipiga hatua zake kwa spidi Kali sana alimpiga yule mwanaume ambaye alimpiga ngumi zile za mwanzo, alitua na, zaidi ya ngumi kumi kwenye kifua chake ambacho kilivunjwa vibaya mwanaume yule akawa anatoa damu nyingi sana, kilikuwa ni kitendo cha sekunde kadhaa tu hata wale wanaume wengine walibaki wanashangaa kitu kilicho tokea, alijiviringisha ili kumpiga mwingine na mateke yake mazito aliotewa ngumi mbili kwenye mbavu zake kabla hajatua chini alipokea buti zito tumboni na kudondokea pembeni, sehemu ambayo alidondokea kulikuwa na ule upanga ambao alikuwa nao Salem Malek ambaye kwa wakati huo alikuwa anatazama pambano hilo kwa pembeni yake kidogo, Zakaria aliushika upanga huo na kusimama nao taratibu.

"Kimbieni mkiwa bado mna nafasi" aliongea kwa sauti kali ambayo ilimuumiza kila mtu aliyekuwa hapo kuna wengine waliziba masikio yao, wanaume ambao walikuwa wamesimama wima kupambana naye walikuwa wanne tu basi mmoja wao hakuwa hata na uwezo wa kusimama, licha ya kutoa hilo onyo hakuna mtu ambaye aliondoka,upanga ulikuwa kwenye mkono wake moja yati ya silaha zake pendwa sana alijua kitu ambacho alikuwa anaenda kukifanya baada ya hapo. Yule kiongozi wa wale wanaume aliiweka mikono yake kwapani alitaka vijana wake wamalizane na mtu ambaye alitishia usalama wa mtu ambaye wao walijua kwamba ni raisi wao wote watatu walikuwa wanakuja kwa kasi sana Zakaria alifumba macho na kuyafumbua wanaume hao walikuwa wamefika kitu alicho kifanya kilikuwa kinatisha sana mguu wa mwanaume mmoja ulishuka chini baada ya kuurusha kwa nguvu ukakutanishwa na upanga alilia sana kuushuhudia mguu wake ukiwa chini kwenye vumbi na yeye amekaa kando yake alipigwa buti la uso alishindwa kuelewa kama apige makelele au atulie tu kusikilizia maumivu yake.

Wapili aliruka sarakasi ambayo ilimponza, wakati anatua mwanaume alisogea nyuma hatua kadhaa na kuja ghafla aliuvuta mkono wa mtu huyo na kuuachia alimpa nafasi ya kurusha ngumi mwanaume huyo aliingia mtegoni kweli aliirusha, mkono ulipitiwa na upanga kabla hajafanya chochote alikoswa shingo upanga ulizama kwenye bega lake ukachomolewa kwa nguvu naye hakuwa na mkono, wa tatu alikuwa anakuja kwa mahesabu sana ila bahati mbaya ilikuwa upanda wake wakati anaruka juu kabla hajatua chini mwanaume alimfuata huko huko alimpiga ngumi ya mguu na kumfanya mtu huyo apoteze uelekeo akadondoka vibaya eneo ambalo upanga ulikuwepo mkononi shingo yake ikadondokea sehemu hiyo maisha yake yaliishia hapo hapo, Zakaria aliinua macho yake na kumtazama yule mwanaume ambaye alionekana kuwa kiongozi wao alikuwa anakuja kwa hasira sana akiwa amechukia vibaya mno vijana wake walifanywa kitu kibaya sana.

Upanga ulirushwa kwa nguvu ulizama kwenye mguu wake lakni hakujali alifika hapo na kurusha ngumi kumi mfululizo, Zakaria alizipangua ila zilimuingia sana tu akiwa anashangaa alipokea teke la kichwa alimanusura adondokee uso alijigeuza na kusimama, alijinyoosha mkono wake vizuri, wanaume waliupanga mkono zilipita dakika kama mbili wakiwa wanapimana uwezo wao upanga ulikuwa bado haujachomolewa kwenye mguu wa yule mwanaume, Zakaria aliuchomoa kwa nguvu ule upanga alihitaji kumaliza kazi ila alisita baada ya kusikia sauti kali

"Stooooop" ni sauti ambayo iliwashtua sana wote wawili.

Unadhani atakuwa nani huyo? Binafsi 61 naweka nukta hapa tukutane tena wakati ujao

Bux the story teller

Chao.
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA SITINI NA MBILI

TULIPO ISHIA UKURASA WA SITINI NA MOJA
Upanga ulirushwa kwa nguvu ulizama kwenye mguu wake lakni hakujali alifika hapo na kurusha ngumi kumi mfululizo, Zakaria alizipangua ila zilimuingia sana tu akiwa anashangaa alipokea teke la kichwa alimanusura adondokee uso alijigeuza na kusimama, alijinyoosha mkono wake vizuri, wanaume waliupanga mkono zilipita dakika kama mbili wakiwa wanapimana uwezo wao upanga ulikuwa bado haujachomolewa kwenye mguu wa yule mwanaume, Zakaria aliuchomoa kwa nguvu ule upanga alihitaji kumaliza kazi ila alisita baada ya kusikia sauti kali

"Stooooop" ni sauti ambayo iliwashtua sana wote wawili.

ENDELEA.........................
"Yes hiyo ndiyo sababu inayo mfanya huyo mtu anatafutwa sana na hao wana familia wawili"
"Aliua watu wote hao kwenye hiyo familia kisa nini?"
"Sikuwahi kuijua sababu ya msingi sana mpaka siku ambayo nilikutana na kijana mwingine wa hiyo familia ndiye ambaye alienda kuniambia ukweli wa mambo upoje, huyo ndiye aliye nipa tahadhari juu ya huyo mtu, nasikia ni jitu la ajabu sana kuwahi kuishi duniani"

"Kwamba ulikuja kumtafuta mtu ambaye humjui?"
"Yes"
"Kwanini iwe hivyo?"

"Mheshimiwa nadhani wewe ni mkuu wa nchi unaelewa namna unavyofanya kazi kuna vijana wako unaweza ukawapa kazi na wakaifanya bila kuuliza kama inahusu nini kikubwa kama tu wewe umewapa wao ruhusa ya kukifanya hicho kitu"

"Bado sijaielewa pointi yako ya msingi ni ipi hasa"
"Namaanisha kwamba nilitumwa tu kuja kumtafuta mtu huyo ila sikujua kwanini na alifanya kitu gani kikubwa juzi hapo ndipo nimeweza kujua kwamba kwanini anatafutwa sana na hao watu"

"Nipe maelekezo taratibu nikuelewe na unijibu maswali yangu vyema, kama huyo mtu anamtafuta sana kiasi hicho kwa kudai kwamba aliuliwa familia yake ina maana kuna sababu kubwa sana nyuma yake haiwezekani mtu aue familia nzima ya watu zaidi ya 50 bila kuwa na sababu ya msingi"

"Inasemekana kwamba hiyo familia ilimuulia familia yake pia"
"Familia yake ipi?
"Huko Libya inasemekana alioa na alipata mke pamoja na mtoto wa kiume"

"Mhhhhhhhhhh"
"Yes hicho ndicho kitu ambacho kilileta yote haya"

"Sababu ilikuwa ni ipi mpaka wafikie hatua ya kuua familia yake?"

"Inasemekana huyo mtu uliandaliwa mpango wa serikali tangu akiwa ni mdogo sana aliibiwa kwenye familia yake na kwenda kutengenezwa ambapo ameishi kwenye maeneo mengi sana duniani ili kupata hayo mafunzo, mafunzo hayo yalikuwa yanaongozwa na watu wawili, waziri mkuu wa zamani pamoja na muidhini mkuu wa dawa za binadamu nchini Libya, watu hao wanadaiwa kwamba walimlisha sumu kwamba mheshimiwa raisi alikuwa anashirikiana na magaidi hivyo walimuua kwahiyo walimuandaa yeye ili kwenda kupambana na magaidi hao ambao walikuwa wamejimilikisha eneo la kusini mwa Libya ambako ndiko iliko hifadhi kubwa ya mafuta ndani ya nchi.

"Aliambiwa ana kazi kubwa mbili ya kwanza ilikuwa ni kuwateketeza hao magaidi na ni kazi ambayo aliimaliza kwa muda wa siku moja tu lakini baadae akaja kupewa kazi ya pili ambayo alitakiwa kumkamatisha tajiri mmoja ambaye ndiye huyo AMADOU MBAYE ambaye watoto wake ndio hao wanamtafuta, kwenye kuifanya kazi hiyo alifanikiwa kupata ushahidi wa biashara haramu ambazo alikuwa anazifanya mzee huyo ila kuna kitu ambacho hakukijua kwamba alikuwa amechezewa mchezo kila alichokuwa anakifanya kilikuwa kinafuatiliwa, alimuua mtoto mdogo zaidi wa mke wa kwanza wa mzee huyo na mzee huyo alitumiwa video hiyo ambayo ilirekodiwa na mtu mmoja kwa siri sana na walio fanya hilo tukio walikuwa ni wale wawili ambao ndio walimpa hiyo kazi aliyo takiwa kuifanya"

"Ile hali ilipelekea mpaka familia yake kutekwa na kuuliwa yeye akatumiwa video, hapo ndipo mtu ambaye alikuwa mlezi wake alipo mpa historia yake kwamba yeye ni nani, maamuzi aliyo yafanya ni kuua familia nzima ya yule mzee pamoja na wale viongozi wawili ambao ndio walikuwa waratibu wa kila kitu. Baada ya hilo tukio hakutaka kujihusisha na mambo yoyote yale tena ndipo alipo amua kuja Tanzania kwa siri sana akijifanya kama ni maskini mkubwa ila baadae tena alipotea bila kujulikana kaenda wapi, nilipewa kazi ya kuja kumtafuta huku Tanzania ambayo mpaka sasa mmenikuta nikiwa naendelea nayo".

"Kwenye moja ya makosa makubwa ambayo aliyafanya ni kuhisi ameua familia nzima bila kujua kuna watu wawili waliweza kuishi na hao ndio wanao mtafuta kwa udi na uvumba na yeye hajui hilo jambo lakini pia anatafutwa sana na umoja wa nchi za magharibi kwa sababu huyo aliye muua alikuwa moja ya viongozi wakubwa sana ndani ya ECOWAS, hata nchi yake inamtafuta sana kwa kosa la kuweza kuwaua makomando na wanajeshi wapatao 100 jumla na watu wa ile familia inakuwa ni 150, hivyo ni mtu ambaye anasakwa kila Kona na sio sisi tu" maelezo ya Qade yalimfanya mheshimiwa raisi amtazame sana kwenye macho yake kumaanisha kwamba alikuwa anamskiliza kwa umakini sana.

"Inawezekanaje mtu akupe siri nzito sana za ndani namna hiyo halafu akakuacha hai?"
"Hakunipa siri zote lakini hata hivyo sina hata uwezo wa kumkimbia mtu mwenyewe"

"Kivipi"
"Ni siri nzito sana sehemu ambazo nimefanikiwa kuzipata ila huyo mtu ambaye naye ana hizo taarifa ni mtu ambaye ananijua naamka saa ngapi nalala saa ngapi, nina uhakika hata muda huu anajua kwamba nipo hapa ndio maana nimekwambia hawa watu ni hatari na wanatisha kuliko hata unavyo fikiria wewe"

"Anaitwa nani huyo mtu ambaye unamuogopa sana namna hiyo hata mbele ya raisi?"
"Aami Amadou Mbaye ndiye jina lake"

"Ndiye nani hasa huyo?"
"Kwa madai yake anadai yeye ndiye mtoto wa mwisho zaidi wa huyo mzee na ndiye mtoto tajiri zaidi wa huyo mzee" Qader alinyamaza kumwangali mheshimiwa ambaye ni wazi alionekana kwamba kichwa chake hakipo sawa, stori alizokuwa anapewa zilikuwa zinamchanganya sana.

"How (kivipi)?"
"Huyu alikuwa ni mtoto wa mke mdogo zaidi wa huyo tajiri ambaye alikuwa amemuoa kwa siri sana huko Libya hata familia yake ilikuwa haijui kabisa kuhusu hilo jambo, inasemeka ndiyo ilikuwa roho ya mzee huyo ndio maana alimpatia utajiri mkubwa sana"

"Huyo kijana mama yake yuko wapi"
"Nilivyo ongelea hilo suala na kumuuliza kuhusu mama yake alinipiga vibaya sana mpaka nikapoteza fahamu na kujikuta nikiwa ufukweni kabisa mwa bahari"

"Umeonana naye kwa mara ya mwisho lini"
"Jana"
"Jana?"
"Yes, muda ambao nimekamatwa na kuletwa hapa nimetoka ufukweni ambako ndiko aliko nitupa baada ya kunizimisha"

"Anapatikana wapi?"
"Unahisi kama ningejua anako patikana angeweza kuniacha hai mpaka muda huu?"
"Sasa ulikutana naye wapi?"
"Huyu ndiye mtu ambaye aliniokoa kule Bukoba"

"Alikuokoaje wakati ulikimbia?"
"Yes nilikimbia lakini nilikuwa kwenye hali mbaya sana nisingeweza kufika mbali baada ya kupigwa na huyo mlinzi wako, nikiwa kwenye sekunde zangu ambazo nilijua ni za mwisho ndipo mtu huyo alipofika na gari yake na kunichukua"

"Ina maana alikuwa anajua kila kilichokuwa kinafanyika"
"Hapana"
"Sasa alijuaje kama upo kule?"
" Ni hadithi ndefu sana mheshimiwa ambayo hadi wewe unaingia humo ndani"

"Mhhhhhhh kijana kuwa makini sana na mdomo wako kabla sijaukata huo ulimi wako"
"Nadhani kama ningekuwa naongea kitu ambacho ni uongo nisinge endelea kwa maumivu uliyo nipa sasa utachagua wewe kama utanisikiliza au utanipuuzia ila usije ukanilaumu baadae nahitaji baada ya japa uniache na maisha yangu nataka nikimbie niende mbali sana na huu ulimwengu wa kawaida"

"Kuna kitu gani ambacho kinaonekana cha siri sana ambacho hata mimi naonekana nahusika bila hata kujijua?"

"Unamfahamu kijana wako ambaye anaitwa Jiti Maalimu?" Raisi alishtuka sana baada ya kusikia jina hilo, huyo ni kijana ambaye alimtafuta kwa siri kubwa mno na ambaye alikuwa anajua ni mkurugenzi wa usalama wa taifa sasa lilikuwa ni jambo la ajabu kukuta hizo taarifa nyeti anazo mtu wa nje kabisa ambaye hata hamhusu.

"Umesema nani?"
"Jiti Maalimu"
"Nambie ukweli wewe ni nani?" Aliongea kwa sauti kali akichomoa bastola kwenye kiuno chake alikuwa anapewa hadithi ambazo zilikuwa zinamchanganya sana

"Sasa hicho kiumbe ambacho nimekwambia kinamtafuta Zakaria, huyo mtu amnbaye aliniteka, huyo mtu ambaye nimekwambia ndiye aliyenipa hadithi ya maisha ya Zakaria kwa undani ndiye huyo ambaye wewe unamjua kama Jiti Maalimu.

"Nooooooo ,noooooo hapana hapana hapana hahahahahaha hahahahahah" mheshimiwa raisi alikuwa kama kapandwa na kichaa hakutaka kuamini hicho kitu alibisha na kwa upande wake alikuwa na asilimia zote miamoja kulikataa hilo jambo.

Qader alipewa onyo kwamba ikitokea siku akatoa hiyo siri ambayo alikuwa anaimwaga hapo basi alikuwa ana dakika chache sana za kuendelea kuishi na leo alikuwa amemwaga mboga na ugali akasahau kwamba angeutunza kwa baadae angepata mboga zingine. Unahisi nini kinajiri? Naweka nukta ukurasa wa 62 tukutani wakati ujao tena.

Wasalaam
Bux the story teller.
 
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
AGE: 18+

UKURASA WA SITINI NA TATU

TULIPO ISHIA UKURASA WA SITINI NA MBILI
"Sasa hicho kiumbe ambacho nimekwambia kinamtafuta Zakaria, huyo mtu amnbaye aliniteka, huyo mtu ambaye nimekwambia ndiye aliyenipa hadithi ya maisha ya Zakaria kwa undani ndiye huyo ambaye wewe unamjua kama Jiti Maalimu.

"Nooooooo ,noooooo hapana hapana hapana hahahahahaha hahahahahah" mheshimiwa raisi alikuwa kama kapandwa na kichaa hakutaka kuamini hicho kitu alibisha na kwa upande wake alikuwa na asilimia zote miamoja kulikataa hilo jambo.

ENDELEA...........................
"Mimi sidanganyi huo ndio ukweli wenyewe, nishakuwa mateka wako sina haja ya kukupatia uongo wowote tena"

"Hili jambo limewezekaka vipi?"

"Mr president hii dunia hakuna kitu ambacho kinashidikana, hii dunia wanaishi watu wenye akili kuliko hata unavyo fikiria wewe, mtu akikuzidi akili kidogo tu basi anaweza kukuendesha anavyotaka yeye hata kama una madaraka makubwa kiasi gani"

"Aliweza vipi kufanya kitu cha hatari kama hicho?"

"Kwa sababu huyo Jiti Maalimu ndiyo ilikuwa silaha pekee ya kufanikisha mambo mengi sana ya siri"

"Kivipi?"

"Unakumbuka kwamba wewe ulimuita kwa siri sana huyo Jiti Maalimu ili umpe kazi?" Mheshimiwa jasho lilimtoka, kidogo hakuamini kama siri zake za ndani huwa zinatoka kiwepesi sana nje namna hiyo hilo lilikuwa ni jambo la hatari sana

"Enhe"

"Basi huyo ndiye aliyetumika kujua kila kitu"

"Sasa unasemaje huyo bwama mdogo ndiye Jiti Maalimu?"

"Jiti Maalimu alishakufa muda mrefu sana"

"Whaaaaaat"
"Yes huo ndio ukweli"

"How is this possible?(Hii inawezekanaje?)"

"Ni story ndefu kidogo"

"Tell me" alifoka kwa sauti kubwa sana mheshimiwa raisi wa Tanzania ajulikanaye kama Alan Mwaiponela.

"Kwenye harakati zangu za kuweza kumtafuta Zakaria nilifanikiwa kumjua usalama wa taifa mmoja ambaye ndiye Jiti Maalimu, baada ya kumjua nilianza kufanya mpango wa kumuweka kwenye mkono wangu kwa sababu nilijua lazima atakuwa na baadhi ya taarifa za ndani ya idara ya usalama ambazo zingenisaidia sana kwenye kazi yangu hivyo niliandaa mtego ili niweze kumpata. Siku moja alikuwa kwenye moja ya kumbi za starehe huko Tabata ndipo nilipofanya mpango wa kumkamata na kumpeleka kwangu".

"Nilimtesa sana akawa amekiri kwamba atanipa ukweli wa kila kitu baada ya mateso kumzidia ila ghafla tu alianza kuniuliza kama nina familia, nilishangaa kwa sababu haikuwa ikihusiana na jambo lolote na kile ambacho nilikuwa nimemuuliza pale ila alisisitiza sana hivyo alinionya kwamba huo muda niutumie kwenda kuificha familia yangu na niachane a hayo mambo ambayo nilikuwa nayafuatilia"

"Sikuamini hicho kitu mpaka alipoanza kunipa ukweli wa mambo kuhusu huyo mtu Zakaria, kwa stori zake sio mwanadamu ni jini lile na kauli ambayo aliniambia ni kwamba ni yeye tu pekee ambaye ana uwezo wa kumpiga huyo mtu na hakuna mwanadamu mwingine yeyote ambaye anaweza kusimama mbele ya Zakaria, nilimshangaa mno ila wakati ule namshangaa alifanya kitu cha ajabu sana ambacho mpaka leo kila nikikumbuka huwa natetemeka mno"

"Alitoa kichupa kidogo sana kweye mfuko wake na kunywa kisha akajimwagia kweye kidonda ambacho nilimtoboa toboa lile eneo lilijiunga pale pale akakata mpaka kamba ngumu ambazo nilikuwa nimemfunga pale kiwepesi sana, lile jambo mpaka leo huwa sielewi liliwezekanaje ba......"

"Stooooop"
"Ushaniona mimi mtoto unaanza kunisimulia mambo ya kwenye movie za magharibi sio, hivi unahisi kwamba unaongea na mhuni mwenzako hapa" ulimwengu ulikuwa unamshangaza sana Alan Mwaiponela mheshimiwa raisi hivyo aliona kama mtu huyo alikuwa anamuenjoy tu kitu ambacho alikiongea hakukuwa na ukweli wowote ule

"Mimi nakujibu maswali ambayo umeniuliza na uhalisia wake sasa kama hutaki kuniamini basi unaweza ukaniacha tu mimi niende"

"Endelea"

"Kile kitu kilinishangaza sana alidai kwamba kwenye nchi hii hakuna mtu ambaye anaweza kusimama mbele yake akafanikiwa kumaliza hata dakika kadhaa tu akiwa hai zaidi zaidi yeye ndiye anaweza kumpiga Zakaria, hicho kitu kilinishangaza sana kwani sikuamini kama Tanzania ina viumbe vya kutisha sana kiasi hicho, alizidi kunishangaza zaidi baada ya kuniambia kwamba yeye sio Jiti Maalimu"

"Hapo alinishangaza mara mbili baada ya kuivua sura ya Jiti Maalimu usoni ilikuwa ni sura ambayo sikuwahi kuishuhudia kwenye maisha yangu yote, su,ra ya kijana mdogo tu wa kiarabu sikuweza kuivumilia yale mambo yake ya kutisha nilizimia pale pale. Baada ya kuzinduka ndipo alipo nisimulia kitu kilicho mfanya yeye kuwa Jiti Maalimu na ukweli wa maisha yake yote"

"Hata yeye wakati anamtafuta Zakaria hapa Tanzania alibahatika kukutana na huyo kijana Jiti Maalimu, hakuwa na haraka naye baada ya kugundua kijana huyo ni usalama wa taifa, alicho kifanya ni kuanza kumfuatilia kijana huyo kuanzia historia nzima ya maisha yake na kila alichokuwa anakifanya hivyo alifanikiwa kumjua kuanzia alipo zaliwa mpaka siku ya mwisho ambayo alikuwa anaendelea kuiishi"

"Baada ya kumjua kijana huyo ndipo alipo amua kumuua kijana huyo na kuitumumia sura yake kama hakuna kilicho tokea, na huo ndio muda ambao wewe hapo ulimchukua kijana huyo ili akusaidie kwenye kazi zako za siri za kufuatilia kuhusu hili jambo"

"Usiniambie kwamba huyo kijana ndiye ambaye mimi nilimuita ikulu kumpa kazi"

"Yes ndiye huyo huyo wala hujakosea"

"Fu*****k"

"Baada ya wewe kumpatia hiyo kazi hilo lilimrahisishia yeye kupata taarifa kwa wepesi sana kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa"

"Na hiyo ambayo umesema historia yake ni ipi"

"Mhhhhhh ni mtu wa usalama na yeye"

"Kutoka wapi?"

"Ndani ya nchi ya URUSI"
"Hey whaaaaat the f***"*k"

"Yes"

"Kwao ni wapi"

"Libya na Senegal"

"Sasa Urusi inaingiaje tena hapa"

"Yule ni jasusi kutoka katika shirika la kutisha la kijasusi duniani la FSB ambalo zamani lilikuwa linajulikana kama KGB"

"Hahahahahah hahahahahah haya mambo yanawezekana vipi?"

"Baba yake ndiye aliye mpeleka huko ili akafanye kazi zake na kumlinda"
"Ebu nipe hiyo Stori nzima bado sielewi nini kinacho endelea" Qader hakuwa na namna zaidi ya kunisimulia historia nzima ya maisha ya Aami Amadou Mbaye ambaye mheshimiwa raisi alikuwa anafikria kwamba ni Jiti Maalimu mpaka mtu huyo alivyo ingia kwenye mikono ya CIA na kufanikiwa kutoroka, mpaka ujio wake kwa mara nyingine na namna alivyoshindwa kumsaidia baba yake mpaka anafia kwenye mikono ya Zakaria. Ni Stori ambayo ilimshangaza sana mambo hayakuwa mepesi kama yeye alivyokuwa anayachukulia mambo yalikuwa mazito sana na yalihitaji moyo wa uvumilivu sana kuyakamilisha au kuyashuhudia, mheshimiwa alivuta pumzi ndefu sana na kuuliza.

"Nawewe kwanini alikuonya kuhusu huyu mtu?"

"Mimi nilifanya kosa kwa kukurupuka sana ambalo mtu huyo hawezi hata kukusamehe kama kweli basi mimi nitakuwa mtu ambaye nitauawa kikatili sana tena sana"

"Kwanini?"

"Mimi ndiye niliye muua mtoto wake na mke wake kwa familia ambayo alikuwa ameianzisha hapa Tanzania"

Bado tupo ndani ya GEREZ LA HAZWA, sehemu ya 63 tupumzike kidogo wakati mwingine tena utatupatia majibu sahihi.

Bux the story teller

Chao.
 
Back
Top Bottom