STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA HAMSINI NA SABA
TULIPO ISHIA UKURASA WA HAMSINI NA SITA
"Hahahaha hahahaha hahahahahah" Kani alicheka sana tena sana, wanaume hao walipata hasira mno yule black alikishusha kibao chake ili amzabe nacho mwanaume huyo alikishusha wakati kinaelekea eneo la shavu alijikuta anapokea ngumi kama tano kwenye uso wake alishangaa kwa sababu aliambiwa Kani alikuwa dhaifu sana kweli alivyo mwangalia Kani alikuwa amesimama vile vile akiwa anavuta sigara yake kubwa huku mlinzi mmoja akiwa analifuta koti lake la suti.
ENDELEA.............................
Kilichokuwa kinatokea pale hakuna ambaye alikuwa anakiamini kilikuwa kinashangaza, yule black alipigwa bila kujua kapigwa na nani, alijipanga na kurudi tena kwa spidi pale ambapo alikuwa amesimama Kanivasi alijipinda na moja ya teke safi kuelekea kwenye shingo ya mtu ambaye yeye hakuwa na muda nae zaidi ya kuendelea kuivuta sigara yake bila pupa kabisa, black alishtuka na kuguna kwa sauti baada ya kupokea ngumi nzito ya goti kabla hajatua chini alipigwa mateke mazito na wanaume wawili kwenye kifua chake kiasi kwamba alitoa damu na kukaa chini kifua chake kilikuwa kinawaka moto kana kwamba amepigwa na nyundo hapo ndipo walipojitokeza wanaume wanne waliokuwa na asili ya kichina wakiwa kwenye suti zao nzuri sana nyeusi (code ya dunia black suit).
"Hawa watu umewatoa wapi?"
"Hahahahahah haya sio mambo ambayo yanakuhusu wewe hapo yatetee maisha yako" baada ya kuongea tu hivyo Kanivasi alienda kukaa kwenye kiti chake na kugeukia walipo wanaume hao akihitaji kuushuhudia huo mchezo, alisogea mwarabu mmoja kati ya wale watatu ambao walikuja pamoja na kuwasogelea wale wachina alidhani atapigana nao wote alishangaa kila mtu anampisha alibakia mchina mmoja tu mbele yake huyo ndiye aliyetakiwa kupigana naye na sio wote kama alivyokuwa anahisi. Alisogea kwa kasi ya ajabu huku akiirusha kadi yake uelekea kwa huyo mchina hiyo kadi ilidakwa kwa vidole viwili na kuvunjwa ulipigwa mkono wa wanaume ila hazikuisha hata dakika mbili yule mwarabu alikuwa chini uso wake ukiwa umetapakaa damu mwarabu mwenzake alitaka kuingilia hilo jambo lakini alizuiwa.
"Stooooop" yule black alitamka kwa sauti huku akicheua damu, alikuwa ameshasimama tayari, wote waligeuka kumtazama yeye alimpa ishara Kanivasi asimame.
"Hatujaja hapa kuleta ugomvi nawewe tumekuja hapa kufanya biashara nawewe"
"Hata mimi najua ni suala la biashara limekuleta na hivyo ndivyo watu tunaofanya biashara kubwa tumavyoweza kutambuana tunapokuwa tunahitaji kufanya biashara kubwa"
"Ok ila hawa watu umewatolea wapi?"
"Hiyo ndiyo biashara iliyo kuleta?"
"No nimeshangaa tu raia wa kawaida kwenye nchi yako unalindwa sana namna hii"
"Wewe hapo ndo unaniita mimi raia wa kawaida?"
"Yes, wewe ni raia wa kawaida tu kwenye nchi yako kuna viongozi wengi sana lakini hawana uwezo wa kuwa na watu wa namna hii"
"Hahahahah hahahaha sasa kama ningekuwa wa kawaida unahisi wewe ungefanikiwa kunipata?"
"Mara ya Kwanza baada ya kulisikia jina lako nilihisi itakuwa ni kijana mhuni mhuni tu mtaani cha ajabu tunafika ndani ya hili jiji tunakuta mitandao mingi ya kijamii inasifia kile ambacho umetoka kukiongea hiyo ndiyo sababu tumeweza kukupata kirahisi tu tofauti na tulivyokuwa tumefikiria"
"Wewe haujanipata kirahisi ni mimi tu nimeamua, unaweza ukaishi ndani ya nchi hii hata mwaka kama nikiamua usinipate wala kuniona basi hautaweza mpaka unakufa, nambie hiyo biashara ambayo imekuleta kwangu"
"Tunahitaji kujua taarifa za rafiki yako ambaye nadhani anaitwa Alen na wewe unamjua hivyo ila kwa sisi tunamjua kama Zakaria" hiyo sentensi ilimfanya Kanivasi atoe kitambaa chake mfukoni jasho lilikuwa limeanza kumtiririka usoni kwake ilikuwa ni mara ya pili kwa watu tofauti analisikia jina la rafiki yake ambaye alimjua kwa jina la Alen ukiwa ni muda mfupi tu tangu amsaliti rafiki yake huyo, alikumbuka siku ya mwisho ambayo alimuona rafiki yake akiwa chini ya dimbwi la damu za kutosha, kisha akakumbuka lile tukio la kumbaka mke wa Alen kisha muda mfupi baadae kuja kupata taarifa kwamba ameuawa yeye na mtoto wake, mwili ulimsisimka mno.
"Nyie ni akina nani"
"Sisi ni watu kutoka Dubai"
"Mnataka nini na unaiitaje hiyo biashara?"
"Ni biashara kwa sababu ina malipo"
"Wewe una uwezo wa kunilipa mimi?"
"Vipi unatuona wa kawaida sana?"
"Unanipotezea muda nambie huo mpango wa biashara"
"Kuna milioni miatano kwa taarifa ndogo tu ambayo utatusaidia"
"Ipi?"
"Tunahitaji taarifa chache za huyo mtu" Kanivasi aliwaza kidogo kisha akamkonyeza mlinzi wake mmoja ambaye alisogea sehemu aliyokuwepo yule black, alipewa namba za akaunti ya benki, aliinamia kwenye simu yake ya mkononi ndani ya dakika moja tu Kanivasi aliinyanyua simu yake baada ya kusikia sauti ya meseji kuingia,alitabasamu kwa mbali baada ya kuona muamala wa shilingi za kitanzania milioni miatano haikuwa pesa ndogo, ilikuwa ni pesa nyingi sana kwa taarifa chache tu ambazo zilihitajika, hakuwa na undugu na Alen tena alishamuuza na leo alikuwa anammaliza kabisa kwa kutoa taarifa zake zingine.
"Ni kipi mnataka kukijua kwake?"
"Tunataka kujua huyo mtu ulikutana naye vipi na alipotea vipi?"
"Baada ya hapo sitataka swali lingine kutoka kwenu na nitataka mnipatie taarifa huyu mtu ni nani hasa maana nahisi simjui kabisa kwa lolote lile"
"Sawa haina shida".
"Ni usiku mmoja ambao ulikuwa una baridi sana ndani ya Arusha nikiwa natoka kwenye harakati zangu za uchimbaji wa madini, nilitoka dukani kununua zangu mkate na kinywaji ili usiku wangu uishe salama wakati naanza kurudi nyumbani nilisikia kuna mtu anagugumia pembeni mwa kibanda kimoja hivi basi nikasogea karibu na pale nilimuona mtu mmoja ambaye alikuwa amekauka sana midomo yake akiwa anahitaji kama ni msaada,nilimpatia mkate na kinywaji alifakamia sana kana kwamba hakuwa amegusa kitu chochote kile kwa zaidi ya mwaka mzima. Huo ndo ulikuwa mwanzo wangu wa kukutana na yule mtu niliishi naye kama ndugu yangu nikampleka mpaka machimboni ili naye aweze kupata chochote kitu.
Ndipo siku moja alipo lalamika kwamba anaumwa wakati tupo ndani ya shimo alifanikiwa kupelekwa hospitalini ambako ndiko huko alikokuja kupotelea, kwa sababu mimi nilikuwa ndiye rafiki yake basi nilikamatwa kwa kudhaniwa kwamba nimemtorosha na madini lakini baada ya uchunguzi wa muda mrefu nilikutwa sina hatia nikatoka ndani ya jela, hapo ndipo nilipo ielewa njaa nilipigwa na njaa vibaya sana, siku moja nikiwa nimejikatia tamaa nilipigiwa simu ambayo ilinipa tumaini jipya la maisha kunihitaji nifike Dar es salaam simu ilitoka kwa Alen sikuamini kile kitu mpaka nilipokuja kukutana naye tena. Alikuwa na maisha mazuri mno nilijitahidi sana kutaka kujua huo utajiri kautolea wapi lakini hakuwahi kunipa jibu lolote lile, na huo ndio ukawa mwanzo wangu wa kuyaishi maisha mazuri sana ndani ya jiji hili, lilifanyika kosa moja tu ambalo ndilo lilisababisha mambo ya kutisha kutokea baada ya mimi kuiposti picha yake kwenye mitandao ya kijamii.
Ndani ya dakika moja tu ile picha ilifutika na muda mfupi tu nilivamiwa na watu wakiwa wanamhitaji huyo mtu na ndipo hapo nilipokuja kuambiwa kwamba huyo mtu anaitwa Zakaria Mansour nilishangaa mno kwa sababu ni miaka mitano nilikuwa namjua ila niliambiwa sijui chochote kuhusu yeye. Walikuwa wanaume 12 ndio waliokuja kumchukua baada ya kunipa taarifa kwamba ni komando wa kutisha na kiumbe cha ajabu anatafutwa kwa kuhusika na mauaji ya watu 150 zikiwemo familia mbili zenye watu 50, walimkamata na kuondoka naye sijui kama walimuua au vipi nadhani pesa yako imeishia hapo unaweza kwenda na tusitafutane tena"
"Nashukuru sana kwa maelezo yako hukutaka swali ila maelezo hayajajitosheleza hivyo ni lazima niulize swali, waliweza vipi kumkamata kiwepesi sana hivyo mtu ambaye ameua watu 150?"
"Mhhhhhhh kama sio msaada wangu sidhani Kama wangemkamata kwa sababu walikuwa wanamuogopa sana, ni wanaume wa kazi 12 hivyo mimi ndiye niliye mlegeza kwa sababu aliniamini sana, nilifanikiwa kumshuhudia kwa dakika chache tu na nilikiri wazi kwamba yule sio mwanadamu ni jini lile. Hiyo ndiyo sababu mimi kwa sasa nimewatafuta watu wa kutisha sana namna hii hata kama atafanikiwa kupona huko waliko enda naye kama akirudi basi nitammaliza mimi mwenyewe kwa sababu atakuwa na kisasi namimi hahahahahahahahahha" alijigamba sana nadhani kwa jambo ambalo hata yeye mwenyewe hakuwa anajua anacho kifanya.
"Hao walio mchukua ni akina nani?"
"Mhhhh hiyo ni taarifa ambayo siwezi kukupa kirahisi sana namna hii tafuta wakati mwingine kama tukikutana tutaongea kwa urefu mkono wako bado ni mfupi sana kwenye utoaji milioni miatano unataka kila taarifa, sasa namimi nakuuliza maswali machache kama makubaliano yetu ya mdomoni yalivyo fanyika. Huyo mtu anatafutwa kwa kuua hiyo familia, ni familia ipi hiyo na huyo Zakaria ni nani hasa mbona anaimbwa sana?" Kanivasi hakuwahi kupewa taarifa za kutosha za Zakaria hata mara ya kwanza hakupewa taarifa zozote za kumhusu huyo mtu.
"Hata sisi hapa wote watatu hatuijui historia ya huyo mtu tuna taarifa zake chache sana kwa sababu inadaiwa hata nchi yake watu wenye taarifa zake hawafiki hata watatu unahisi sisi tutazipatia wapi? Mtu anaishi kwa siri sana sehemu yoyote ile duniani utazipatia wapi taarifa zake? Sisi hapa tupo kumtafuta huyo mtu kwa namna yoyote ile tumeagizwa na mtu ambaye ndiye pekee anaye ishi kwenye hiyo familia iliyo uawa na Zakaria ilikuwa familia yake, ana uchungu sana na huyo mtu ila kwa taarifa chache ambazo zipo ni kwamba sio mwanadamu kama walivyo wengine anadaiwa kuwa mtu wa kipekee sana kwenye huu ulimwengu, anadaiwa kuwa na dunia yake kwenye ulimwengu wa watu hatari hivyo lengo la kuja Tanzania ni baada ya upatikanaji wa taarifa za uwepo wake na familia yake yeye, tunataka kujua yuko wapi kwa sasa ama familia yake baada ya hapo tufanye kazi yetu ya kumkamata" maneno ya huyo mtu yalimfanya Kanivasi ashushe pumzi kwa nguvu, alimwangalia mtu huyo hakujibu chochote aliingia kwenye gari yake na kuwaamuru watu wake waondoke ndani ya hilo eneo.
Niseme tu 57 inatia nanga hapa tukutane mpaka wakati ujao tena
Bux the story teller
Chao.
Sent from my TA-1053 using
JamiiForums mobile app