Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Nimemsikiliza Ndg. Gerson Msigwa kwakweli nimesikitika sana kuona watumishi wa umma nyakati hizi badala kuwa watumishi wa umma wamegeuka kuwa watetezi wa viongozi wabovu. Sakata hili jinsi anavyotetea ni sawa na jinsi alivyotetea uongo na udhaifu mkubwa uliosemwa na kiongozi mmoja kuhusu kununua umeme nje ya nchi, Wakati huohuo alishasema Tanzania itauza umene nje ya nchi.OK, Tuyaache hayo.
Tangu mwaka 2023 Tulielezwa kwamba zaidi ya Bilioni 31 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa uwanja wa Mkapa, Baada ya hapo uwanja ukafungiwa.
Unapokarabati uwanja wa mpira, Ni jambo gani la msingi zaidi? Vyoo? Running tracks? Rangi ya milango ya uwanja? Hivi unaweza kutenga budget ya kutengeneza gari ambalo limekufa engine, kisha ukaanza na ukarabati wa radio, air freshener, lether seats nk.
Badala ya kuanza na engine? Maana yangu ni kwamba unapozungumzia mpira wa miguu unazungumzia 'pitch' eneo la kuchezea ndilo eneo muhimu, watu hawaendi uwanjani kujisaidia haja ndogo! Wanaenda kutazama wachezaji wakicheza.
Tangu 2023 hiyo ndiyo pitch iliyokarabatiwa katika hiyo Bilioni 31?? Kama tangu 2023 hali ndiyo hiyo unathubutuje kusema wiki mbili zilizopita na sasa hali ni tofauti?
Uwanja wa Amahoro ulitumia muda mfupi na gharama ndogo ila quality inaonekana, Nyie miaka miwili, Bilioni 31 hata pitch haieleweki! MAAJABU
TAFADHALI ELEZA PESA HIZO AMBAZO NI KODI ZA WANANCHI MMEZIPELEKA WAPI?