Gerson Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu

Gerson Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu

RAIS WANGU SAMIA, MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA ANIOMBE RADHI HADHARANI.

Mheshimiwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi,

Awali ya yote naomba nikupe Pole na hongera kwa majukumu mazito unayoendelea kutufanyia kwa weledi na mafanikio makubwa sisi wananchi wako wa Watanzania tangu uingie Ikulu miezi sita sasa. Kwa majina naitwa Suphian Juma Nkuwi, ni Mtanzania Mzaliwa wa Kijiji cha Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mkoa wa Singida.

Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, kwa kuzingatia Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Katiba ya Chama cha Mapinduzi sehemu ya Kwanza, fungu la 4. Imani (1) Binadamu wote ni sawa (2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake;

Kwa masikitiko makubwa kupitia barua hii ya wazi napenda kuleta malalamiko yangu mbele ya ofisi yako takatifu kwamba Msaidizi wako, Gerson Msigwa ambaye kwa sasa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Septemba 18, 2021 akihojiwa na Mtangazaji katika kituo cha habari cha Star TV () alitamka kwamba habari iliyochapishwa ukurasa wa mbele, Aprili 20, 2019 na gazeti la Tanzanite iliyosomeka kwamba "SHOGA AWACHANGANYA ZITTO, MAALIM SEIF" kwamba ILITHIBITISHWA ndio maana gazeti hilo la ndugu Cyprian Musiba halikuwahi kufungiwa na Serikali.

Rais wangu, ndani ya habari hiyo mwathirika aliyetambulishwa kama 'shoga' kwa majina na picha ni mimi. Na kwa hakika haikuwa habari ya kweli kwani natambua mapenzi ya jinsia moja si tu ni kinyume na sheria zetu za Tanzania bali pia maadili na tamaduni zetu haziruhusu. Na mbaya zaidi gazeti hilo linalofahamika nchini kama 'bingwa' wa kuchafua VIONGOZI wa Chama, Serikali, wanasiasa na Wanaharakati halikuwahi kunitafuta kabla ya kutoa habari hiyo ovu kama alivyodai ndugu Msigwa.

Hivyo, kauli hiyo potofu kutoka kwa Kiongozi Mkubwa kabisa wa Serikali yetu si tu imezua tafrani mtandaoni bali pia hadi naandika barua hii kwako imeendelea kunidhalilisha na kuusigina Utu wangu mbele ya familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu na kuniharibia taswira yangu na hata majukumu yangu ya kila siku kama Mtanzania na Mwanasiasa mchanga mwenye ndoto ya kuijenga nchi yake kwa wivu mkubwa.

Kwa kuzingatia ofisi yako ni tegemewa kwa kutoa haki, naomba ndugu Msigwa aniombe radhi hadharani kupitia chombo cha habari alichonichafulia jina na Utu wangu hadharani, ili tu si kufuta kashfa hiyo kwangu bali pia kuondoa tafsiri potovu kwamba Ofisi yako tukufu na hata Chama chetu cha Mapinduzi kimempa nafasi nyeti mtu asiye makini na asiyeona aibu kutamka kauli za uwongo mbele ya umma. Vinginevyo, nitaomba ruhusa ya ofisi yako niendelee kutafuta haki yangu kwa njia zingine ikiwemo njia za kisheria.

Aidha, Rais wangu kabla ya kukuandikia barua hii ya wazi, naomba pia kukujulisha kwamba Octoba 1, 2021 nilishawahi kutuma barua ya malalamiko haya kwako dhidi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia barua pepe ya Ofisi ya Rais Ikulu press@ikulu.go.tz ambapo kwa barua hiyo niliambatanisha kopi ya gazeti la Tanzanite lililonichafua na kipande cha video cha ndugu Gerson Msigwa akibariki kashfa hiyo dhalilishi kupitia Star TV. Ingawa sikupatiwa mrejesho wowote wa barua pepe hiyo hadi naandika barua hii ya wazi kwako.

Natanguliza Samahani kwa usumbufu. Na natumaini ombi langu litafanyiwa kazi mapema. Nakutakia kazi njema Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi na Mwenyezi Mungu azidi kukutunza.

Raia wako mwema,
Suphian Juma,
Singida, Tanzania
Octoba 7, 2021.
Email: yessuphian@gmail.com
Phone: 0717027973

View attachment 1966980
Kwa pozi hizi wewe usitafute mchawi Msigwa yuko sahihi kabisa
JamiiForums-251271226.jpg
JamiiForums691792977.jpg
 
Huyu shoga masikio yake hayasikii vizuri. Msigwa alisema kama lile gazeti halikufungiwa LABDA,alisema LABDA zile habari zilithibitishwa.
Ndiyo ile posting posting yangu niliandika jana kuhusu Musiba moderator ameiondoa. Mambo anayoandika Musiba yanaweza kuwa ya ajabu sana lakini yakawa kweli.
Viongozi wanaweza kufanya makosa. B
Viongozi siyo malaika. Wamejenga madaraja,wamejenga zahanati,unataka nini tena toka kwao?
Kwa mfano Magufu alikuwa anawakumbatia watoto hadharani kwenye jukwaa. Ilitakiwa wapambe wake wawaalike wale watoto ili Mkulu aweze kuomgea nao kwa sababu akifanya mambo yale hadharani it can cost him his life.
Inaonyesha disconnect kati ya dikteta na wapambe wake.
 
Kama Msemaji wa Serikali amesema sisi ni nani wa kumpinga?
Mtu anapolalamika kuwa ameonewa ana haki zote....msemaji wa serikali ni mhukumu wa kuzuia watu kulalamikia wanayoona si sawa kwao?!!!Khaa 😳😳
 
Kama Msemaji wa Serikali amesema sisi ni nani wa kumpinga?
Pole sana ndugu Sufian. Nenda mahakamani tume ya madaktari wabobezi itaundwa kwa weledi na umakini mkubwa watachunguza kama una marinda au umepoteza marinda. Ikithibitishwa pasipo shaka kwamba hujachokonolewa na sphincter zako hazijalegea fungua kesi ya madai utalipwa pesa nyingi mno pia watakuomba radhi.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Mtu anapolalamika kuwa ameonewa ana haki zote....msemaji wa serikali ni mhukumu wa kuzuia watu kulalamikia wanayoona si sawa kwao?!!!Khaa [emoji15][emoji15]
Sasa kuja kulalamikia humu JF unaona ni njia sahihi? Unaona alivyojivua nguo.
 
Duuuh[emoji15][emoji15][emoji15]

Sitetei tabia hizo mbaya...bali ninashutumu tabia ya hovyo ya kutoheshimiana kwa kuongea HADHARANI kashfa za AIBU NA FEDHEHA.......kwa yeyote afanyaye......

Haya umeshanidhalilisha basi furahisha nafsi yako mkuu....

Peace
Mbona unatumia nguvu nyingi sana kutetea kuliko muhanga mwenyewe?

Naanza kuliona tatizo kwako!
 
Back
Top Bottom