Gerson Msigwa: Changamoto ya wagonjwa wa figo nchini inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Tusimbeze Profesa Janabi

Gerson Msigwa: Changamoto ya wagonjwa wa figo nchini inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Tusimbeze Profesa Janabi

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema changamoto ya wagonjwa wa figo nchini imeongezeka kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na watu kutumia lishe isiyo bora, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, sukari, kutokufanya mazoezi, unywaji pombe kupita kiasi, matumizi holela ya dawa pamoja na kutotumia maji ya kutosha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma alipotembelea Bohari ya Dawa (MSD) kanda ya kati, Msigwa amesema serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuhakikisha inakabiliana na hali hiyo kwa ufanisi na kupunguza athari kwa wananchi.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupunguza gharama za huduma kwa wagonjwa wa figo- moja ya hatua kubwa zilizochukuliwa ni kuongeza idadi ya mashine za kuchujia damu kutoka mashine 60 zilizokuwepo awali hadi kufikia mashine 137 hivi sasa ambapo ongezeko hilo limekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wagonjwa wengi zaidi nchini.

Kama mtu na elfu 2 anapata pombe inatomlewesha kutwa nzima ataachaje kuwa na figo mbovu maana unywaji umekuwa mkubwa kupitiliza yaani mtu akiamka asbh kwabla ya chai anawahi kupata kisungura au smart gin
Yaani sojo la gongo limeshuka sana hivi visungura na smart gin vinanyweka sana
 
Serikali inacheza na afya za wananchi wake
Wananchi nsio wanacheza na afya zako

Wewe unafahamu kabisa pombe ni shida halafu unatumia pombe weeee, ukianza kuugua unalaumu serikali?

Nadhani ifike mahala sasa watanzania tubebe majukumu yetu w
 
Kama mtu na elfu 2 anapata pombe inatomlewesha kutwa nzima ataachaje kuwa na figo mbovu maana unywaji umekuwa mkubwa kupitiliza yaani mtu akiamka asbh kwabla ya chai anawahi kupata kisungura au smart gin
Yaani sojo la gongo limeshuka sana hivi visungura na smart gin vinanyweka sana
Na cha kushangaza zaidi, hivi vipombe vinauzwa mpaka kwenye maduka yasiyo ya pombe (Maduka ya mahitaji ya nyumbani), stendi za mabus na daladala. Mtu ana buku lake anashushia kisungura chake anamalizia na ugoro.
 
Kama mtu na elfu 2 anapata pombe inatomlewesha kutwa nzima ataachaje kuwa na figo mbovu maana unywaji umekuwa mkubwa kupitiliza yaani mtu akiamka asbh kwabla ya chai anawahi kupata kisungura au smart gin
Yaani sojo la gongo limeshuka sana hivi visungura na smart gin vinanyweka sana
Fanyeni mazoezi na mpate lishe bora.

Nyie endeleeni kudhani kila kitu ni pombe, haya.
 
PIA KUNA MATUMIZI MABAYA SANA YA VIWATILIFU
Mtu ananyunyizia kiwatilifu siku mbili anapeleka mboga sokoni....
hata mm nahisi shida ipo apo maana unakuta hii michicha na chainizi tunakula inauzwa ikiwa na madawa yenye sumu kali za viwandani. ww bila kujua unanunua unapikia familia inakula ivoivo. ndomaana unaskia kitoto kidogo nacho kinaumwa kansa.
 
Back
Top Bottom