Gerson Msigwa: Hakuna uvamizi uliofanyika katika Ofisi za JamiiForums

Gerson Msigwa: Hakuna uvamizi uliofanyika katika Ofisi za JamiiForums

Screenshot_20250905-212938.jpg
 
Jamii forum iwazuie members wote wanaomtukana rais. Hawatasumbuliwa , la sivyo...
Haiwezekani, nature ya platform ni watu kuwa huru kuongea mambo uhuru, wakianza ku control a lot of peope will left and ukuaji wao utaishia hapo
 
Hapo patakuwa pagumu sana, wanawataka watu wale kwenye uzi uliofufuliwa jana. Ule uzi ulikuwa wa May, ukafukuliwa jana sijui Polepole alimtaja bonge. Sasa watu walichafukwa sana na zile picha, hawajapenda yale yaliyokuwa yanachangiwa. Hii ngoma ngumu sana.
 
Hii ndo Tarifa yake "Gerson Msigwa " usiku huu.

Hakuna uvamizi uliofanyika katika ofisi za Jamii Forums. Kilichotokea ni utaratibu wa kawaida wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Serikali na wadau wake ambapo leo Maafisa wa Serikali walikwenda kuwasilisha barua ya wito kwa Jamii Forums. Ndugu Maxence Melo usilete taharuki isiyo na sababu za msingi, toa ushirikiano.

Soma Pia: Maxence Melo: Ofisi za JamiiForums, Mikocheni zimevamiwa

View attachment 3466077
Kwani hakuna footage wakati huo uvamizi unafanyika Jamii Forums waiachie kama ilivyokuwa wakati wa uvamizi Coulds?
 
Back
Top Bottom