Gerson Msigwa: Huwezi kukurupuka kumfukuza mtu, pengine hata wakaguzi wa CAG nao ukaguzi wao una dosari

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kwamba ni vema Wadau wakavuta subira badala ya kutaka kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG achukuliwe hatua, yapo maeneo ambayo ni lazima yapitiwe upya ili kujiridhisha na kila lililotajwa.

Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa.

Toa Maoni yako.

=========================

UPDATES...
Baada ya taarifa hiyo kusambaa, Msigwa ametumia ukurasa wake wa kijamii kutoa ufafanuzi wa kile alichokizungumza kwa kuandika: "Nilichokisema kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) baada ya kuulizwa swali na Watangazaji wa EA Radio leo asubuhi. PUUZENI ile screenshot inayoenezwa ikiwa imemega maneno machache yanayoleta TAHARUKI (spinning)."

Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa .
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Watanzania wengi wana mihemko na hawako objective, ndio maana serikali huwa inapuuza na kungojea mijadala ife yenyewe, kubishana nao ni kupoteza muda.

Msigwa ameongea ukweli mtupu, wenye uzoefu na ripoti za CAG wanayajua hayo, huwa zina makosa mengi tu, na ndio maana baadhi ya hoja zake huwa zinafutwa na kufungwa kabisa.

Wanaofanya ukaguzi ni watumishi wa umma wa kawaida tu, tena wengine wameajiriwa juzi juzi hapa hata uzoefu hawana. Watu huwa wanadhani Kichere mwenyewe ndio anakwenda 'site'.

Hatusemi kuwa ripoti yote imejaa makosa, tunachosema ni kuwa watu wawe watulivu utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ufuatwe, wenye makosa watachukuliwa hatua na wale wasio na makosa hoja zao zitafutwa.

Kwa hisia kali za watanzania ni bora Msigwa angekaa kimya, sometimes it doesn't matter if you are correct.
 
Msemaji wa Serikali ya Tanzania , Gerson Msigwa amesema kwamba ni vema Wadau wakavuta subira badala ya kutaka kila aliyetajwa kwenye ripoti ya CAG achukuliwe hatua , yapo maeneo ambayo ni lazima yapitiwe upya ili kujiridhisha na kila lililotajwa .

Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa .

Toa Maoni yako .
Msemaji mjinga sn huyu, si kuna mahakama shida iko wapi? nchi imekuwa na wasemaji wajinga sn hata aliyetoka naye alikuwa ni mpumbavu sn
 
Watanzania wengi wana mihemko na ni wajinga, ndio maana serikali huwa inapuuza na kungojea mijadala ife yenyewe, kubishana nao ni kupoteza muda.

Msigwa ameongea ukweli mtupu, wenye uzoefu na ripoti za CAG wanayajua hayo, huwa zina makosa mengi tu, na ndio naana baadhi ya hoja zake huwa zinafutwa na kufungwa kabisa.

Wanaofanya ukaguzi ni watumishi wa umma wa kawaida tu, tena wengine wameajiriwa juzi juzi hapa hata uzoefu hawana. Watu huwa wanadhani Kichere mwenyewe ndio anakwenda 'site'.

Kwa umbumbumbu wa watanzania ni bora Msigwa angekaa kimya, sometimes it doesn't matter if you are correct.
We ndiyo mjinga zaidi, watumishi wa CAG huanza ukaguzi baada ya mwaka wa fedha kufungwa June 30 na wao July wanaingia kazini, wanaanza kuomba viambatanisho vyote, ikifika October hutoa hoja zao na kuwapa muda management kuzijibu mpaka January, how huo muda hautoshi na wakati kuna kuwa na exit meeting?
 
Amedai kwamba unaweza kumchukulia mtu hatua kumbe hana makosa na pengine ripoti ya CAG ndio iliyokosewa .
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Imeisha hiyo [emoji38][emoji38]
 
Report ya CAG haiwezi kua na makosa ila kuna tatizo la uelewa tu.

CAG hujikita kwenye ufuatiliaji wa kanuni na taratibu. Iwapo kanuni zilizowekwa hazikufuatwa hata kama kitu kilichopaswa kufanyika kimefanya ila kwa kikiuka taratibu CAG husema kuna ubadhirifu ama upotevu wa mapato.

CAG hujikita kwenye compliance of rules, regulations and laws.

Iwapo sheria imepindishwa CAG husema kuna ubadhirifu. Hua kuna uhusiano ama asilimia kubwa sana ya ukweli kwenye uvunjaji wa taratibu na upigani. Taratibu nyingi huvunjwa ili watu wafanye yao so 99.9% ya report ya CAG hua ina ukweli.
 
We ndiyo mjinga zaidi, watumishi wa CAG huanza ukaguzi baada ya mwaka wa fedha kufungwa June 30 na wao July wanaingia kazini, wanaanza kuomba viambatanisho vyote, ikifika October hutoa hoja zao na kuwapa muda management kuzijibu mpaka January, how huo muda hautoshi na wakati kuna kuwa na exit meeting?
Unadhani wanakaa kwenye taasisi moja kwa muda gani? CAG hana workforce ya kukagua taasisi zote kwa pamoja, wanatumia muda mfupi sana kwenye kila eneo.

Mbali na hapo watumishi wa ofisi ya CAG wanaweza kuwa na changamoto za uelewa wa baadhi ya mambo, jambo ambalo ni kawaida kwa watumishi wote serikali, wao sio malaika. Kuna vitu wanaibua kama dosari ambavyo sio dosari.

Hata wakipewa maelezo na vielelezo haisaidii, ndio maana kwa mujibu wa sheria ripoti ya CAG ni 'input' kule bungeni, sio final.

Lazima kamati za bunge zipitie kwa umakini hoja zote, na wakihitaji maelezo zaidi pande zote mbili zinaitwa, upande CAG na taasisi husika.

Mara nyingi tu CAG mwenyewe anaridhia baadhi ya hoja zifutwe baada ya wote kukalishwa na kamati ya bunge.

CAG ni kama mwendesha mashtaka, kushtakiwa haimaanishi una hatia. Bunge ndio mahakama, na taasisi zenye kasoro ni watuhumiwa.

It's basic stuff, but somehow people don't get it. Ndio maana nasema watanzania wengi ni wajinga.
 
Msigwa anatoa majibu mepesi kwenye masuala muhimu, namuona anaishusha hadhi kazi iliyofanywa na CAG, huu unaweza kuwa muendelezo wa mpango wa kuwalinda wezi wa pesa zetu unaofanywa na serikali.
 
Unadhani wanakaa kwenye taasisi moja kwa muda gani? CAG hana workforce ya kukagua taasisi zote kwa pamoja, wanatumia muda mfupi sana kwenye kila eneo.

Mbali na hapo watumishi wa ofisi ya CAG wanaweza kuwa na changamoto za uelewa wa baadhi ya mambo, jambo ambalo ni kawaida kwa watumishi wote serikali, wao sio malaika. Kuna vitu wanaibua kama dosari ambavyo sio dosari.

Hata wakipewa maelezo na vielelezo haisaidii, ndio maana kwa mujibu wa sheria ripoti ya CAG ni 'input' kule bungeni, sio final.

Lazima kamati za bunge zipitie kwa umakini hoja zote, na wakihitaji maelezo zaidi pande zote mbili zinaitwa, upande CAG na taasisi husika.

Mara nyingi tu CAG mwenyewe anaridhia baadhi ya hoja zifutwe baada ya wote kukalishwa na kamati ya bunge.

CAG ni kama mwendesha mashtaka, kushtakiwa haimaanishi una hatia. Bunge ndio mahakama, na taasisi zenye kasoro ni watuhumiwa.

It's basic stuff, but somehow people don't get it. Ndio maana nasema watanzania wengi ni wajinga.
Kwa maelezo yako ni kwamba Hakuna haja ya kuwa na CAG. Mbona tutaibiwa mpaka tukome.
 
Hahah...Kama kweli Msigwa kasema hivyo hafai kuwa Msemaji wa serikali... Ilitakiwa aseme ripoti imetolewa, serikali inafanyia Kazi ripoti hiyo na kila atakayebainika kuhusika na ufujaji huo,atachukuliwa hatua za kisheria kama Sheria na katiba inavyoelekeza...

Kusema Ripoti imekosewa ni ku-undermine integrity, independence na weledi wa ofisi ya CAG...

Gerson Msigwa anapaswa kujua CAG anatumia vielelezo na informations anazopewa huko kwenye Taasisi za serikali anazozikagua,..sasa either ripoti imekosewa au la,sio Kazi ya Msigwa Kusema, ndio maana kuna Mahakama, watakaoperekwa huko ndio wataieleza Mahakama ni wapi CAG kakosea na ukweli ni upi.

Walio karibu na Msigwa mnaweza kumwuliza ni kwanini hajawahi kuhoji ni kwanini Police wanawashikilia watuhumiwa kwenye sero zao ambao baadae Mahakama inawaachia huru wakikutwa/wakithibitisha hawana hatia..au hao walioko serikalini na wametajwa kwenye Ripoti ni Extraordinary na Sheria za Nchi ya Tanzania haziwahusu!?
 
Kazi ipo !
 
Back
Top Bottom