Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kuna Tofauti kubwa sana kati ya kuwa Msemaji wa Ikulu na kuwa Msemaji wa Serikali ama kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo , Ikulu unaongea wewe tu na wala huhojiwi na mtu yeyote , kuna maswali uchwara tu yaliyojaa uoga uoga hivi , tena unaweza hata usiyajibu na shughuli ikaisha tu.
Idara ya Habari Maelezo haina mchezo na wala hakuna mtu atakuogopa kwa lolote, kifupi ni kwamba umeletwa kwenye moto ambako weledi wako ndio utakaokuokoa, hata hivyo naamini awamu ya Mama haitakuwa na fungia fungia Vyombo vya habari , vinginevyo hapo ndio mahali ambapo ungejibebea lawama za milele na laana kubwa mno .
Kimsingi umeshushwa kutoka juu na kuporomokea kwenye tanuri la moto , sasa jiongeze mwenyewe .
Kwa leo ni hayo tu mjomba , ukitaka mengine nipigie .