Gerson Msigwa: Kinachoendelea mitandaoni kuhusu "No Reforms, No Election" ni UPUUZI

Wapalestina, sudan n.k ni ndugu zangu, upo hapo?
Tangia lini jitu jeusi akawa na undugu na muarabu hii Kali au huonagi majitu meusi yakitemewa mate na waarabu huku yakiwa maislamu Yani muarabu hataki hata kumsikia undugu na jitu jeusi🤣🤣🤣🤣
 
Hao wapumbavu wa chadema na Gwajima
FB_IMG_1748360197313.jpg
 
Wewe umejuaje mzee kibao kauawa na ssh???? Je, ikiwa kuna chama flani limefanya hivyo ili kumchafua huyu mama!! Ulishawahi kufikiria hilo!!

Free palestine šŸ‡µšŸ‡ø
Wewe ndiye ssh!?
 
View attachment 3359827
DAR. Kufuatia wimbi la wananchi kujibu posti za viongozi wa Serikali na watu maarufu kwa kampeni ya No Reforms No Election inayotumiwa na CHADEMA, Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ni upuuzi akiwataka wajiepushe na kampeni zisizo na tija.

No Reforms No Election ni kampeni iliyoanzishwa na inayotangazwa kwenye mikutano ya CHADEMA wakitaka kuwepo mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kufika siku ya kupiga kura Oktoba 2025.

Katika mitandao ya kijamii makundi mbalimbali yanahamasisha kupaza sauti za kampeni hiyo kwa kuchapisha ujumbe na kutoa maoni ya No Reforms, No Election pale ukurasa fulani unapokuwa umechapisha maudhui yake yoyote.

Haijalishi ni ukurasa wa nani, iwe wa vyombo vya habari, kampuni, matangazo sehemu kubwa ya maoni ni No Reforms, No Election na wengine wanafupisha kwa kuandika NRNE.

Hali hiyo imewalazimu baadhi ya viongozi kuzima sehemu ya maoni ili kujiepusha na kampeni

Kauli ya Serikali
Alipoulizwa na tovuti ya Mwananchi Communications Ltd kuhusu hatua hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amejibu "Watu wameamua kufanya hivyo, tutafanyaje," amesema.

Ingawa katika maelezo yake aliwatahadharisha wanaofanya mchezo huo akidai hauna tija na 'upuuzi' zaidi ya kupoteza muda wao.

"Watu wajiepushe na kampeni zisizokuwa na tija, watumie mitandao kama fursa ya kujifunza teknolojia mpya, wanapaswa kutambua na kujua kutumia mitandao vibaya ni kupoteza rasilimali fedha kwa kuwa wanatumia bando," amesema.

Katika maelezo yake Msigwa amesema badala ya kupoteza muda kuendesha kampeni hizo watumie nafasi hiyo wajielekeze kujenga nchi yao.

"Kinachoendelea kwenye mitandao ni upuuzi. Huu ni upuuzi unaoendelea Watanzania wajielekeze kujenga nchi yao. Huwezi kuendesha kampeni ya kuzuia Uchaguzi wakati nchi imejiwekea kalenda yake," amesema Msigwa.

Kampeni hiyo imeenda mbali zaidi kwa kumgusa hadi msanii wa Nigeria Chellaboi ambaye amekuja nchini hivi karibuni na kushangazwa na ukurasa wake kumiminika maoni yanayohusu kampeni hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Sawa.
No reform no election
 
No reform No Election ndio wanataka kujenga nchi yao sasa aendelee kuita upuuzi Ego Ego Ego
 
Kasema "tujenge nchi" haha ms*nge huyu,.sisi tujenge wao wabomoe,no..now wote tunabomoa tukose wote..

Na tangu lini wamekua na huruma na bando letu?mind your own data msigwa,tutapush hashtag hata kwa Tuzo Points.. #NoReformNoElection
 
Yeye ni msemaji wa serikali siyo wa ccm ajaribu kutenganisha hayo mambo anapokuwa anaiongelea serikali yake.

No reform no election ni ajenda ya chama cha siasa, yeye hana mamlaka kuongelea yanayohusu vyama bali serikali tu.

Kusema ni ujinga anaonyesha yeye ndiye mjinga, ya chadema haya muhusu, na ya ccm yeye siye msemaji wake.
 
Back
Top Bottom