Wewe na Msigwa Nani Yuko serikalini?
Mkuu
Bila bila, mimi kwa sasa siko serikalini ila zamani niliingia serikalini kabla yake, i
Msigwa anasema hatuna hata moja, wewe unasema tunazo 4. Kama ni kweli zipo 4 nini Nia ya Msigwa kusema hatuna hata moja?
Serikali ni mdude mkubwa sana, hakuna mtu yoyote anayeijua kila kitu kuhusu serikali, mtu unavijua tuu vile vinavyokuhusu, hivyo mimi nilikoingilia serikali siko alikoingilia yeye, hivyo usikute hata yeye hajui kuwa tunazo, ila kama anaingia jf, akiingia na kutusoma humu kaka zake, sasa ndio na yeye atajua tunazo!. Kinachofanywa zisitajwe kwasababu hazikuletwa kwa madhumuni ya rescue oparations na uokoaji!, hizo kitu tunazo zipo tunazo ziko 4, zimeletwa kwa kazi maalum na zipo tuu zimepaki pale mahali zikisubiria kilichofanywa ziletwe kitokee!.
Amini usiamini, kule mahali, angekuwepo yule Msukuma!, zingetolewa and within 1 hour ndege ingecholopolewa!, hivi ile paredi ya miaka 60 ya uhuru, hamkuiangalia?, mbona zilikuwepo!.
Kuna vitu vingine jameni ni siri za usalama wa taifa na nchi, hatuwezi kusema humu!, hizo chopa tunazo 4, moja ya 4 hizo ndio baba lao!, yenyewe haikuonyeshwa for diplomatic reasons kwasababu jeshi letu tunasaidiwa sana na Waingereza na vifaa vingi tumenunua BAE, huo mdude funga kazi tulipewa na taifa fulani rafiki ambalo mabeberu hawalipendi!.
Mfano hata bunduki za AK- 47, tunao mzigo wa kutosha tuu!, tulipewa na rafiki yetu fulani!, tumezisunda tuu mahali tukisubiria kiwake, tunamchakaza adui fasta!, hatuwezi kusema tunazo wala kuzionyesha kwasababu mabeberu wamezipiga marufuku AK 47!, hata mimi nimesema humu kwa sababu mabeberu hawajui Kiswahili!.
Baada ya vita vya Kagera na daraja kuvunjwa na yule nduli, jeshi letu lilijikuta linakwama kupeleka vifaa front, askari wetu wakalazimika kuvuka mtu kwa kuzama kwenye maji usiku kucha, kufika ngambo wakajikuta wana kwama ku advance hadi daraja la muda lilipotengenezwa, sasa from that lesson, ukaletwa mdude wa kufa mtu wa kubeba vifaru!, mtu akituchokoza, hata akivunja daraja, tunabeba vifaru, tunambwagia mlangoni kwake!.
Kuna siku niliwahi kuzungumza kuhusu ukakamavu jeshini, sio kila kabila ni la kupewa u CDF kwasababu tuu ya seniority!. Blaza alipoingia, CDF aliyepo aliishafikia umri wa kustaafu!, Blaza akamuongezea muda kidogo ili atafute jembe kazi!, likapatikana lile jembe kazi la Ngw'anangosha toka pale Masanza One au Masanza Kona
Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?
Amini nakuambia CDF angekuwa ni yule Msukuma, lile likitu lingetolewa!.
Sasa hivi tuko kwenye mchakato wa mtangamano wa nchi za Afrika Mashariki kuwa nchi moja, hivyo hatuna tena jirani yoyote ambaye ni threat to our national security, yale mavifaa bab kubwa ambayo tumeyasunda pale mahali chini ya ule mlima, tuyatoe yawe yanatumika for civilian humanitarians rescue missions maana hatuna tena any combat operations!, unadhani hata madata watu wote wa serikalini wanayajua?, mi mwenyewe nimeyajua kwa sababu mimi licha ya kuwa ni mwandishi tuu wa habari, pia ni mjeda!.
P