Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Msemaji Mkuu wa Serikali akiwa Mkoani Morogoro, Gerson Msigwa leo Mei 31, 2026 akitoa taarifa ya Serikali kwa Umma wa Watanzania amesema;
"Niwahakikishie wana Morogoro na Watanzania wote kwa ujumla kwamba nchi yetu ni shwari, tena shwari sana. Nchi yetu ina amani ya kutosha na Watanzania wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Na napenda kuchukua nafasi hii kuwatia moyo Watanzania, msibabaiwshwe na maneno yanayotembea mitandaooni ya kuwavunja moyo, ya kuwatishia, ya kuwatia wasiwasi. "
"Nchi yetu ni salama, fanyeni kazi zenu vizuri. Mashambani nendeni mkalime mkiwa na amani kabisa. Wale mnaofanya kazi, fanyeni kazi iwe ni serikalini, iwe ni katika kampuni binafsi fanyeni kazi zenu kwa amani. Nchi yenu iko salama, serikali inatekeleza majukumu yake kama kawaida na kila kitu kinakwenda vizuri.
Mtu asiache kupanga mipango yake ya maendeleo akasikiliza watu ambao wanasema, "hapakaliki." Tanzania panakalika, pako salama na Watanzania wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, viongozi nao wanatekeleza majukumu yao."