DUNIA INAJUMLA YA WATALI 1.5BL WANATAFUTA WAPI WAKALE BATA KILA MWAKA | TANZANI NI YAPILI KWA VIVUTIO ASILIA DUNIANI TUNAPOKEA WATALI CHINI YA 1M,IKOJE HII!?
_____________________________________
Niseme kidogo kuhusu Rais Samia na "Royal Tour. "Tanzania ni nchi ya Pili kwa Vivutio vya asili duniani baada ya Brazili,Tofauti na nchi zingine 80% ya Watali wote wanaozuru Vivutio vya Brazili ni Wabrazili,Niwatali 6.5m ndio wanatoka nje ya Brazili kwa mwaka,Mwaka 2018|19 Brazili ilijikusanyia kiasi cha $97.11BL karibu Tshs 215 trilioni kama mapato yatokanayo na Utali, Fedha hii inaweza gharamia bajeti ya Serikali ya JMT kwa miaka 5 mfululizo tena bila ya Mtanzania yeyote kutozwa kodi|tozo,Namaanisha hadi Vyoo vya kulipia viwe bure.Je,tumewahi kujiuliza kwanini hawa Brazili wakusanye Tshs 215trilioni kwa mwaka na Sisi tukusanye Tshs 5.3trilioni kwa mwaka sawa na tofauti ya Tshs 210trilioni ili hali Sisi ni Wapili baada ya wao kwa Vivutio duniani, Yaani Kwanini Wao!!? Rais Samia Suluhu amekuja na jibu ambalo ni "Royal Tour Film " na hapa lazima tutambue Tanzania Kiutali haifahamiki kabisa duniani heri ya Bongo Zozo.
Leo kwa mwaka Tanzania inapokea watali chini ya 1m pamoja na utitiri wa Vivutio ilivyonavyo, Chaajabu Ufaransa inayoongoza kwa Utali duniani haina twiga wala Simba inamagofu na Mnara ( all are man-made ) lakini inaingiza zaidi ya watali 89m na €56.2BL kwa mwaka sawa na Tshs 154trilioni,Hivi kwa vivutio tulivyonavyo nikweli tumeshindwa kuinyanga'nya hata Watali 5m tu kwa mwaka waje Tanzania!? Lazima tufahamu duniani kwa Sasa Utali ni biashara kipaumbele na msitegemee nchi yeyote duniani kutangaza vivutio vyenu zaidi ya Sisi wenyewe kwa Platform hizi za " Royal Tour Film. " Tatizo la Uhaba wa watali Tanzania sio tu Corona hata "Ushawishi " pia uko chini, Kwaakili ya kawaida ni ngumu zaidi kwa Mtali anayefahamu "Nini Kipo Tanzania " aache kuja kumtazama nyumbu|tembo "Live " pale Serengeti aende kumtazama tembo wa kwenye michoro kule Ufaransa,
Siku Mungu akitupa walau watali 5m tu kwa mwaka nchi yetu itaingiza zaidi Tshs 10trilioni kama mapato yatokanayo na Utali,Pesa hii inakwenda moja kwa moja kwa wanachi kwanjia ya kuwahudumia Watali na serikali itapata kiasi kama tozo ya Utali,Nchi hii inaweza kuendeshwa kwa Utali tu kama tu dunia itafahamu "Nini Kipo Tanzania " Zaidi ya 50% ya watali wanaofika Kenya kwa Utali wamevutiwa na Vivutio vilivyopo Tanzania,inauma Sana na lazima tumshukuru Rais Samia kwaajili ya "Royal Tour Film " Mfano, Mwaka 2017|18 mapato yetu yatokanayo na Utali yalifikia $2.4BL sawa na Tshs 5.5trilioni wakati rekodi ya Watali ikiwa 2m,Lakini tunafahamu duniani kila mwaka kuna zaidi ya Watali 1.5bl wanatafuta wapi waende kula bata,Lakini Sisi Tanzania pamoja na kuwa Wapili kwa Vivutio tena vya asili duniani tunaambulia watali 2m tu,Nadhani kunasehemu tulikwama na ndio Sababu ya Mungu kumleta Rais Samia na yeye kutuletea "Royal Tour Film. "Mnaolalamikia gharama za Tour rudieni kusoma andiko hili,
.........Kazi iendele.........