Gesi mnayopiga kelele kuuzwa Kenya haitatumika kwenye Viwanda vya Tanzania?

Gesi mnayopiga kelele kuuzwa Kenya haitatumika kwenye Viwanda vya Tanzania?

Watu hawana jema, kibaya zaidi wanapiga kelele bila hata kujua makubaliano na mkataba unasemaje

Ukiwa na tabia ya unyimi sana unawezajikuta unakufa njaa sababu tuu hutaki kuuza mali usiyoitumia ili mwenye uhitaji aitumie akupe pesa nawe upate chakula
Kabisa. Hii haihitaji kuwa genius kuijua.
 
Wasukuma Rais wenu kalala chattle, msitusumbue tafadhali!!!!
Tembea uone ww panya buku unaye shangilia ujinga wa kile kibanda chenu Kama jiko pale ufipa, Nenda mtwara uone jinsi ambavyo wale wananch wapo ktk uchumi up ilihali gesi inatoka huko.
 
Hiyo gesi ni nyingi mno,ndio maana inatakiwa iuzwe ilete fedha za kigeni,zilete maendeleo nchini kwrtu,hivyo ndivyo nchi zote zenye gesi duniani zanafanya,urusi wanauza gesi hadi ulaya na wana bomba la gesi kuelekea nchi nyingi tu
Wale wa shujaa ni ngumu kukuelewa, kwa sababu alikua anafikiri badala yao.
 
mkuu shida kuna watu wana mahaba na mwenda zake hadi hawatumii akili zao tena
Wapumbavu wakubwa hao jamaa

Mijitu mibinafsi sanaaa
Tutawanyoosha pumbavu mkubwa hawa
 
Kwani hii gesi haitumiki au haitatumika kwenye viwanda vya Tanzania? Kama inatumika au itatumika kwenye viwanda vya Tanzania tatizo lipo wapi? Kwani kuna ubaya gani kama una chakula cha kutosha nyumbani kwako ukaamua kumuuzia jirani yako ili kupata pesa ya ziada kufanya mambo yako mengine?

Kama viwanda vya ndani vitakuwa vinatumia hii gesi au vitatumia hii gesi basi mama yupo vizuri sana. Kama taifa lazima tupambane kuuza bidhaa zetu nje ili kupata fedha za kigeni na hiki ndio mama anafanya.

Kuna hoja watu wanaileta kuwa bidhaa za kenya zita-dominate soko la ndani kwa sababu vitakuwa vinazalishwa kwa gharama ndogo hivyo vitauzwa kwa bei ya chini. Hii hoja haina mashiko kama na sisi viwanda vyetu vitatumia gesi kwa sababu vitaweza pia kuzalisha bidhaa kwa gharama ya chini na kupelekea kuuza bidhaa zetu kwa bei ya chini pia.

Mwisho kabisa nawaomba watanzania tumuunge mkono mama. Nasikia mama ni mwanauchumi kitaaluma hivyo anajua anachokifanya, tumpe support atupeleke kwenye nchi ya asali na maziwa. Rais aliyesomea uchumi ndio tunamtaka kwa sasa.
Ujue tz ina gesi nyingi sans
Ila meko kuipenda kwa sababu asingeweza kuiba .bomba la gedi limekuja hadi dsm.
Mradi ulishaisha jk alishaumaliza meko aksu abandon kwa vile he cant steal.

Kwa hio gesi lazima iuzwe kwa majirani
 
Mkuu una uhakika gesi haitutoshi? Hivi unadhani kama kweli gesi haitutoshi mama angeiuza nje? Unadhani mama hana akili mpaka auze nje gesi ambayo sisi wenyewe tunaihitaji? Binafsi nadhani zingine ni propaganda tu. Sidhani mama atakuwa na akili ya kujihujumu mwenyewe.
Wewe unatumia gesi kwa umeme tuanzie hapo kwanza
 
Wewe unatumia gesi kwa umeme tuanzie hapo kwanza
Hapana, situmii gesi kwa umeme ila sijui "kilichoko nyuma ya pazia" kwa nini situmii umeme wa gesi wakati ninaambiwa gesi ipo ya kutosha. Kilichopo nyuma ya pazia ndio fumbo ambalo wengi hatulijui. Kipindi cha Kikwete tuliambiwa gesi ni nyingi sana na mradi wa Kinyerezi ukikamilika umeme utakuwepo wa kutosha na gharama za umeme zitashuka. Baada ya Magufuli kukamata nchi tukaambiwa gesi ilishauzwa kwa mafisadi. "Kilichopo nyuma ya pazia" hatukijua ila nina uhakika mama anakijua ndio maana ameamua na kuiuza nje.
 
Watu hawana jema, kibaya zaidi wanapiga kelele bila hata kujua makubaliano na mkataba unasemaje

Ukiwa na tabia ya unyimi sana unawezajikuta unakufa njaa sababu tuu hutaki kuuza mali usiyoitumia ili mwenye uhitaji aitumie akupe pesa nawe upate chakula
Wasamehe mama. Bado wako kwenye fikra za shujaa, ubongo haukuzoea kufikiri kwa sababu kila aliloliamua lilikua sahihi, watu walitukuza mno mawazo ya shujaa, yaani akili zilishikwa. Sasa lazima muda upite ndipo warudi kwenye uelewa wao. Nakuona umetambua tofauti ya hawa watu wawili.
 
Wabongo wanapenda sana kurukia tu mambo kulichukua na kulishadadia….Gesi sio kwamba haiuzwi Kenya inauzwa hata sasa,kinachotaka kubadilishwa au kuongezwa ni njia tu ya usafirishaji yaani badala ya kutumia malori basi isafirishwe kwa bomba ambalo uendeshaji wake ni rahisi na gharama nafuu
 
Kwani hii gesi haitumiki au haitatumika kwenye viwanda vya Tanzania? Kama inatumika au itatumika kwenye viwanda vya Tanzania tatizo lipo wapi? Kwani kuna ubaya gani kama una chakula cha kutosha nyumbani kwako ukaamua kumuuzia jirani yako ili kupata pesa ya ziada kufanya mambo yako mengine?

Kama viwanda vya ndani vitakuwa vinatumia hii gesi au vitatumia hii gesi basi mama yupo vizuri sana. Kama taifa lazima tupambane kuuza bidhaa zetu nje ili kupata fedha za kigeni na hiki ndio mama anafanya.

Kuna hoja watu wanaileta kuwa bidhaa za kenya zita-dominate soko la ndani kwa sababu vitakuwa vinazalishwa kwa gharama ndogo hivyo vitauzwa kwa bei ya chini. Hii hoja haina mashiko kama na sisi viwanda vyetu vitatumia gesi kwa sababu vitaweza pia kuzalisha bidhaa kwa gharama ya chini na kupelekea kuuza bidhaa zetu kwa bei ya chini pia.

Mwisho kabisa nawaomba watanzania tumuunge mkono mama. Nasikia mama ni mwanauchumi kitaaluma hivyo anajua anachokifanya, tumpe support atupeleke kwenye nchi ya asali na maziwa. Rais aliyesomea uchumi ndio tunamtaka kwa sasa.
Safi sana!!!
Tujenge bomba la ges sambamba na bomba la mafuta@hoima@mu7
 
Wasamehe mama. Bado wako kwenye fikra za shujaa, ubongo haukuzoea kufikiri kwa sababu kila aliloliamua lilikua sahihi, watu walitukuza mno mawazo ya shujaa, yaani akili zilishikwa. Sasa lazima muda upite ndipo warudi kwenye uelewa wao. Nakuona umetambua tofauti ya hawa watu wawili.

Kwani hawajui hili lilikua kwenye mipango muda? Kuamini kwamba shujaa alilikataa hili nalo ni tatizo lingine kwa baadhi yetu

Mungu ibariki Tanzania
 
Hapa tatizo la hao watu wanaopingana na hili la gas kusafirishwa Kenya, ni wale wale ambao akili zao zilishikwa na shujaa na bado mawazo yao yako kwa shujaa.
Chuma cha Africa kimezikwa na akili zao.
 
Kwani hawajui hili lilikua kwenye mipango muda? Kuamini kwamba shujaa alilikataa hili nalo ni tatizo lingine kwa baadhi yetu

Mungu ibariki Tanzania
Kuna mambo mengi tu watu tutaelewa jinsi muda unavyokwenda. Kiongozi akikamata akili za watu wake na kubaki yeye ndiyo final, haya ndiyo madhara yake. Hata akiwa hayupo watu wanabaki kuduwaa wasijue kama jambo hilo linalofanywa sasa liko sahihi au la. Mwanadamu asitukuzwe kiasi cha kumkufuru Mungu.
 
Binafsi huwa naamini kwenye ushauri hata kama angekuwa na hiyo taaluma, maana huwezi kujua vyote.

Na Rais wa nchi kila kitu kinamwangalia yeye, akiamua kwenda peke yake ndo ile tunajikuta tumefika lakini kilichofanyika ni kidogo.
 
Mkuu una uhakika gesi haitutoshi? Hivi unadhani kama kweli gesi haitutoshi mama angeiuza nje? Unadhani mama hana akili mpaka auze nje gesi ambayo sisi wenyewe tunaihitaji? Binafsi nadhani zingine ni propaganda tu. Sidhani mama atakuwa na akili ya kujihujumu mwenyewe.
Nilitegemea zaidi unijibu maswali haya Kama unauhakika gesi ina tutosha,

1)Bei ya gas imeshuka kwa kiasi gani tangu gesi imeanza kutumika TZ?na je kila mwananchi anatumia gas ilikulinda mazingira yetu?nikitegemea kusikia mtungi wa gas n sh 30,000 ili hata wanao ishi vijijini waweze kuona umuhimu wa kutumia gas badala ya mkaa au kuni,then hapo ndipo tuone imetutosha kabisa na tunataka kuuza tupate pesa,nilitegemea tuzalishe umeme wa gas wa kututosha kabisa Tz na umeme huo tuwauzie Kenya Kama bidhaa kwa reasonable price na si Kama malighafi,

2)Je, endapo Kama gas inatumika Kama nishati ya umeme, vipi kwasasa Tz kukatikakatika kwa umeme imebakia historia?

3)Je , niajira ngapi zilizo tengenezwa nchini kutokana na uzalishwaji wa gas?

4)je, n ujazo gani wa gasi ambao tunao Kama akiba ndani ya kisima kule mtwara kiasi kwamba tumejiridhisha kwamba itatutosha kwa miaka mingapi mbeleni? ama nikwamba tunataka kuifyonza yotee iishe, nilitegemea majibu ya waziwazi kabisa kila mtanzania ajue nini tunacho na kwa kiasi gani na kitatutosha mpaka lini,
 
Back
Top Bottom