KERO Gesi yangu inawahi kuisha sana, tuchunguze mitungi yetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ninapenda kuwasilisha malalamiko yangu kuhusu ujazo wa gesi ya kupikia.

Tarehe 24 March 2026 nilijaza gesi kama kawaida lakini cha kushangaza ni kwamba tarehe 10 tu ya mwezi Aprili gesi imeisha, matumizi yangu ni yaleyale ya kawaida ya kila siku, hapo nyuma gesi hiyohiyo ilikuwa inanichukua takribani mwezi mmoja na nusu hadi miwili.

Kwa sasa hali imebadilika ghafla gesi ninayojaza inaisha ndani ya wiki mbili hadi tatu tu, jambo ambalo halikuwa likitokea awali.

Naomba wahusika au wataalamu waeleze: Je, kuna mabadiliko yoyote kwenye ujazo wa mitungi? Inawezekana kuna upungufu kwenye ujazo (underfilling)? Au kuna tatizo lingine ambalo watumiaji tunapaswa kulifahamu? Hii hali inaleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji na gharama zinaongezeka bila sababu ya msingi.

Nipo mji mdogo katoro Kata ya Ludete najazia hapo wakati wote cha kushangaza sa hivi nikijaza haidumu kama zamani na matumizi ni yaleyale niliyozoea.

Pia soma ~ Dar: Wachakachuaji wa gesi za majumbani wakamatwa Malamba mawili
 
Ngoja waje, watakwambia Tafuta hela
 
kabla ya kuuchukua kwa muuzaji upime kwanza kwenye mzani ili kujua una uzito kiasi gani.. ila inaezekana pia wakati mwingine gesi iliyojazwa ndani ikawa imechanganyikana na hewa nyingine isiyohitajika kwenye matumizi.
 
Nimekutana na huu ujinga mwezi uliopita,natumia gas na umeme,gesi inapaswa ikae angalau miezi 3 miezi miwili tu imekata nikajua tu hapa nimepigwa☹️☹️☹️☹️☹️
 
nafikiri muhimu ni kujua, mtungi wako ukiwa umejaza gesi unatakiwa uwe na ujazo gani
uzuri juu ya mitungi huandikwa. Mfano. mtungi wa kilo 15 (maarufu kama mtungi mkubwa wa majumbani;
ukiwa umejaa gesi unatakiwa uwe na kilo 33 hivi. Uzito halisi huandikwa juu ya mtungi...
hivyo pima uone kama upo sawa. Tofauti na hapo badilisha sehemu ya kununua gesi kama ipo nyingine...
KUNA WAUZA GESI WACHACHE WASIO WAAMINIFU WANAJAZIA MITUNGI MTAANI NA HIYO NDIO INAKOSA VIWANGO.
 
Ninapenda kuwasilisha malalamiko yangu kuhusu ujazo wa gesi ya kupikia.

Tarehe 24 March 2026 nilijaza gesi kama kawaida lakini cha kushangaza ni kwamba tarehe 10 tu ya mwezi Aprili gesi imeisha, matumizi yangu ni yaleyale ya kawaida ya kila siku, hapo nyuma gesi hiyohiyo ilikuwa inanichukua takribani mwezi mmoja na nusu hadi miwili.

Kwa sasa hali imebadilika ghafla gesi ninayojaza inaisha ndani ya wiki mbili hadi tatu tu, jambo ambalo halikuwa likitokea awali.

Naomba wahusika au wataalamu waeleze: Je, kuna mabadiliko yoyote kwenye ujazo wa mitungi? Inawezekana kuna upungufu kwenye ujazo (underfilling)? Au kuna tatizo lingine ambalo watumiaji tunapaswa kulifahamu? Hii hali inaleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji na gharama zinaongezeka bila sababu ya msingi.

Nipo mji mdogo katoro Kata ya Ludete najazia hapo wakati wote cha kushangaza sa hivi nikijaza haidumu kama zamani na matumizi ni yaleyale niliyozoea.
Ngoja kwanza unatumia mtunginwa kilo ngapi? na ni wa kampuni gani,baada ya kutujibu hapo ndipo ntakuja nikuulize nijue unavyotumia
 
Huko ulipo kama unaweza kupata Total energys nunua ni nzuri sana mimi natumia gas yake inakaa mnoo
 
Nililazimika kununua microwave ili kupunguza matumizi ya gesi. Tangu hapo nimeshuhudia matumizi madogo ya gesi sababu ishu zote za kupasha viporo ni Kwa microwave tuu
 
Back
Top Bottom