Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Tundu Lissu ni mwanasheria makini na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu. Lakini natilia shaka kama yeye ni mwanasiasa mahiri na pia sijui kama yeye pia anajua nafasi yake aliyopo kisiasa.
Wengi wetu tunajua kuwa tangu mwaka 2005 CHADEMA kwa mara ya kwanza kusimamisha mgombea uraisi, CCM imekuwa inatamani sana CHADEMA igeuke kuwa NCCR ya zama hizi.
Harakati za CCM kuisambaratisha CHADEMA zilikuwa zinafanyika toka nje ya CHADEMA kwa umma dhidi ya CHADEMA.
Lakini tangu baada ya uchaguzi wa mwaka 2020, CCM inaonekana imepata usaidizi usiotarajiwa toka kwa Tundu Lissu.
Lissu inawezekana amejipa daraja la kuirekebisha CHADEMA kutokea nje, badala ya ndani ambako yeye ni mjumbe wa vikao vya chama.
Lissu anakikosoa chama chake kutokea nje kiasi kwamba inazusha maswali mengi sana kumhusu Lissu na kujitambua kwake kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa chama inawezekanaje ukawa si sehemu ya maamuzi ya vikao ambavyo wewe ulishiriki na kufanya mijadala iliyofikia maamuzi husika?
Kama maamuzi ya vikao yalikuwa na makosa, kwa nini yeye aamini kuwa si sehemu ya makosa hayo ya vikao?
Bahati mbaya Lissu kila anachosema sasa kinapokewa kwa chereko kubwa sana toka CCM.
Sasa hivi makada maarufu wa CCM ndiyo wamekuwa ni wasambazaji wakubwa wa kila wanachoona kama ni kiashiria cha mfarakano ndani ya CHADEMA kutokana na maneno yasemwayo na Lissu.
Hawa wana CCM ambao walisema waziwazi kuwa walitamani Lissu angekufa kwenye lile shambilio la Dodoma leo ghafla wamekuwa ni waunga mkono mitizamo ya Lissu?
Lissu mwenyewe anaelewa kinachoendelea?