Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
- Thread starter
- #41
CUF na chama cha Mzee ubwabwa kina tofauti gani kwa sasa?Hata CUF bado ipo...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
CUF na chama cha Mzee ubwabwa kina tofauti gani kwa sasa?Hata CUF bado ipo...
Nasikitika umeanzisha mada nyingine nje ya mada yangu. Nani namkingia kifua?....hapa usimtwishe Lissu kuwa mhusika wa kazi hiyo. Wahusika ni hao unao onekana kuwakingia kifua katika andiko lako.
Kwa sasa lakini kuna kipindi ilikuwa juu pia.. Kama wanavyosema, those who do not learn from history are doomed to repeat itCUF na chama cha Mzee ubwabwa kina tofauti gani kwa sasa?
Wishful thinking though...Tundu Lissu ni mwanasheria makini na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu. Lakini natilia shaka kama yeye ni mwanasiasa mahiri na pia sijui kama yeye pia anajua nafasi yake aliyopo kisiasa.
Wengi wetu tunajua kuwa tangu mwaka 2005 CHADEMA kwa mara ya kwanza kusimamisha mgombea uraisi, CCM imekuwa inatamani sana CHADEMA igeuke kuwa NCCR ya zama hizi.
Harakati za CCM kuisambaratisha CHADEMA zilikuwa zinafanyika toka nje ya CHADEMA kwa umma dhidi ya CHADEMA.
Lakini tangu baada ya uchaguzi wa mwaka 2020, CCM inaonekana imepata usaidizi usiotarajiwa toka kwa Tundu Lissu.
Lissu inawezekana amejipa daraja la kuirekebisha CHADEMA kutokea nje, badala ya ndani ambako yeye ni mjumbe wa vikao vya chama.
Lissu anakikosoa chama chake kutokea nje kiasi kwamba inazusha maswali mengi sana kumhusu Lissu na kujitambua kwake kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa chama inawezekanaje ukawa si sehemu ya maamuzi ya vikao ambavyo wewe ulishiriki na kufanya mijadala iliyofikia maamuzi husika?
Kama maamuzi ya vikao yalikuwa na makosa, kwa nini yeye aamini kuwa si sehemu ya makosa hayo ya vikao?
Bahati mbaya Lissu kila anachosema sasa kinapokewa kwa chereko kubwa sana toka CCM.
Sasa hivi makada maarufu wa CCM ndiyo wamekuwa ni wasambazaji wakubwa wa kila wanachoona kama ni kiashiria cha mfarakano ndani ya CHADEMA kutokana na maneno yasemwayo na Lissu.
Hawa wana CCM ambao walisema waziwazi kuwa walitamani Lissu angekufa kwenye lile shambilio la Dodoma leo ghafla wamekuwa ni waunga mkono mitizamo ya Lissu?
Lissu mwenyewe anaelewa kinachoendelea?
Chama kinachotakiwa kujifunza ni CCM na siyo CHADEMA. Iko siku CCM itakuwa kama KANU ya Kenya au UNIP ya Zambia.kwa hiyo ni kiasi cha kujifunza na kujisahihisha
Misukule ya Mzee Mbowe mnateseka saana.Tundu Lissu ni mwanasheria makini na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu. Lakini natilia shaka kama yeye ni mwanasiasa mahiri na pia sijui kama yeye pia anajua nafasi yake aliyopo kisiasa.
Wengi wetu tunajua kuwa tangu mwaka 2005 CHADEMA kwa mara ya kwanza kusimamisha mgombea uraisi, CCM imekuwa inatamani sana CHADEMA igeuke kuwa NCCR ya zama hizi.
Harakati za CCM kuisambaratisha CHADEMA zilikuwa zinafanyika toka nje ya CHADEMA kwa umma dhidi ya CHADEMA.
Lakini tangu baada ya uchaguzi wa mwaka 2020, CCM inaonekana imepata usaidizi usiotarajiwa toka kwa Tundu Lissu.
Lissu inawezekana amejipa daraja la kuirekebisha CHADEMA kutokea nje, badala ya ndani ambako yeye ni mjumbe wa vikao vya chama.
Lissu anakikosoa chama chake kutokea nje kiasi kwamba inazusha maswali mengi sana kumhusu Lissu na kujitambua kwake kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa chama inawezekanaje ukawa si sehemu ya maamuzi ya vikao ambavyo wewe ulishiriki na kufanya mijadala iliyofikia maamuzi husika?
Kama maamuzi ya vikao yalikuwa na makosa, kwa nini yeye aamini kuwa si sehemu ya makosa hayo ya vikao?
Bahati mbaya Lissu kila anachosema sasa kinapokewa kwa chereko kubwa sana toka CCM.
Sasa hivi makada maarufu wa CCM ndiyo wamekuwa ni wasambazaji wakubwa wa kila wanachoona kama ni kiashiria cha mfarakano ndani ya CHADEMA kutokana na maneno yasemwayo na Lissu.
Hawa wana CCM ambao walisema waziwazi kuwa walitamani Lissu angekufa kwenye lile shambilio la Dodoma leo ghafla wamekuwa ni waunga mkono mitizamo ya Lissu?
Lissu mwenyewe anaelewa kinachoendelea?
Hakuna msukule wa mtu hapa. Jenga hoja ujibiwe kwa hoja. Makosa ya Mbowe hayawezi kuhalalisha makosa ya Lissu.Misukule ya Mzee Mbowe mnateseka saana.
Hakuna mtu ambaye hastahili kujifunza na CHADEMA haina utimilifu wa kutokujifunza.Chama kinachotakiwa kujifunza ni CCM na siyo CHADEMA. Iko siku CCM itakuwa kama KANU ya Kenya au UNIP ya Zambia.
Kwa muktadha Wa hoja yako. Kila hoja ijadili kwa muktadha wake.Hakuna mtu ambaye hastahili kujifunza na CHADEMA haina utimilifu wa kutokujifunza.
Niliwahi kuuliza humu Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? hebu msikieLissu anakikosoa chama chake kutokea nje kiasi kwamba inazusha maswali mengi sana kumhusu Lissu na kujitambua kwake kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa chama inawezekanaje ukawa si sehemu ya maamuzi ya vikao ambavyo wewe ulishiriki na kufanya mijadala iliyofikia maamuzi husika?
Kama maamuzi ya vikao yalikuwa na makosa, kwa nini yeye aamini kuwa si sehemu ya makosa hayo ya vikao?
Lissu mwenyewe anaelewa kinachoendelea?
Mkuu, 'Allen' umetumia akili kubwa katika jibu lako hapa; ila sijui kama unao uhakika kuwa huko kwenye vikao unavyo vizungumzia mambo haya hayakuzungumzwa.Nasikitika umeanzisha mada nyingine nje ya mada yangu. Nani namkingia kifua?
Halafu wengine tunaamini Kuna tofauti kati ya mwanachama Wa kawaida na kiongozi. Kiongozi hutumia vikao na kumalizana na viongozi wenzake ndani ya vikao.
Nakumbuka Mwalimu alipoulizwa ni kwa nini maoni yake kuhusu serikali tatu asiyatoe kwenye vikao vya CCM, jibu lake lilikuwa rahisi tu.alisema yeye hakuwa mjumbe kwenye vikao vyoyote vya CCM kwa wakati ule.
Unaweza usiwe unafugwa na watu, Lakini ni lazima ufugwe na kanuni za taasisi uliyomo.
Kwani unacho kiongea hakitoki kwako? Unajitenganisha vipi na unacho kiongea?Ndio tatizo la watu mlioshikilia siasa kama dini. Mnapenda sana kushambulia watu kuliko hoja. Usinipe tags na dhana zisizo sangu. Deal na nilichokiongea tu
Sasa na Mimi hii ni hoja yangu na Kuna mabandiko niliijadili. Maana inasemwa kiujumla Sana bila kutaja ni kina nani hasa walihongwa.Kiongozi/viongozi akishanunuliwa na Abdul, unadhani hapo bado kuna nafasi ya kuyamaliza maswala ya chama kwenye taratibu tunazo zitambua sote?
Tusilizungushe sana hili bila ya sababu, wakati sote tupo pamoja.Sasa na Mimi hii ni hoja yangu na Kuna mabandiko niliijadili. Maana inasemwa kiujumla Sana bila kutaja ni kina nani hasa walihongwa.
Iringa ambako ndipo Lissu kwa mara ya kwanza alizungumzia mambo ya "fedha za Abdul" kulikuwa na mshangao mkubwa.
Aliyekuwa naye, Peter Msigwa ndiye aliyekuwa anatuhumiwa na wenzake kuchukua fedha hizo za Abdul, Sasa watu wakahoji, imekuwaje anayetuhumiwa anatuhumu wenzake?
Nadhani ni wakati Sasa Kwa Lissu kuwataja hao waliopewa Hela na Abdul ili umma uwajue.
Nakubaliana na wewe kwenye hitimisho lako.Hiyo ndiyo hali iliyopo, na ina wafurahisha sana CCM wakati huu.
Nilitaka nikae kimya, maana ni kama tunarudia yale tunayo kubaliana. Ila nadhani ni muhimu nitaje hapa, kuwa uongozi ndani ya CHADEMA sasa unatuonyesha 'pattern' inayo rudiwa rudiwa kila mara; na siyo mtindo mzuri.Nakubaliana na wewe kwenye hitimisho lako.
Hapo Sasa jee viongozi wa kitaifa (Mwenyekiti na Katibu Mkuu) Wana maslahi gani kwa kutojadiliwa kwenye vikao kwa tuhuma hizo?
Ninachoweza kubashiri inawezekana hakuna uwezo wa kujadili kwa uwazi masuala yenye utata ndani ya vikao vya chama.
Wengine wanadai Mbowe kaambiwa achague kati ya kuwa mgombea Urais 2025 au Mwenyekiti wa chama.
Kuna tetesi kuwa ndani ya Kamati kuu wamegawanyika juu ya hoja hiyo ya ama Mbowe awe Mwenyekiti au mgombea Urais ili Lissu awe mgombea Urais 2025 au Mwenyekiti wa chama.
Wote wawili wameambiwa hawawezi kuwa na yote mawili.
Unajua kuna vyama ni kampuni za mtu havina itikadi za kulinda wala kuendeleza maslahi ya umma ila kumuingiza mtu urais au kuendeleza maslahi yake binafsi na wale wenye hisa kwnye hiyo kampuni. Kule Angola mnakumbuka Unita ya Savimbi au vyama vinavyozuka Kenya kila uchaguzi. Siku hizi Kenya kuna chama kinaitwa UDA. Ndio kimemuingiza Ruto madarakani na yule makamu wa rais aliyetoswa kwa kuzungumzia kuhusu hiza zake kwamba ni za wakikiyu.Tundu Lissu ni mwanasheria makini na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu. Lakini natilia shaka kama yeye ni mwanasiasa mahiri na pia sijui kama yeye pia anajua nafasi yake aliyopo kisiasa.
Wengi wetu tunajua kuwa tangu mwaka 2005 CHADEMA kwa mara ya kwanza kusimamisha mgombea uraisi, CCM imekuwa inatamani sana CHADEMA igeuke kuwa NCCR ya zama hizi.
Harakati za CCM kuisambaratisha CHADEMA zilikuwa zinafanyika toka nje ya CHADEMA kwa umma dhidi ya CHADEMA.
Lakini tangu baada ya uchaguzi wa mwaka 2020, CCM inaonekana imepata usaidizi usiotarajiwa toka kwa Tundu Lissu.
Lissu inawezekana amejipa daraja la kuirekebisha CHADEMA kutokea nje, badala ya ndani ambako yeye ni mjumbe wa vikao vya chama.
Lissu anakikosoa chama chake kutokea nje kiasi kwamba inazusha maswali mengi sana kumhusu Lissu na kujitambua kwake kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa chama inawezekanaje ukawa si sehemu ya maamuzi ya vikao ambavyo wewe ulishiriki na kufanya mijadala iliyofikia maamuzi husika?
Kama maamuzi ya vikao yalikuwa na makosa, kwa nini yeye aamini kuwa si sehemu ya makosa hayo ya vikao?
Bahati mbaya Lissu kila anachosema sasa kinapokewa kwa chereko kubwa sana toka CCM.
Sasa hivi makada maarufu wa CCM ndiyo wamekuwa ni wasambazaji wakubwa wa kila wanachoona kama ni kiashiria cha mfarakano ndani ya CHADEMA kutokana na maneno yasemwayo na Lissu.
Hawa wana CCM ambao walisema waziwazi kuwa walitamani Lissu angekufa kwenye lile shambilio la Dodoma leo ghafla wamekuwa ni waunga mkono mitizamo ya Lissu?
Lissu mwenyewe anaelewa kinachoendelea?
Kama unaijua propaganda ama character assassination kwenye mijadala. Hili swali hukutakiwa hata kuuliza maana ni concepts ndogo sanaKwani unacho kiongea hakitoki kwako? Unajitenganisha vipi na unacho kiongea?
Umeandika upuuzi kama upuuzi wenu hapo WajaTundu Lissu ni mwanasheria makini na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu. Lakini natilia shaka kama yeye ni mwanasiasa mahiri na pia sijui kama yeye pia anajua nafasi yake aliyopo kisiasa.
Wengi wetu tunajua kuwa tangu mwaka 2005 CHADEMA kwa mara ya kwanza kusimamisha mgombea uraisi, CCM imekuwa inatamani sana CHADEMA igeuke kuwa NCCR ya zama hizi.
Harakati za CCM kuisambaratisha CHADEMA zilikuwa zinafanyika toka nje ya CHADEMA kwa umma dhidi ya CHADEMA.
Lakini tangu baada ya uchaguzi wa mwaka 2020, CCM inaonekana imepata usaidizi usiotarajiwa toka kwa Tundu Lissu.
Lissu inawezekana amejipa daraja la kuirekebisha CHADEMA kutokea nje, badala ya ndani ambako yeye ni mjumbe wa vikao vya chama.
Lissu anakikosoa chama chake kutokea nje kiasi kwamba inazusha maswali mengi sana kumhusu Lissu na kujitambua kwake kisiasa.
Makamu Mwenyekiti wa chama inawezekanaje ukawa si sehemu ya maamuzi ya vikao ambavyo wewe ulishiriki na kufanya mijadala iliyofikia maamuzi husika?
Kama maamuzi ya vikao yalikuwa na makosa, kwa nini yeye aamini kuwa si sehemu ya makosa hayo ya vikao?
Bahati mbaya Lissu kila anachosema sasa kinapokewa kwa chereko kubwa sana toka CCM.
Sasa hivi makada maarufu wa CCM ndiyo wamekuwa ni wasambazaji wakubwa wa kila wanachoona kama ni kiashiria cha mfarakano ndani ya CHADEMA kutokana na maneno yasemwayo na Lissu.
Hawa wana CCM ambao walisema waziwazi kuwa walitamani Lissu angekufa kwenye lile shambilio la Dodoma leo ghafla wamekuwa ni waunga mkono mitizamo ya Lissu?
Lissu mwenyewe anaelewa kinachoendelea?
Sio lazima umtaje Mzee Mbowe,maandishi yako tu yanajitosheleza.Ombeni sana Mungu Lissu asiondoke kwa maana ndio utakuwa mwisho wa hii SACCOS.Hakuna msukule wa mtu hapa. Jenga hoja ujibiwe kwa hoja. Makosa ya Mbowe hayawezi kuhalalisha makosa ya Lissu.
Kuna sehemu nimemtaja Mbowe?