Ghafla CCM wanampenda Lissu. Yeye ataingia mtegoni?

....hapa usimtwishe Lissu kuwa mhusika wa kazi hiyo. Wahusika ni hao unao onekana kuwakingia kifua katika andiko lako.
Nasikitika umeanzisha mada nyingine nje ya mada yangu. Nani namkingia kifua?

Halafu wengine tunaamini Kuna tofauti kati ya mwanachama Wa kawaida na kiongozi. Kiongozi hutumia vikao na kumalizana na viongozi wenzake ndani ya vikao.

Nakumbuka Mwalimu alipoulizwa ni kwa nini maoni yake kuhusu serikali tatu asiyatoe kwenye vikao vya CCM, jibu lake lilikuwa rahisi tu.alisema yeye hakuwa mjumbe kwenye vikao vyoyote vya CCM kwa wakati ule.

Unaweza usiwe unafugwa na watu, Lakini ni lazima ufugwe na kanuni za taasisi uliyomo.
 
CUF na chama cha Mzee ubwabwa kina tofauti gani kwa sasa?
Kwa sasa lakini kuna kipindi ilikuwa juu pia.. Kama wanavyosema, those who do not learn from history are doomed to repeat it

Kwa hiyo CHADEMA haipo ilipokuwa, je kuna uwezekano wa kupanda au kushuka zaidi?.. Majibu yote mnayo

Kwa hiyo ni kiasi cha kujifunza na kujisahihisha
 
Wishful thinking though...

Hakununulika kwa Mkapa, JK na Jiwe itakua leo? Inaonekana humjui kijana
 
kwa hiyo ni kiasi cha kujifunza na kujisahihisha
Chama kinachotakiwa kujifunza ni CCM na siyo CHADEMA. Iko siku CCM itakuwa kama KANU ya Kenya au UNIP ya Zambia.
 
Misukule ya Mzee Mbowe mnateseka saana.
 
Chama kinachotakiwa kujifunza ni CCM na siyo CHADEMA. Iko siku CCM itakuwa kama KANU ya Kenya au UNIP ya Zambia.
Hakuna mtu ambaye hastahili kujifunza na CHADEMA haina utimilifu wa kutokujifunza.
 
Niliwahi kuuliza humu Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? hebu msikie
View: https://youtu.be/Qa59DIQs2yI?si=l8ZgJm-QoO4Fj63fP
 
Mkuu, 'Allen' umetumia akili kubwa katika jibu lako hapa; ila sijui kama unao uhakika kuwa huko kwenye vikao unavyo vizungumzia mambo haya hayakuzungumzwa.
Sote tunajuwa kila njia zinazo tumiwa na CCM kukivuruga chama hicho, hadi kununua baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA; labda uwe pia huamini kuwa hilo lipo, kwa kuwa lilisemwa na mtu huyo huyo unaye taka ajadili maswala hayo hayo na hao hao walio nunuliwa!

Hebu nifahamishe, ni kikao kipi cha chama kilicho amua taarifa itolewe kwa umma kukanusha yaliyo semwa na kiongozi wa chama; badala ya kukaa na kuyazungumzia huko huko ndani ya chama kama unavy eleza; na kwa hali ya kawaida nami ningekubaliana nawe juu ya hili?

Kwa hiyo, sioni kuwa nimeingiza mada nyingine kwenye mada yako, kwa maana wewe umejikita upande mmoja wa viongozi, ukifikiri kuwa huko ndani kuko shwari na taratibu zipo kamili. Kiongozi/viongozi akisha nunuliwa na Abdul, unadhani hapo bado kuna nafasi ya kuyamaliza maswala ya chama kwenye taratibu tunazo zitambua sote?
 
Ndio tatizo la watu mlioshikilia siasa kama dini. Mnapenda sana kushambulia watu kuliko hoja. Usinipe tags na dhana zisizo sangu. Deal na nilichokiongea tu
Kwani unacho kiongea hakitoki kwako? Unajitenganisha vipi na unacho kiongea?
 
Kiongozi/viongozi akishanunuliwa na Abdul, unadhani hapo bado kuna nafasi ya kuyamaliza maswala ya chama kwenye taratibu tunazo zitambua sote?
Sasa na Mimi hii ni hoja yangu na Kuna mabandiko niliijadili. Maana inasemwa kiujumla Sana bila kutaja ni kina nani hasa walihongwa.

Iringa ambako ndipo Lissu kwa mara ya kwanza alizungumzia mambo ya "fedha za Abdul" kulikuwa na mshangao mkubwa.

Aliyekuwa naye, Peter Msigwa ndiye aliyekuwa anatuhumiwa na wenzake kuchukua fedha hizo za Abdul, Sasa watu wakahoji, imekuwaje anayetuhumiwa anatuhumu wenzake?

Nadhani ni wakati Sasa Kwa Lissu kuwataja hao waliopewa Hela na Abdul ili umma uwajue.
 
Tusilizungushe sana hili bila ya sababu, wakati sote tupo pamoja.
Haya yanayo letwa nje ya chama na Lissu; yalitakiwa yasemwe kinaga ubaga huko huko ndani ya vikao vya viongozi wa CHADEMA na kupatiwa majibu sahihi ya kuyazima moja kwa moja, huko huko.
Haya yana bubujika hadi nje, ujue kuwa yameshindikana huko ndani. Viongozi walio 'compromized' hawana uwezo wa kuukata mzizi huko huko ndani. Yanabaki tu yanaelea.

Vikao vinge kaa,; kujadili na kufikia uamzi ambao ungetolewa waziwazi kwa wanachama wote na umma. Badala yake; yameachwa tu yabaki yanaelea hivyo hivyo, kila mtu akijazia anavyoona mwenyewe.
Hiyo ndiyo hali iliyopo, na ina wafurahisha sana CCM wakati huu.
 
Hiyo ndiyo hali iliyopo, na ina wafurahisha sana CCM wakati huu.
Nakubaliana na wewe kwenye hitimisho lako.

Hapo Sasa jee viongozi wa kitaifa (Mwenyekiti na Katibu Mkuu) Wana maslahi gani kwa kutojadiliwa kwenye vikao kwa tuhuma hizo?

Ninachoweza kubashiri inawezekana hakuna uwezo wa kujadili kwa uwazi masuala yenye utata ndani ya vikao vya chama.

Wengine wanadai Mbowe kaambiwa achague kati ya kuwa mgombea Urais 2025 au Mwenyekiti wa chama.

Kuna tetesi kuwa ndani ya Kamati kuu wamegawanyika juu ya hoja hiyo ya ama Mbowe awe Mwenyekiti au mgombea Urais ili Lissu awe mgombea Urais 2025 au Mwenyekiti wa chama.

Wote wawili wameambiwa hawawezi kuwa na yote mawili.
 
Nilitaka nikae kimya, maana ni kama tunarudia yale tunayo kubaliana. Ila nadhani ni muhimu nitaje hapa, kuwa uongozi ndani ya CHADEMA sasa unatuonyesha 'pattern' inayo rudiwa rudiwa kila mara; na siyo mtindo mzuri.

Kumbuka ujio wa marehemu Edward Lowassa ndani ya chama- mengi yalibaki bila majibu hadi leo

Kukaja wabunge wanawake 19 wa CHADEMA walivyo ingia Bungeni- hadi leo hakuna mwenye majibu ya kueleza waliingia ingia vipi Bungeni, bila uhusika wowote wa viongozi wa chama chao.

Yakaja mazungumzo ya maridhiano; ambayo hakuna anaye juwa yalifikia wapi

Sasa tena haya ya viongozi ndani ya chama kuwa na makundi

Yote haya hayaonyeshi tofauti kubwa na yale yanayo fanyika ndani ya CCM. Hakuna uongozi unao taka uwazi na kumaliza matatizo bila ya kupindisha pindisha mambo.

Mtindo mbovu kabisa wa uongozi.
 
Unajua kuna vyama ni kampuni za mtu havina itikadi za kulinda wala kuendeleza maslahi ya umma ila kumuingiza mtu urais au kuendeleza maslahi yake binafsi na wale wenye hisa kwnye hiyo kampuni. Kule Angola mnakumbuka Unita ya Savimbi au vyama vinavyozuka Kenya kila uchaguzi. Siku hizi Kenya kuna chama kinaitwa UDA. Ndio kimemuingiza Ruto madarakani na yule makamu wa rais aliyetoswa kwa kuzungumzia kuhusu hiza zake kwamba ni za wakikiyu.
 
Kwani unacho kiongea hakitoki kwako? Unajitenganisha vipi na unacho kiongea?
Kama unaijua propaganda ama character assassination kwenye mijadala. Hili swali hukutakiwa hata kuuliza maana ni concepts ndogo sana
 
Umeandika upuuzi kama upuuzi wenu hapo Waja
 
Hakuna msukule wa mtu hapa. Jenga hoja ujibiwe kwa hoja. Makosa ya Mbowe hayawezi kuhalalisha makosa ya Lissu.

Kuna sehemu nimemtaja Mbowe?
Sio lazima umtaje Mzee Mbowe,maandishi yako tu yanajitosheleza.Ombeni sana Mungu Lissu asiondoke kwa maana ndio utakuwa mwisho wa hii SACCOS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…