Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Ghalib wa GSM atoa vielelezo kuthibitisha Umiliki wa Kiwanja na Nyumba. Aagiza wanasheria kumchukulia hatua anayepotosha umma

Huyu mwanasheria ni poyoyo, huo ushahidi wa GSM ni wa kubumba maana mwenzake kaleta ushahidi wa tangu 2013. Pamoja na udhaifu wa Makonda hapo Riziwani Kikwete anahusika na hii kitu nawahakikishia itakuja kumgharimu yeye na huyo GSM.


Hacha vitisho kwa Riziwani ni wakati wake wa kujidai toeni vielelezo

2013 Makonda alikua hana hata uwezo wa kununua mkate na chai ndio anunue kiwanja cha m 120
 
Inawezekana kutokana na changamoto za awamu ya tano ilibidi kweli GSM wamkabidhi kiwanja Paul Makonda wakakubaliana wa backdate tarehe isomeke 2013 kabla ya Makonda kupata Presidential appointment ambayo inamlazimu ku declare kila mali anayomiliki


Inawezekana pia baada ya JPM kutokuwepo na baada ya kupata baraka za Mamlaka mpya imebidi arudishiwe plot yake

Maana naskia za chinichini wale wote walioporwa mali zao kwa dhulma au kufungwa kwa uhujumu uchumi wanaendelea kuachiwa

Kwanini GSM hataki kueleza mazingira yoyote yaliyosababisha Makonda alazimishe kuwa hicho kiwanja no chake

Kwanini wote Makonda na GSM hawataki kwenda Mahakamani badala yale wote wanashinda kwny mitandao kutulisha story za uongo na kweli

Wote Gharib na Paul kuna ka sehemu muhimu wana ki skip kwny story yao ni sawa na ile story ya Mama Mkwe na Mka mwana kutuhumiana uchawi kwa kuwa walikutana kwa Mgang na kila mmoja hataki ijulikane

Hapo Gharib aende mahakamani kufanya nini wakati title ya kiwanja anayo yeye ni Mali yake , Makonda ndio aende akafungue case akiona anaonewa
 
Lete ushahidi kwamba yote waliyofanya akina Mpina nk.yalikuwa na baraka zake.Short of that haya yatabaki kuwa majungu,uzushi, uongo na chuki binafsi.
Kwani wewe ni Mahakama mpaka nikupe ushahidi? Tumia akili zako kidogo ili usijeonekana kichwa chako ni cha kufugia nywele tu
 
K

Kwaiyo sasahivi police wanavyoua watu na kuwanyanganya mali zao Samia anausika? acheni vitu vya kijinga kumuhushisha Magufuli na ujinga, Nchi hii ni kubwa sana hauwezi futilia kila Mtu,kuna Wakati mlikuwa mnalalamika Wakati anatumbua watu,kuwa Magufuli hafuati utawala wa sheria,amewaacha eti Magufuli amelinda watu wake,bure kabisa wanadamu
mtumishiwaleo laiti ungekaa kimya bila kuandika ungeficha UMBUMBU wako. Huwezi ukamtenga Magufuli na UFEDHULI akina Ole Sabaya na Makonda.

Hata kama alikuwa hajui kama akina Makonda na Sabaya wanadhulumu mali za watu kwa kutumia vyeo vyao vya kiserikali basi naye hana msamaha kwa hilo
 
These are stupid dots.Tuambie unayojua maovu aliyofanya Hayati Magufuli.Hamchoki tu,mnapaka matope hata marehemu!You are so evil.Ni uzuchi tu na kusingizia watu.
Hivi Lissu aliuwawa lini?
 
Huyu mwanasheria ni poyoyo, huo ushahidi wa GSM ni wa kubumba maana mwenzake kaleta ushahidi wa tangu 2013. Pamoja na udhaifu wa Makonda hapo Riziwani Kikwete anahusika na hii kitu nawahakikishia itakuja kumgharimu yeye na huyo GSM.
Mkuu !

Poo Makonda mwaka 2013 ndio alikuwa ametoka kuhitimu Muccobs kwa ufaulu wa alama za chini kabisa.Alitoa wapi milioni 120 ?
 
Makonda nae Atoe vielelezo ili Mamlaka husika ivichunguze Luna VIELELEZO VYA KUGUSHI ili mhusika na Wahusika WASHTAKIWE
hivi kibali cha ujenzi ni kielelezo cha umiliki? Nauliza tu inaweza ikanisaidia na mimi hii kwangu
 
Mtu akija eneo lako kufanya fujo kudai mali ambayo si yake unachotakiwa ni kwenda Mahakamani sio kutishia kwa risasi
G


Hapo Gharib aende mahakamani kufanya nini wakati title ya kiwanja anayo yeye ni Mali yake , Makonda ndio aende ku fungua case akiona anaonewa
 
Binafsi naamini MAKONDA na GHALIB(GSM) "hawakukutana barabarani" , bali wanajuana vizuri tofauti na picha inayojengwa na hili "saga" lao la kugombea kiwanja linaloendelea hivi sasa.

Kwamba Makonda anamtuhumu GSM anataka kumdhulumu na ni mfanyabiashara tapeli, wakati huo huo, GSM anadai kiwanja Ni chake kwa maana kwamba zile hati za kuuziana mbele ya wakili Ibrahim Shinene sio za kweli kwa mujibu wa GSM yaani ni za kughushi(forged documents).

Haihitaji kuwa "Genius" wala "IQ" iliyoshiba kujua kwamba hawa watu wawili, yaani MAKONDA na GSM wote kwa pamoja kuna kitu wanakificha na hawataki kijulikane na umma. Badala yake wote wawili wanacheza "social media game" ili kuvutia upande wao "public sympathy".

GSM wameamua kuchukua hatua hii (maybe ikiwemo kurusha ile clip mitandaoni pamoja na kumtuma wakili wao aongee na waandishi badala ya kwenda Mahakamani) sababu wanajua Makonda anachukiwa sana na watu wengi hivyo wanaamini watu watawaunga mkono dhidi ya Makonda kwa vile wanajua akili zetu wabongo sio za kuhoji bali zipo kimuhemuko zaidi yaani "zipozipo tu".

Na pengine wametuma ujumbe kwa mamlaka zinazomlinda kwamba mtu wenu atawaaibisha.

Baada ya kuona hivi, Makonda kuonyesha kwamba yeye ni "mafia" na kwamba haogopi na yuko tayari kwa lolote, akatumia njia ile ile ya "social media" kupiga mkwara mzito dhidi ya GSM, Polisi na "watu walio nyuma ya GSM". Makonda amefanya hivi ili kubalance hii issue na kuwatishia maadui zake hao kwamba "wakimwaga mboga, atamwaga ugali".

Watu wote wanaomchukia Makonda wako upande wa GSM. Hali kadhalika watu wote wanaompenda Makonda wanamtetea. Kwa mtu makini, bila kufuata hisia binafsi, inabidi ajiulize maswali yafuatayo?

1. Huo ugali anaotaka kuumwaga Makonda ni upi?
2. Je, Makonda from nowhere kaenda kujenga kwenye kiwanja cha GSM? Kwa nini si kiwanja cha mtu mwingine?
3. Wakati Makonda anajenga kwenye hicho kiwanja, GSM walikuwa wanamuangalia tu?
4. Je, Makonda kapata wapi fedha za kununua kiwanja hicho toka kwa GSM, pia kapata wapi pesa za kujenga "mjengo wa maana" kwenye kiwanja hicho?
5. Je, mapato na matumizi ya Makonda yanaakisi mali alizonazo?
6. Je, kwa nini hawa watu hawajaenda kudaiana mahakamani badala yake wamekimbilia mitandaoni?

Laiti kama nchi hii ya Tanzania ingekuwa na viongozi/serikali makini kama ilivyo kwa nchi za wenzetu huko Duniani zilizo na viongozi walio makini wanaochukulia serious uwajibikaji, maadili ya utumishi wa umma, Rushwa pamoja na Ufisadi naamini hili suala lingejulikana mustakali na ukweli wote.

Hili suala haliitaji kuunda tume ya kuchunguza bali a very simple approach ingetosha kupata ukweli, Jibu la nani Muovu kati ya GSM na Makonda lingepatikana kwa kutumia wapelelezi wa Polisi na Takukuru, kiweledi na sio kisiasa.

Lakini kwa kuwa Tanzania ni nchi ambayo Raisi akikupenda hakuna wa kukugusa, raisi asipokukubali utashitakiwa (Ref approach ya Magu na Samia kwa Sabaya) ,Takukuru haikuchunguzi mpaka waamuriwe na Raisi yaani hakuna "Rule of law" katika kuwashughulikia wanasiasa mpaka Raisi atake.

Sitarajii kuona lolote la maana kutoka kwenye mamlaka zinazohusika juu ya suala hili zaidi ya wao "kufunika kombe mwanaharamu apite".
 
Wote waovu, huenda makonda alikichukua enzi akiwa na dar es salaam yake, sasa mpira umerudi kwapani kwa refa.
 
Huyu mwanasheria ni poyoyo, huo ushahidi wa GSM ni wa kubumba maana mwenzake kaleta ushahidi wa tangu 2013. Pamoja na udhaifu wa Makonda hapo Riziwani Kikwete anahusika na hii kitu nawahakikishia itakuja kumgharimu yeye na huyo GSM.
Ushahidi wa Makonda upo wapi?
 
Safi kabisa vielelezo ndio njia nzuri ya kumaliza hili swala!
 
Iko siku wahindi na wenye asili za akina GSM tutawafukuza wote. Sijui anatokea nchi gani. Kinachokera ni ujinga wa kuhusisha kila jambo eti Dkt Magufuli alikuwa mbaya. Nyie subirini, mtakuja tiwa adabu very soon.
Yani inakera sana
 
Huwa matajiri wa afrika hawaheshimiwi huko nje hata siku moja. Utajiri wao hutegemea nani yupo ikulu na wanaiva vipi nae.

Afrika ni bara limejaa matajiri wa misimu, wengi wao wana mambo mengi ya chini kwa chini na hujulikana inapotokea kiongozi mpya anapokuwa kakalia kiti cha ikulu.
Kama matajiri wa russia
 
Back
Top Bottom