Binafsi naamini MAKONDA na GHALIB(GSM) "hawakukutana barabarani" , bali wanajuana vizuri tofauti na picha inayojengwa na hili "saga" lao la kugombea kiwanja linaloendelea hivi sasa.
Kwamba Makonda anamtuhumu GSM anataka kumdhulumu na ni mfanyabiashara tapeli, wakati huo huo, GSM anadai kiwanja Ni chake kwa maana kwamba zile hati za kuuziana mbele ya wakili Ibrahim Shinene sio za kweli kwa mujibu wa GSM yaani ni za kughushi(forged documents).
Haihitaji kuwa "Genius" wala "IQ" iliyoshiba kujua kwamba hawa watu wawili, yaani MAKONDA na GSM wote kwa pamoja kuna kitu wanakificha na hawataki kijulikane na umma. Badala yake wote wawili wanacheza "social media game" ili kuvutia upande wao "public sympathy".
GSM wameamua kuchukua hatua hii (maybe ikiwemo kurusha ile clip mitandaoni pamoja na kumtuma wakili wao aongee na waandishi badala ya kwenda Mahakamani) sababu wanajua Makonda anachukiwa sana na watu wengi hivyo wanaamini watu watawaunga mkono dhidi ya Makonda kwa vile wanajua akili zetu wabongo sio za kuhoji bali zipo kimuhemuko zaidi yaani "zipozipo tu".
Na pengine wametuma ujumbe kwa mamlaka zinazomlinda kwamba mtu wenu atawaaibisha.
Baada ya kuona hivi, Makonda kuonyesha kwamba yeye ni "mafia" na kwamba haogopi na yuko tayari kwa lolote, akatumia njia ile ile ya "social media" kupiga mkwara mzito dhidi ya GSM, Polisi na "watu walio nyuma ya GSM". Makonda amefanya hivi ili kubalance hii issue na kuwatishia maadui zake hao kwamba "wakimwaga mboga, atamwaga ugali".
Watu wote wanaomchukia Makonda wako upande wa GSM. Hali kadhalika watu wote wanaompenda Makonda wanamtetea. Kwa mtu makini, bila kufuata hisia binafsi, inabidi ajiulize maswali yafuatayo?
1. Huo ugali anaotaka kuumwaga Makonda ni upi?
2. Je, Makonda from nowhere kaenda kujenga kwenye kiwanja cha GSM? Kwa nini si kiwanja cha mtu mwingine?
3. Wakati Makonda anajenga kwenye hicho kiwanja, GSM walikuwa wanamuangalia tu?
4. Je, Makonda kapata wapi fedha za kununua kiwanja hicho toka kwa GSM, pia kapata wapi pesa za kujenga "mjengo wa maana" kwenye kiwanja hicho?
5. Je, mapato na matumizi ya Makonda yanaakisi mali alizonazo?
6. Je, kwa nini hawa watu hawajaenda kudaiana mahakamani badala yake wamekimbilia mitandaoni?
Laiti kama nchi hii ya Tanzania ingekuwa na viongozi/serikali makini kama ilivyo kwa nchi za wenzetu huko Duniani zilizo na viongozi walio makini wanaochukulia serious uwajibikaji, maadili ya utumishi wa umma, Rushwa pamoja na Ufisadi naamini hili suala lingejulikana mustakali na ukweli wote.
Hili suala haliitaji kuunda tume ya kuchunguza bali a very simple approach ingetosha kupata ukweli, Jibu la nani Muovu kati ya GSM na Makonda lingepatikana kwa kutumia wapelelezi wa Polisi na Takukuru, kiweledi na sio kisiasa.
Lakini kwa kuwa Tanzania ni nchi ambayo Raisi akikupenda hakuna wa kukugusa, raisi asipokukubali utashitakiwa (Ref approach ya Magu na Samia kwa Sabaya) ,Takukuru haikuchunguzi mpaka waamuriwe na Raisi yaani hakuna "Rule of law" katika kuwashughulikia wanasiasa mpaka Raisi atake.
Sitarajii kuona lolote la maana kutoka kwenye mamlaka zinazohusika juu ya suala hili zaidi ya wao "kufunika kombe mwanaharamu apite".