Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Imekuwa si nadra kusikia ankara za mamilioni ya pesa kwa ajili ya tiba kwenye hospitali za umma.

Nani anayepanga bei hizi na kwa vigezo gani?

Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kwamba kama bei ni kubwa basi kila mtu akaanzishe hospitali yake?

Kama taifa tunakoelekea yaweza kuwa siyo kwema sana.
 
Cost sharing. Zinahitaji fedha kwa ajili ya kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Hazina. Ruzuku inabaki kama sehemu tu ya mapato ya hospitali.

Hayupo anayekataa cost sharing ila break down ya gharama ni vyema vikajulikana, nani anaweka bei na vigezo gani.

Vinginevyo hapa ni ujanja ujanja tu.
 
Hayupo anayekataa cost sharing ila break down ya ghara ni vyema vikajulikana, nani anaweka bei na vigezo gani.

Vinginevyo hapa ni ujanja ujanja tu.
Sidhani kama kuna taasisi inajiamulia gharama bila kuwasilisha kwa kwa umma na wadau kwa ajili ya kutoa maoni Bodi na Waziri mwenye dhamana. Tena gharama hizo zitangazwe kwenye gazeti la serikali na kupewa GN number kama jina na utambuzi. Bila hivyo ni batili na wakishtakiwa hawachomoki.
 
Hili blanket la kusema tu kuhusu bodi haitoshi maana tunaolipa ni sisi iwe moja Kwa moja au kupitia bima.

Ipo hatari kubwa ya kuwa tunapigwa.

Tupewe wazi wazi vigezo hivi maana majengo ni ya umma na wafanyakazi ni wa umma pia.
 
Kila mmoja wetu anatakiwa kuwa na bajeti ya matibabu. Na hapo ndipo inapokuja umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote.

Bajeti ya matibabu ya 10m/- kwa mwanafamilia kwenye nchi yenye tozo na kodi zote zilizopo nchini haiwezekani.

Hali kadhalika hakuna bima ya Afya itaacha kufilisika Kwa bei hizo.

Zingatia msingi wa hoja:

Bei ni kwa kigezo cha ugonjwa, ujuzi, dawa, vifaa au majengo?

Bila kusahau kuwa wawekezaji kwenye vyote hivyo ni sisi wananchi.
 
Imekuwa si nadra kusikia ankara za mamilioni ya pesa kwa ajili ya tiba kwenye hospitali za umma.

Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

Je ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kwamba kama bei ni kubwa basi kila mtu akaanzishe hospitali yake?

Kama taifa tunakoelekea yaweza kuwa siyo kwema sana.
Nikusaidie kitu rafiki!

Hospitali sio mambo ya CCM Vs CDM or CUF.

Kama unafikiri matibabu ni rahisi fungua hospitali yako kama una uwezo huo alafu utuletee mrejesho...
 
Nikusaidie kitu rafiki!
Hospitali sio mambo ya CCM Vs CDM or CUF...
Kama unafikiri matibabu ni rahisi fungua hospitali yako kama una uwezo huo alafu utuletee mrejesho...

Uliyoandika hapo ni yale ya Mwigulu na vyakula.

Kwamba hospitali siyo CCM na hao wengine uliowataja? Kwa sasa mwishoni juu katika kila sekta ni CCM.

Ninachouliza kiko wazi na kama una majibu si uyaweke hapa:

1. Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

2. Je ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Ninaamini kujibu hayo haihitaji rocket science.

Mwongozo wako tafadhali.
 
Hili jambo linashangaza sana mkuu, iweje hospitali ya umma gharama zake ziwe sawa na private wakati vifaa, wataalamu na wahudumu wanalipwa na serikali?Kuna siku nilipeleka kipimo kwa ajili ya dogo pale muhimbili nikaambiwa elfu 80, kipimo cha kawaida kabisa. Bora waseme sasa kwamba serikali imejitoa kwenye kuhudumia afya za wananchi kila mmoja abebe msalaba wake kama walivyofanya kwenye bure elimu.​
 
Hili jambo linashangaza sana mkuu, iweje hospitali ya umma gharama zake ziwe sawa na private wakati vifaa, wataalamu na wahudumu wanalipwa na serikali? Kuna siku nilipeleka kipimo kwa ajili ya dogo pale muhimbili nikaambiwa elfu 80, kipimo cha kawaida kabisa. Bora waseme sasa kwamba serikali imejitoa kwenye kuhudumia afya za wananchi kila mmoja abebe msalaba wake kama walivyofanya kwenye bure elimu.....​
Hii nchi hata hospital ziwe kila mtaa , Watanzania wengi hawawezi kumudu huduma kubwa ...Tunajua watanzania ni masikini ila bado gharama ni kubwa unaweza kufa huku unajiona.
 
Cost sharing. Zinahitaji fedha kwa ajili ya kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Hazina. Ruzuku inabaki kama sehemu tu ya mapato ya hospitali.
Kwenye hospitali ya umma cost sharing haiwezi kuwa kuweka gharama zinazoendana na hospitali binafsi, kwani kodi za wananchi ndo zinazoendesha hospitali hizo ikiwemo kulipa mishahara ya wataalamu na wahudumu, kununua vifaa tiba na madawa nk. Huwezi kutoza kipimo cha kawaida cha makohozi elfu 80 kwenye hospitali ya umma kwa kisingizio cha cost sharing, ingekuwa elfu 5 ingeeleweka kwamba ni kuchangia gharama.
 
Jambo la kushangaza wizara ya afya inapewa bajeti kubwa sana kwa wa ajili ya mishahara, madawa na vifaa tiba. Majengo ya hospitali yamejengwa kwa fedha za umma, wahisani na wananchi wanajitolea.

Sasa tuelezwe gharama kubwa kiasi hiki kinasababishwa na nini?
 
Hili jambo linashangaza sana mkuu, iweje hospitali ya umma gharama zake ziwe sawa na private wakati vifaa, wataalamu na wahudumu wanalipwa na serikali? Kuna siku nilipeleka kipimo kwa ajili ya dogo pale muhimbili nikaambiwa elfu 80, kipimo cha kawaida kabisa. Bora waseme sasa kwamba serikali imejitoa kwenye kuhudumia afya za wananchi kila mmoja abebe msalaba wake kama walivyofanya kwenye bure elimu.....​

Mkuu tatizo pia siyo kuwa gharama ni kubwa kama za private tu.

"Private unawaelewa wao wamejenga zao kama anavyosema Bashe."

Tatizo hapa ni kwa nini ni bei hizo zilizopo.

1. Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?
2. Je ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Iko kama lengo ni kuhakikisha tunakuwa mafukara kweli kweli.
 
Tena unaweza kuta private bei ziko chini na huduma ni za uhakika.......vinginevyo pesa nyingi za umma zinazoelekezwa afya zisitishwe ili tujue kwamba wanajiendesha asilimia mia.
 
Hii nchi hata hospital ziwe kila mtaa , Watanzania wengi hawawezi kumudu huduma kubwa ...Tunajua watanzania ni masikini ila bado gharama ni kubwa unaweza kufa huku unajiona.
Kwanini gharama hizi kubwa?

Nani anayepanga bei hizi na kwa vigezo gani?

Je ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Tungeanzia hapa tukafahamishana badala ya kukubali tu kuwa gharama ni kubwa.
 
Watu wanajadili vitu vya maana wewe unaleta uchawa wako wa CCM!

Hali kama hizi ndizo zinazotuweka kwenye kuchukuliwa poa.

Mtanzania mjinga akisha aminishwa jambo hubakia kukenua kama huyo ndugu.

Ndiyo maana waziri anadiriki kusema tukalime vyetu na watu bado wanakenua badala ya kumwajibisha.
 
Back
Top Bottom