Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Mimi huwa najiuliza ikiwa tuu NHIF, ambayo wenye hiyo bima nchi nzima ni wachache, je hii bima ya afya kwa wote ndiyo itawezekana kweli?
Kwa gharama zinazotozwa kuwa kubwa kuliko uhalisia, unaenda kuleta ufisadi wa kutisha na kuua mfuko au mfuko kushindwa kugharamia matibabu inavyotarajiwa. Inafikia kipindi mnaenda mnaambiwa kipimo hiki hakimo kwenye bima, dawa hii haitolewi na bima, matibabu haya hayatolewi na bima, mnaambiwa mtoe pesa......
 
Gharama zipo za aina Mbili.

Kwa Hospitali kubwa (mashirika yanayojitegemea gharama zinapangwa na bodi ya Hospitali ).

Kwa hospital za Wilaya, vituo vya Afya gharama zinapangwa na Halmashauri.

Vyanzo vya mapato ya Hospitali huwa ni Kama ifuatavyo:

  • BIMA
  • Kama huna Bima utalipa gharama zifuatazo:
  • Kumuona Daktari ( Medical consultation ).

Daktari akikuandikia vipimo ukifika Maabara utalipia.

Ukirudi kwa Daktari akikuandikia Dawa ukienda duka la Dawa utalipia.

Ikitokea UKALAZWA utalipia Kitanda kwa siku kulingana na gharama za Kituo husika.

Ukifa, ndugu zako watalioia gharama za mortuary kulingana na siku ulizokaa.
Ukilazwa siku 10 kwa nini kila siku unalipishwa gharama za daktari, manesi etc halafu mbaya zaidi huko wodini wanaokuwa na wagonjwa ni madaktari wanafunzi, maktari bingwa huwaoni lakini unalipishwa costs zao why?
 
Kama ilivyo sekta zingine pana haja ya hizi bei kuwa kuwa regulated. Watu hawawezi kujipangia tu kiholela hivi. Labda tu kama lengo ni kuwafilisi watu au hiyo mifuko kama inavyojili.
Naunga mkono hoja kuwe na chombo cha ku regulate gharama za mahospitalini kama ilivyo LATRA nk
 
Nipo Kwenye field ya medical
Serekali inatoa pesa nyingi mno kusaidia makali na zinaonekana wazi kabisa

Wewe ulie nje ndie unarusha mate

Hakuna gharama Kali kama za afya kwenye maisha

Weka bima Yako ya afya au tafuta pesa , hospital za serekali pia zina social office unaenda wanakusikiliza kama wewe ni pimbi huwezi tafuta pesa wanakusaidia
Umeshindwa kuja na justifications unaanza kuita watu pimbi. Na hili ni tatizo lingine la wafanyakazi wa serikali, kibri na dharau, kama yule waziri aliyesema wenzake wakajadili hoja za uganga wa kienyeji... Watu kama ninyi unaweza kukuta eti ndiyo mmepewa jukumu la kupanga bei, so ni lazima kuwa na chombo cha kuwa regulate na kuwarudisha kwenye mstari.
 
Kitanda umelipa 3000 it's so cheap wakati sehemu zengine hospital za serekali tunalipa per day tsh 25000/ hiyo ni private room sio icu lakini unajiuliza mwanachi wa kawaida alotakiwa aienjoy huduma hizi ndani ya hospital za serekali analipishwaje tsh 25000 na tozo lukuki zinazomsubiria huko nje kwenye ukamuaji mwengine alosema tuamamie Burundi kweli alimaanisha
Mimi nina bili hapa kitanda kwa siku 50,000....
 
Ukilazwa siku 10 kwa nini kila siku unalipishwa gharama za daktari, manesi etc halafu mbaya zaidi huko wodini wanaokuwa na wagonjwa ni madaktari wanafunzi, maktari bingwa huwaoni lakini unalipishwa costs zao why?
Wapi huko?
 
Ukilazwa siku 10 kwa nini kila siku unalipishwa gharama za daktari, manesi etc halafu mbaya zaidi huko wodini wanaokuwa na wagonjwa ni madaktari wanafunzi, maktari bingwa huwaoni lakini unalipishwa costs zao why?

Angalia gharama hizi za bima Ili kuyalipia hayo uliyoorodhesha:

Masharti mapya bima afya yaanza
 
Pamoja na hiyo cost sharing lakini wakati mwingine hizo gharama huwa haziendani kabisa na huduma iliyotokewa, nitatoa mfano: mgonjwa wetu alipelekwa Mloganzila baada ya kubainika na matatizo ya Figo. Baada ya kupokewa alikaa bila huduma mpaka siku ya 5 (huduma ya kusafisha damu). Huduma halisi ya kusafisha damu ilianza day 6 na baada ya siku 2 akafariki. Katika kipindi chote hicho waliokuwa wanashughulika na mgonjwa ni wanafunzi, daktari nilimuona only one day. Sasa njoo kwenye bili sasa yaani siku zote alizokuwa pale wameweka mpaka gharama za madaktari, manesi, etc... Yaani unakuta kabisa daktari hajaja kumuona mgonjwa pale wodini, ni wale wanafunzi ndiyo wapo hapo ku attend wagonjwa lakini eti bili inasoma gharama za daktari hii ni uonevu. Unaambiwa gharama za kitanda elfu 50 kwa mfano lakini hapo hapo mpaka gloves na vifaa vingine viko kwenye bili pia. Sasa unajiuliza hicho kitanda ndiyo elfu 50?? Hata hotel ukilipa 50,000 utakuta sabuni, taulo, na breakfast juu...

Tuna nchi ya hovyo sana kiuongozi
 
Back
Top Bottom