Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kama 'think tank' kwa nini asijipendelee kwa sasa, akijua kuwa kesho kwenye hiyo nafasi hatokuwepo?Si umesema alikaa kwenye kikao , Yani yeye ndie think tank
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama 'think tank' kwa nini asijipendelee kwa sasa, akijua kuwa kesho kwenye hiyo nafasi hatokuwepo?Si umesema alikaa kwenye kikao , Yani yeye ndie think tank
Nakupongeza sana kuendelea kubishana na huyu KIBUYUKwanini mmeshindwa Kuweka za halali na zisizo halali ?
Weka huduma kadhaa linganisha na nchi nyingine tuone kwetu zipo juu
Sio kila mtu anakuwa front Kuna ma think tank wanalipwa kwa kuwa think tankUko sahihi, lakini amezalisha nini?
Kwanini mmeshindwa Kuweka za halali na zisizo halali ?
Weka huduma kadhaa linganisha na nchi nyingine tuone kwetu zipo juu
Ukiona umepuuzwa mkumbuke kiumbe Pimbi 🤣🤣Nakupongeza sana kuendelea kubishana na huyu KIBUYU
Anaekunywa pombe analipa Kodi kubwa Sana ya VAT kuliko anaeshindwa kununua maharage
Halali inalinganishwa na haramu ili uwe na haramu lazima uwe na halaliZa halali au za haramu siyo namba inayotoka mbinguni.
Uhalali na ujaramu unatokana na ghrama za uzalishaji.
Kama gharama ya kuzalisha huduma ni thamani "x" na tunauziwa "10,000x" bei hiyo siyo halali.
Ninyi mnaodhani bei zenu mnazotupa ni halali ziko wapi "x" tujiridhishe?
Relax niangalie Mpira , karibu mkapa
Nini usichoelewa? Weka itemized cost ya unachouza tujiridhishe?Halali inalinganishwa na haramu ili uwe na haramu lazima uwe na halali
Weka apa haramu na halali
Relax niangalie Mpira , karibu mkapa
Ingekuwa hivyo, tungekuwa na visima vingi vya kuchimba mafuta na kuuza njeSio kila mtu anakuwa front Kuna ma think tank wanalipwa kwa kuwa think tank
Na mnywa pombe ndie analipa Kodi kubwa mno direct kabisa
Alafu mnalia apa Kodi yake ukilipie huduma binafsi
Ila we jamaa bana , ungechimba mafuta unajua mafuta yapo kila sehemu 😂😂😂Ingekuwa hivyo, tungekuwa na visima vingi vya kuchimba mafuta na kuuza nje
Ni wazawa wangapi wapo kwenye utafiti wa kujua hapa kuna mafuta au hapana?Na je, wametoa mapendekezo gani, na hatua zipi zimechukuliwa?Ila we jamaa bana , ungechimba mafuta unajua mafuta yapo kila sehemu 😂😂😂
Hebu tupe hizo bei za private vs Umma. Acha bla bla ku justify andiko lako.
Waache blaablaa aisee mimi nimelipishwa 250,000 Moshi kcmc hosptal kubwa kabisa...
Hata kama ni cost sharing gharama ni kubwa sana hazina Uwiano ukizingatia hiyo ni serikaliCost sharing. Zinahitaji fedha kwa ajili ya kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Hazina. Ruzuku inabaki kama sehemu tu ya mapato ya hospitali.
Hata kama ni cost sharing gharama ni kubwa sana hazina Uwiano ukizingatia hiyo ni serikali
Jana na juzi watu wawili nimewasikia wanalalamika, mmoja mtoto mchanga amelazwa Amana siku 5 bill ikaja laki 3.
Akapewa referral kwenda Muhimbili amkaa wiki bill mil 1 na ushee.
Mimi mwaka juzi mke wangu alifanyiwa operesheni kutoa mtoto aliyefia tumboni akakaa pale siku ICU siku kama 3 na wodini siku 2 bili ikaja mil 2 na ushee nikawaambia kulikoni wakasema hakuna namna kama huna aendelee kukaa wodini siku ukipata unakuja kumkomboa
Pamoja na hiyo cost sharing lakini wakati mwingine hizo gharama huwa haziendani kabisa na huduma iliyotokewa, nitatoa mfano: mgonjwa wetu alipelekwa Mloganzila baada ya kubainika na matatizo ya Figo. Baada ya kupokewa alikaa bila huduma mpaka siku ya 5 (huduma ya kusafisha damu). Huduma halisi ya kusafisha damu ilianza day 6 na baada ya siku 2 akafariki. Katika kipindi chote hicho waliokuwa wanashughulika na mgonjwa ni wanafunzi, daktari nilimuona only one day. Sasa njoo kwenye bili sasa yaani siku zote alizokuwa pale wameweka mpaka gharama za madaktari, manesi, etc... Yaani unakuta kabisa daktari hajaja kumuona mgonjwa pale wodini, ni wale wanafunzi ndiyo wapo hapo ku attend wagonjwa lakini eti bili inasoma gharama za daktari hii ni uonevu. Unaambiwa gharama za kitanda elfu 50 kwa mfano lakini hapo hapo mpaka gloves na vifaa vingine viko kwenye bili pia. Sasa unajiuliza hicho kitanda ndiyo elfu 50?? Hata hotel ukilipa 50,000 utakuta sabuni, taulo, na breakfast juu...Cost sharing. Zinahitaji fedha kwa ajili ya kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Hazina. Ruzuku inabaki kama sehemu tu ya mapato ya hospitali.
Bima tuu ya NHIF inabagua matibabu, mara huduma hii bima haiko covered na bima, sasa ndiyo bima kwa watanzania wote milioni 61 itawezekana kweli?Kila mmoja wetu anatakiwa kuwa na bajeti ya matibabu. Na hapo ndipo inapokuja umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote.
Exactly mfano hapo Mloganzila au MOI, wanakupa bili ikionyesha kwamba kuna gharama za kila siku za madaktari, manesi etc kumbuka hiyo ni mbali na gharama za kitanda na vifaa mbalimbali na madawa. Huwa najiuliza kwanza unakuta madaktari wenyewe wanakuja mara chache most of the time ni wanafunzi ndo wako wodini, lakini kwa nini kuwe na gharama za madaktari na manesi daily? Hawa si wanalipwa mishahara? Kwa nini kusiwe na consultancy fee inayolipwa just once? Kwani hii ni private hospital? Majengo yamejengwa kwa fedha za umma, vifaa vyote ni vya umma etc etcHili blanket la kusema tu kuhusu bodi haitoshi maana tunaolipa ni sisi iwe moja Kwa moja au kupitia bima.
Ipo hatari kubwa ya kuwa tunapigwa.
Tupewe wazi wazi vigezo hivi maana majengo ni ya umma na wafanyakazi ni wa umma pia.