Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Exactly mfano hapo Mloganzila au MOI, wanakupa bili ikionyesha kwamba kuna gharama za kila siku za madaktari, manesi etc kumbuka hiyo ni mbali na gharama za kitanda na vifaa mbalimbali na madawa. Huwa najiuliza kwanza unakuta madaktari wenyewe wanakuja mara chache most of the time ni wanafunzi ndo wako wodini, lakini kwa nini kuwe na gharama za madaktari na manesi daily? Hawa si wanalipwa mishahara? Kwa nini kusiwe na consultancy fee inayolipwa just once? Kwani hii ni private hospital? Majengo yamejengwa kwa fedha za umma, vifaa vyote ni vya umma etc etc

Staajabu ya Mussa ndugu mrejesho wa wengi waliokwenda India na South Africa Bei huko ni nafuu zaidi na cases za "wrong diagnosis" kutokea nyumbani zimekuwa zikisikika:

Mgonjwa adai fidia TMJ, Hindu Mandal
 
Mwaka jana september nilipata mtihani wa kumuuguza mama pale Muhimbili ikafika mahali akahitajika afanyiwe MRI unfortunately bima niliyomkatia NHIF iliyoni-cost Tsh 360,000/= ikawa haiwezi ku-cover hicho kipimo nikaambiwa nitalipa cash.

Nikawauliza bei gani nikaambiwa kwa mgonjwa wa cash ni 210K nikasema aipitishe ili mama apewe huduma kuingiza jina la mgonjwa wakasema huyu ameingia hapa kwa bima so itabidi ilipwe 450K,nilipata mfadhaiko sana nikaona kama napigwa wakanielekeza kwa msimamizi wa kitengo nikaenda akanionyesha ipo kabisa kwenye system zao.

Mpaka namaliza matibabu ya mgonjwa wangu sikuwahi kupata jibu kwamba kwanini mtu akiwa na bima na asiyekuwa na bima kipimo kile kile kinatofautiana bei kwa ukubwa ule?kama kawaida yetu wabongo nikanung'unika tu moyoni huku nikishukuru mzazi kupona.
Niliwahi kukutana na situation kama hiyo pale MOI na sikuwahi kupata majibu, Mpaka nililalamika kwa waziri wa afya kupitia page yake ya Twitter niliambulia kujibiwa kuwa nipe details zako ili niufuatilie but mpaka mgonjwa anaruhusiwa sikupata msaada wowote.
 
NHIF wameifanya kichaka cha kupiga pesa kwa hizi hospitali kuweka gharama kubwa za vipimo na matibabu zisizo na uhalisia. Ndo maana ili NHIF iweze kuwa sustainable itabidi wafungue hospitali zao wenyewe....
Mimi huwa najiuliza ikiwa tuu NHIF, ambayo wenye hiyo bima nchi nzima ni wachache, je hii bima ya afya kwa wote ndiyo itawezekana kweli?
 
pamoja na uzalendo na kila kitu lkn lazima ifaamike pi akuwa gharama za matibabu ni kubwa dunia nzima ni sio kwetu hapa. Sasa ndio maaan kuepuka dhahma kama hii srikali ikaja na mpango wa bima kwa wote ili hizi ghrama ziwe shared kupitia bima na kuleta unafuu na uhakika wa huduma pia. Hakuna namna hizi taasisi za afya ziaweza kujiendesha bila pesa, maana zinahitaji pesa kufanya tafiti , kulipa hao wataalamu na kuwekeza kwenye vifaaa na majengo ilio hizo tiba tunazifuata nje zipatikane hapa ndani
Bajeti ya Wizara ya afya huwa ni kwa ajili ya kugharimia nini? Lakini kama mleta mada ulivyouliza hizi bei hupangwa kwa kuzingatia vigezo gani?
 
Gharama kubwa hazitoki mbinguni. Kwa nini hatupeani vigezo vya bei hizo Ili tukubaliane sote kuwa dialysis Kwa mfano gharama yake ni 400,00/- kwa mpigo na hufanyika angalau mara 2 kwa wiki?

Tukajua gharama hizo zinatokana na:

1. Umeme kiasi kiasi gani?
2. Maji kiasi gani?
3. Ujuzi kiasi gani?
4. Chemicals kiasi gani?
5. Sindano kiasi gani?
6. Nk

Vivyo hivyo kwa MRI, CT scan, Ventilator, ICU, kulazwa, machela, nk?

Kwa bei hewa hIzi tunazoona haupo mfuko wa bima wala mtu atakayeweza ku survive.

Kimsingi lengo la serikali hapa litakuwa ni kufukarisha watu kwa kisingizio cha gharama kubwa zisizokuwapo.
Well said [emoji120] [emoji120]
 
mkuu mada yako ina mashiko sana ila serikali ya ccm inajua jinsi gani inawanyonya wananchi ilo uwezi kuwafundisha, kwanza hawakomi kudhulumu, ili la afya ndio sehemu zao pendwa kuwapiga walalahoi
Huwa najiuliza hypothetically kwamba hivi ingekuwa Bima ya afya kwa wote imefanikiwa je bei za vipimo, madawa na gharama zingine zingekuwa za kawaida mfano kupima malaria elfu 2 au napo ingekuwa zaidi (mara 2 ya bei ya kawaida) kwa sababu ni bima?
 
Niliwahi kukutana na situation kama hiyo pale MOI na sikuwahi kupata majibu, Mpaka nililalamika kwa waziri wa afya kupitia page yake ya Twitter niliambulia kujibiwa kuwa nipe details zako ili niufuatilie but mpaka mgonjwa anaruhusiwa sikupata msaada wowote.

Waziri katumwa pesa:

Watendaji CCM jukumu la kwanza ni kusifia sifia

Hicho ni kigezo #2 muhimu kutimba kitchen cabinet.
 
Ndio mana kuna ishu ya bima ya Afya ambayo malipo yake ni kidogo lakini ita cover haya mambo yote, leo mtu anapinga 340,000 km malipo ya bima ya Afya Kisha akipewa gharama halisi qnalalaika inakuwaje? Tujifunze
Umeambiwa hapo juu mtu Kalipa bima ya afya 340,000 lakini kaambiwa kipimo cha MRI hakipo kwenye Bima na anatakiwa kulipa cash laki mbili na ushee, sasa anaenda kulipia anaambiwa huyo mgonjwa ana bima (ambayo wahusika wamesema hicho kipimo hakiko covered) hivyo anatakiwa kulipa laki 4 na ushee, yaani mara 2 zaidi ya mtu asiye na bima. Sasa tuambie wewe nini hasa logic behind that? Hivi from that experience next time si mgonjwa ataamua aseme hana bima?? Mbona kwenye elimu ambako serikali imewekeza huduma ya elimu siyo ghali kihivyo? Hatukatai kuchangia gharama lakini hii kitu iwe transparent kwa kila mtu na kwenye mahospitali...
 
Tunajua kuwa amekaa hospitali kwa kipindi gani? Zimetumika gharama kiasi gani za ununuzi wa dawa na baadhi ya matibabu yamekwendaje? Yawezekana kwa kiasi hicho cha pesa angekwendq India ingekuwa zaidi ya milioni hamsini huko, lazima tulinganishe huduma na gharama za matibabu mana serikali ikiboresha huduma gharama nazo lazima ziongezeke hata kwa kiasi fulani
Hivi mgonjwa akikaa hospital siku 10 huwezi kumpa bili kuonyesha gharama za kitanda kwa siku, madawa etc?
 
Huduma siyo anasa. Hospitali inalipa umeme, maji, wataalamu ,matengenezo ,madawa na uchunguzi na vitu vingine vingi . Ni muhimu sana kuchangia matibabu ili kuwa na uhakika wa uendeleevu wa utoaji huduma katika vituo vyetu vya afya. Hili linawezekana tu pale kila mtu atakapokuwa na bima. Nguvu yetu iende huko ,tusipolipa kesho tutashindwa kutoa huduma kwa watanzania wengine .Bima inaweza onekana haina umuhimu ila ukikata bima inaweza kuokoa mamilioni ya fedha ,UGONJWA HAUPIGI HODI
Hii BIMA ya wote unayong'ang'ania bado ni kitendawili kwa sababu kwanza kwa maisha ya watanzania milion 61 ni wangapi wana uwezo wa kulipa let's say laki 3 kwa mwaka ili apate full treatment? Imagine wafanyakazi tuu under NHIF yenye uhakika wa malipo kila mwezi, bado kuna vipimo na dawa utaambiwa havimo kwenye Bima, sasa najiuliza hiyo bima kwa wote itaweza kweli? Ngoja tuone muswaada utakapikuwa sheria.
 
Kuiondoa ccm madarakani sio solution. Solution hapa ni Mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambao utakua mfumo rfiki wa kuhakikisha Matibabu kwa wote yanakua sawa
Bima ya afya kwa wote si ndiyo wanavutana huko bungeni? Tuambie nini kimekwamisha huo muswaada bunge la juzi?
 
Hii BIMA ya wote unayong'ang'ania bado ni kitendawili kwa sababu kwanza kwa maisha ya watanzania milion 61 ni wangapi wana uwezo wa kulipa let's say laki 3 kwa mwaka ili apate full treatment? Imagine wafanyakazi tuu under NHIF yenye uhakika wa malipo kila mwezi, bado kuna vipimo na dawa utaambiwa havimo kwenye Bima, sasa najiuliza hiyo bima kwa wote itaweza kweli? Ngoja tuone muswaada utakapikuwa sheria.

Kama unavyowaona hapa:

FpPZ7dKWAAMHQrq.jpeg
 
Hana lolote huyu bima ya afya imefilisika kutokana na serikali ya ccm kuchota pesa hovyo hovyo, wanataka kufufua kwa lazima kwa kunyonya wananchi
Bima ya afya kwa wote si ndiyo wanavutana huko bungeni? Tuambie nini kimekwamisha huo muswaada bunge la juzi?
 
Hana lolote huyu bima ya afya imefilisika kutokana na serikali ya ccm kuchota pesa hovyo hovyo, wanataka kufufua kwa lazima kwa kunyonya wananchi

Yaonesha mawaziri na warendaji kuwa na majukumu 2 makuu:

1. Kumsifia sifia mwenyekiti kwa lolote hata kama halina tija.
2. Kufanikisha kuchukua pesa kwa wananchi kwa namna yoyote hata kama ni kwa unyang'anyi.

Uzi huu hapa umejielekeza:

Watendaji CCM jukumu la kwanza ni kusifia sifia
 
Sekta ya Afya inahitaji fedha kujiendesha ndio maana wananchi tunapaswa kuchangia ,je ? Gharama ya matibabu ya moyo au figo inaweza kuwa sawa na mtu anayeumwa malaria ?? Utaalamu na vifaa vinalingana ?? Tusiongee mambo kwa ushabiki tukateni Bima za Afya ,serikal kwa sasa inafanya kazi nzuri ya kuleta teknolojia pamoja na ujenzi wa mahospital ya kisasa nchi nzima ,huu wakati wa ujenzi wananch hatuna budi kuchangia ili huduma iendelee BIMA BIMA BIMAA ni muhimu ndugu zangu
Bima ya afya iliyoboreshwa inaweza kulipia magonjwa ya Figo na moyo? NHIF inaweza kufanya kipimo cha MRI? inaweza kufanya Dialysis au kuzibua mishipa ya moyo? Hebu nisaidie tafadhali.
 
mkuu embu fikiria kidogo kila mtu ana bima ya afya ya sh laki tatu, alafu unakwenda hospitali unaambiwa panado hakuna, we utafanya nini?
Mradi wa mwendo kasi nauli ni kubwa kuliko daladala lakini upo ICU, Bima ya afya ni upigaji tu hakuna cha kuboresha huduma
Kwanza ni kwa mazingira gani mtanzania wa kawaida ataweza kulipa bima ya afya sh laki tatu? Ile ya elfu 40 tuu huko vijijini imeshindikana sembuse laki tatu? Mwaka jana nilitembelea shule moja ya msingi huko mikoa ya magharibi aisee zaidi ya 70 % ya wanafunzi wako pekupeku, yaani hata zile yebo yebo za buku jero imeshindikana kununuliwa. Jamani huko vijijini watu wako hoi kweli kweli.
 
Kwanza ni kwa mazingira gani mtanzania wa kawaida ataweza kulipa bima ya afya sh laki tatu? Ile ya elfu 40 tuu huko vijijini imeshindikana sembuse laki tatu? Mwaka jana nilitembelea shule moja ya msingi huko mikoa ya magharibi aisee zaidi ya 70 % ya wanafunzi wako pekupeku, yaani hata zile yebo yebo za buku jero imeshindikana kununuliwa. Jamani huko vijijini watu wako hoi kweli kweli.
Kuna mtu hapa dar analipwa sh 3500 kwa siku masaa kumi na mbili kiwandani , piga hesabu kwa mwezi, halafu fanya Kama unatoa kwa laki tatu

Huyu mtu ana familia halafu kapanga, huyu Ni wa mjini Kijiji Ni hali mbaya zaidi
 
Back
Top Bottom