Gharama zipo za aina Mbili.
Kwa Hospitali kubwa (mashirika yanayojitegemea gharama zinapangwa na bodi ya Hospitali ).
Kwa hospital za Wilaya, vituo vya Afya gharama zinapangwa na Halmashauri.
Vyanzo vya mapato ya Hospitali huwa ni Kama ifuatavyo:
- BIMA
- Kama huna Bima utalipa gharama zifuatazo:
- Kumuona Daktari ( Medical consultation ).
Daktari akikuandikia vipimo ukifika Maabara utalipia.
Ukirudi kwa Daktari akikuandikia Dawa ukienda duka la Dawa utalipia.
Ikitokea UKALAZWA utalipia Kitanda kwa siku kulingana na gharama za Kituo husika.
Ukifa, ndugu zako watalioia gharama za mortuary kulingana na siku ulizokaa.