Gharama kubwa hazitoki mbinguni. Kwa nini hatupeani vigezo vya bei hizo Ili tukubaliane sote kuwa dialysis Kwa mfano gharama yake ni 400,00/- kwa mpigo na hufanyika angalau mara 2 kwa wiki?
Tukajua gharama hizo zinatokana na:
1. Umeme kiasi kiasi gani?
2. Maji kiasi gani?
3. Ujuzi kiasi gani?
4. Chemicals kiasi gani?
5. Sindano kiasi gani?
6. Nk
Vivyo hivyo kwa MRI, CT scan, Ventilator, ICU, kulazwa, machela, nk?
Kwa bei hewa hIzi tunazoona haupo mfuko wa bima wala mtu atakayeweza ku survive.
Kimsingi lengo la serikali hapa litakuwa ni kufukarisha watu kwa kisingizio cha gharama kubwa zisizokuwapo.