Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Mwaka jana september nilipata mtihani wa kumuuguza mama pale Muhimbili ikafika mahali akahitajika afanyiwe MRI unfortunately bima niliyomkatia NHIF iliyoni-cost Tsh 360,000/= ikawa haiwezi ku-cover hicho kipimo nikaambiwa nitalipa cash.

Nikawauliza bei gani nikaambiwa kwa mgonjwa wa cash ni 210K nikasema aipitishe ili mama apewe huduma kuingiza jina la mgonjwa wakasema huyu ameingia hapa kwa bima so itabidi ilipwe 450K,nilipata mfadhaiko sana nikaona kama napigwa wakanielekeza kwa msimamizi wa kitengo nikaenda akanionyesha ipo kabisa kwenye system zao.

Mpaka namaliza matibabu ya mgonjwa wangu sikuwahi kupata jibu kwamba kwanini mtu akiwa na bima na asiyekuwa na bima kipimo kile kile kinatofautiana bei kwa ukubwa ule?kama kawaida yetu wabongo nikanung'unika tu moyoni huku nikishukuru mzazi kupona.
 
Board za hospitali ndiyo zinapanga bei

Bodi za hospitali ni kwa maslahi ya hospitali. Sisi wateja tunawakilishwa na nani au vipi huko?

Kigezo cha bei hIzi ni nini?

Inaweza kuwa muda muafaka kumtaka mtu kuachia ngazi.

Huu mbona unaoonekana kuwa ni wizi wa wazi?

Kodi zetu, bajeti wizara ya afya na malipo yetu hospitali vinahusiana vipi?

Kwa hakika ni haki yetu kujua.
 
Mwaka jana september nilikuwa namuuguza mama pale Muhimbili ikafika mahali akahitajika afanyiwe MRI unfortunately bima niliyomkatia NHIF iliyoni-cost Tsh 360,000/= ikawa haiwezi ku-cover hicho kipimo nikaambiwa nitalipa cash.

Nikawauliza bei gani nikaambiwa kwa mgonjwa wa cash ni 210K nikasema aipitishe ili mama apewe huduma kuingiza jina la mgonjwa wakasema huyu ameingia hapa kwa bima so itabidi ilipwe 450K,nilipata mfadhaiko sana nikaona kama napigwa wakanielekeza kwa msimamizi wa kitengo nikaenda akanionyesha ipo kabisa kwenye system zao.

Mpaka namaliza matibabu ya mgonjwa wangu sikuwahi kupata jibu kwanini mtu akiwa na bima na asiyekuwa na bima kipimo kile kile kinatofautiana bei kwa ukubwa ule?kama kawaida yetu wabongo nikanung'unika tu moyoni huku nikishukuru mzazi kupona.
NHIF wameifanya kichaka cha kupiga pesa kwa hizi hospitali kuweka gharama kubwa za vipimo na matibabu zisizo na uhalisia. Ndo maana ili NHIF iweze kuwa sustainable itabidi wafungue hospitali zao wenyewe....
 
Bodi za hospitali ni kwa maslahi ya hospitali. Sisi wateja tunawakilishwa na nani au vipi huko?

Kigezo cha bei hIzi ni nini?

Inaweza kuwa muda muafaka kumtaka mtu kuachia ngazi.

Huu mbona unaoonekana kuwa ni wizi wa wazi?

Kodi zetu, bajeti wizara ya afya na malipo yetu hospitali vinahusiana vipi?

Kwa hakika ni haki yetu kujua.
Kwenye hospital kama zile za mikoa na rufaa kuna kitu kinaitwa HMT(Hospital Mgt Team) hupendekeza na board baada ya kulipwa posho hubariki bila kuangalia maslahi mapana kwa wananchi, upande wa council bei hupangwa na baraza la madiwani
 
Mwaka jana september nilikuwa namuuguza mama pale Muhimbili ikafika mahali akahitajika afanyiwe MRI unfortunately bima niliyomkatia NHIF iliyoni-cost Tsh 360,000/= ikawa haiwezi ku-cover hicho kipimo nikaambiwa nitalipa cash.

Nikawauliza bei gani nikaambiwa kwa mgonjwa wa cash ni 210K nikasema aipitishe ili mama apewe huduma kuingiza jina la mgonjwa wakasema huyu ameingia hapa kwa bima so itabidi ilipwe 450K,nilipata mfadhaiko sana nikaona kama napigwa wakanielekeza kwa msimamizi wa kitengo nikaenda akanionyesha ipo kabisa kwenye system zao.

Mpaka namaliza matibabu ya mgonjwa wangu sikuwahi kupata jibu kwanini mtu akiwa na bima na asiyekuwa na bima kipimo kile kile kinatofautiana bei kwa ukubwa ule?kama kawaida yetu wabongo nikanung'unika tu moyoni huku nikishukuru mzazi kupona.

Mkuu sote tumeshuhudia mifadhaiko ya namna hii. Binafsi nimekuwa ninajiuliza vigezo vinavyotumika:

Ni ujuzi, majengo, vifaa, dawa, au ni ugonjwa?

Mhimbili ukifika ukisema una bima tegemea MRI, CT Scan na makorokoro kibao na bei juu zaidi. Ukisema unalipa mwenyewe hali inakuwa tofauti japo bei bado juu.

Hata hivyo bei za kufuru hizi hazina lengo la kukusanya tozo kwa mgongo wa chupa?
 
Imekuwa si nadra kusikia ankara za mamilioni ya pesa kwa ajili ya tiba kwenye hospitali za umma.

Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

Je ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kwamba kama bei ni kubwa basi kila mtu akaanzishe hospitali yake?

Kama taifa tunakoelekea yaweza kuwa siyo kwema sana.
Wanyonge oyeeeee
 
pamoja na uzalendo na kila kitu lkn lazima ifaamike pi akuwa gharama za matibabu ni kubwa dunia nzima ni sio kwetu hapa. Sasa ndio maaan kuepuka dhahma kama hii srikali ikaja na mpango wa bima kwa wote ili hizi ghrama ziwe shared kupitia bima na kuleta unafuu na uhakika wa huduma pia. Hakuna namna hizi taasisi za afya ziaweza kujiendesha bila pesa, maana zinahitaji pesa kufanya tafiti , kulipa hao wataalamu na kuwekeza kwenye vifaaa na majengo ilio hizo tiba tunazifuata nje zipatikane hapa ndani
 
Kwenye hospital kama zile za mikoa na rufaa kuna kitu kinaitwa HMT(Hospital Mgt Team) hupendekeza na board baada ya kulipwa posho hubariki bila kuangalia maslahi mapana kwa wananchi, upande wa council bei hupangwa na baraza la madiwani

Pana haja ya kuuvaa ujasiri kuukataa wizi wa wazi huu wa wote wanaohusika.

Ina maana waziri husika hayaoni au hayajui haya?
 
pamoja na uzalendo na kila kitu lkn lazima ifaamike pi akuwa gharama za matibabu ni kubwa dunia nzima ni sio kwetu hapa. Sasa ndio maaan kuepuka dhahma kama hii srikali ikaja na mpango wa bima kwa wote ili hizi ghrama ziwe shared kupitia bima na kuleta unafuu na uhakika wa huduma pia. Hakuna namna hizi taasisi za afya ziaweza kujiendesha bila pesa, maana zinahitaji pesa kufanya tafiti , kulipa hao wataalamu na kuwekeza kwenye vifaaa na majengo ilio hizo tiba tunazifuata nje zipatikane hapa ndani

Gharama kubwa hazitoki mbinguni. Kwa nini hatupeani vigezo vya bei hizo Ili tukubaliane sote kuwa dialysis Kwa mfano gharama yake ni 400,00/- kwa mpigo na hufanyika angalau mara 2 kwa wiki?

Tukajua gharama hizo zinatokana na:

1. Umeme kiasi kiasi gani?
2. Maji kiasi gani?
3. Ujuzi kiasi gani?
4. Chemicals kiasi gani?
5. Sindano kiasi gani?
6. Nk

Vivyo hivyo kwa MRI, CT scan, Ventilator, ICU, kulazwa, machela, nk?

Kwa bei hewa hIzi tunazoona haupo mfuko wa bima wala mtu atakayeweza ku survive.

Kimsingi lengo la serikali hapa litakuwa ni kufukarisha watu kwa kisingizio cha gharama kubwa zisizokuwapo.
 
Gharama ni kubwa mno.

Nadhani tughlehailisha Kila kitu na kujadili hili suala.

Ninakubaliana nawe. Hata bungeni panapo dharura mambo yote huahirishwa:

1. Hakuna anayeweza kulipa bei hizi
2. Hakuna mfuko wowote wa bima utanusurika kwa kulipa bei hizi.

Kwa hakika serikali imejipanga kukusanya pesa zote toka kwa wananchi tena kiujanja ujanja tu.

Hii haikubaliki.
 
Mkuu sote tumeshuhudia mifadhaiko ya namna hii. Binafsi nimekuwa ninajiuliza vigezo vinavyotumika:

Ni ujuzi, majengo, vifaa, dawa, au ni ugonjwa?

Mhimbili ukifika ukisema una bima tegemea MRI, CT Scan na makorokoro kibao na bei juu zaidi. Ukisema unalipa mwenyewe hali inakuwa tofauti japo bei bado juu.

Hata hivyo bei za kufuru hizi hazina lengo la kukusanya tozo kwa mgongo wa chupa?
Pamoja na kukusanya tozo nadhani pia kuwatisha wananchi waione bima si chochote si lolote kwamba uwe na bima usiwe na bima lazima hela utatoa tena za kutosha.

Mfano kwa kilichonikuta mimi ikitokea bahati mbaya nikauguza tena siwezi kuthubutu kuonyesha card ya bima itabidi niingie kichwa kichwa wajipigie wanavyotaka maana kama mtu bima unalipa zaidi ya 300K na haikusaidii kwenye vitu vya msingi kama vipimo and still wakishirikiana na m'bia wake wanakukaba shingo tusemeje?

Na ni namna serikali inafanya kui-escape NHIF kwenye issue ya malipo inaona bora mwananchi aumie hela iingie kwake kuliko kwenye mfuko,hovyo kabisa hii serikali sijui wanaotunga hizi sheria huwa wanawaza nini!
 
Kwani vipaumbele vya hii nchi ni vipi? huwa naona tunabangaiza kote tu.

Siku tukiamua kuwa serious, tuainishe vipaumbele vyetu, tujue tuanze na vipi, ndio tutaanza kupiga hatua kama taifa kwenda mbele, lakini kwa sasa, wacha tuendelee kubangaiza tu.
 
Pamoja na kukusanya tozo nadhani pia kuwatisha wananchi waione bima si chochote si lolote kwamba uwe na bima usiwe na bima lazima hela utatoa tena za kutosha.

Mfano kwa kilichonikuta mimi ikitokea bahati mbaya nikauguza tena siwezi kuthubutu kuonyesha card ya bima itabidi niingie kichwa kichwa wajipigie wanavyotaka maana kama mtu bima unalipa zaidi ya 300K haikusaidii kwenye vitu vya msingi kama vipimo and still wakishirikiana na m'bia wake wanakukaba shingo tusemeje?

Na ni namna serikali inafanya kui-escape NHIF kwenye issue ya malipo inaona bora mwananchi aumie hela iingie kwake kuliko kwenye mfuko,hovyo kabisa hii serikali sijui wanaotunga hizi sheria huwa wanawaza nini!

Lengo la serikali ni kuchukua pesa zetu zote kwa namna yoyote.

Ninadhani huku hospitalini ndiyo walikoweka mitego yao sasa.

1. Kwa bima kukusanya viwango vikubwa kadri iwezekanavyo kutoka kwa watu.
2. Kuzitoza bima hizo bei za kufuru huku vikiwekwa visingizio lukuki kuhalalisha unyonyaji zaidi.

Ninadhani kama alivyosema mwendazake: mahakama na polisi vinaweza kuwa vyanzo vizuri sana vya mapato ya serikali, pia hospitali hatukuwa tumeambiwa tu.

Kwa hakika hawa ni wa kukomalia.

Haya hayakubaliki.
 
Imekuwa si nadra kusikia ankara za mamilioni ya pesa kwa ajili ya tiba kwenye hospitali za umma.

Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kwamba kama bei ni kubwa basi kila mtu akaanzishe hospitali yake?

Kama taifa tunakoelekea yaweza kuwa siyo kwema sana.
mkuu mada yako ina mashiko sana ila serikali ya ccm inajua jinsi gani inawanyonya wananchi ilo uwezi kuwafundisha, kwanza hawakomi kudhulumu, ili la afya ndio sehemu zao pendwa kuwapiga walalahoi
 
Mkuu unasomeka. Hawa si wa kuomba.

Kuna bajeti waizara ya afya, kuna tozo na kodi kwetu.

Hawa jamaa wanapanga (hatch) bei kama kuku anavyotaga mayai.

Hawa ni wa kuwavaa head on.

Family member mmoja anatibiwa kwenye viwango vya 10m halafu mkulima anaambiwa anatetewa naye anakenua.

Familia ipi itamudu gharama hewa kama hizo?
 
pamoja na uzalendo na kila kitu lkn lazima ifaamike pi akuwa gharama za matibabu ni kubwa dunia nzima ni sio kwetu hapa. Sasa ndio maaan kuepuka dhahma kama hii srikali ikaja na mpango wa bima kwa wote ili hizi ghrama ziwe shared kupitia bima na kuleta unafuu na uhakika wa huduma pia. Hakuna namna hizi taasisi za afya ziaweza kujiendesha bila pesa, maana zinahitaji pesa kufanya tafiti , kulipa hao wataalamu na kuwekeza kwenye vifaaa na majengo ilio hizo tiba tunazifuata nje zipatikane hapa ndani
Hivi hiyo bima ya afya kwa wote ita-cover kila kipimo katika matibabu, kuna mdau juu hapo, amezungumza juu ya kadhia iliyompata kwa kipimo ilhali alikua amemkatia mgonjwa bima.
 
Hali kama hizi ndizo zinazotuweka kwenye kuchukulia poa.

Mtanzania mjinga akisha aminishwa jambo hubakia kukenua kama huyo ndugu.

Ndiyo maana waziri anadiriki kusema tukalime vyetu na watu bado wanakenua badala ya kumwajibisha.

Tatizo hili taifa linaongozwa na watu ambao hawana uchungu na wananchi kabsaa,huyo Bashe sisi hatuna uwezo wa kunwajubisha wa kumwajibusha ni huyo mnaemwita Mama,Ila mama yenu nae kakaa kimya vijana wake wanaongea tu wanavyojisikia...kauli kama hizi husingezipata wala kuzisikia kipindi Cha JPM.
 
Kwani vipaumbele vya hii nchi ni vipi? huwa naona tunabangaiza kote tu.

Siku tukiamua kuwa serious, tuainishe vipaumbele vyetu, tujue tuanze na vipi, ndio tutaanza kupiga hatua kama taifa kwenda mbele, lakini kwa sasa, wacha tuendelee kubangaiza tu.

Inaonekana kipaumbele cha nchi kwa maana ya serikali ni kukusanya pesa zote kutoka kwa wananchi na kwa njia yoyote.

Haiwezekani kukawepo kodi na tozo zote zilizopo, bajeti wizara ya afya na songombingo hili kwenye hospitali za umma. Huo ni mfano mmoja tu.

Wananchi wamegubikwa na ujinga ambao ndiyo ulio mtaji mkuu wa serikali kwenye kujipatia mapato hayo bila wao kugutuka.

Mbaya zaidi hata wenye kujua wamelambishwa asali. Wakapewa magari na vimaruprupu kidogo basi mwenye shibe hamjui mwenye njaa.

Ikumbukwe pesa za dhuluma zote hizi tokea polisi, mahakamani, TRA, hospitali, LATRA, EWURA, nk zinaishia kwenye mfuko mmoja. Mfuko huo uko na vimifuko vingine China huko.

Sisi kama wananchi kipaumbele kinaweza kuwa katiba. Lakini katiba isisubiri watu wakifa kwa kutomudu gharama hewa za walafi wasioweza kushiba.

Ninadhani pamoja na umuhimu wa katiba mpya hili la gharama za hospitali lilikuwa ni la dharura sana:

1. Nani ana panga bei kwenye hospitali za umma?
2. Bei ni kwa vigezo gani?

Tupate break down ya bei hIzi ambapo mgonjwa anaweza daiwa 10m/- plus akiwa marehemu.
 
Back
Top Bottom