Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Bingwa gani kasomeshwa na umma ? Si tunalipa kodi? Vifaa kuwa vya umma havihalalishi kutolipiwa mkuu , Mwendokasi ni ya Umma ila tunalipa

Usilete siasa hapo mkuu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Ndiyo maana tunataka break down.

Tunavilipia kiasi gani? Malipo hayo yanazingatia mchango wetu kama umma?

Kama unajua tuwekee hapa.

Bila hivyo tuna mashaka tunapigwa Kwa kuuziwa mbuzi kwenye magunia.
 
Sisi ni wateja tunaochelea kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Tumeuliza:

1. Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?
2.Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?
3. Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Majibu yako wapi?
1 .vigezo vinaangalia manunuzi
2.bei ni kwa running cost na manunuzi
Mfano , huwezi pata ajali ukataka mpaka Pini za kuunga mguu wako ambao umevunjika serekali ikulipie , serekali imesha somesha orthopedic surgeons na imeshaweka vitendea kazi ,
Sasa wewe unataka kila kitu wakupe Bure mbaya ufanyi Chochote na Kodi hulipi
 
Gharama zipo za aina Mbili.

Kwa Hospitali kubwa (mashirika yanayojitegemea gharama zinapangwa na bodi ya Hospitali ).

Kwa hospital za Wilaya, vituo vya Afya gharama zinapangwa na Halmashauri.

Vyanzo vya mapato ya Hospitali huwa ni Kama ifuatavyo:

  • BIMA
  • Kama huna Bima utalipa gharama zifuatazo:
  • Kumuona Daktari ( Medical consultation ).

Daktari akikuandikia vipimo ukifika Maabara utalipia.

Ukirudi kwa Daktari akikuandikia Dawa ukienda duka la Dawa utalipia.

Ikitokea UKALAZWA utalipia Kitanda kwa siku kulingana na gharama za Kituo husika.

Ukifa, ndugu zako watalioia gharama za mortuary kulingana na siku ulizokaa.

Zingekuwa namba ingependeza zaidi. Bila hivyo tunaendelea na mbuzi ndani ya gunia.

Hospitali hizi ingekuwa sahihi zisipewe mgawo wowote tokea kwenye tozo na kodi.

Pia zirejeshe gharama zote umma uliwekeza huko.

Vinginevyo tunaibiwa Kodi na tozo kwamba zinaenda mahospitalini ambako hazipo.
 
Mimi ndio nimetoka kumtoa mtu kwa hospital masaa machache yalopita habari za huduma za bure kusema za ukweli ni hakuna zaidi ya ile ya ushauri nasaha
 
1 .vigezo vinaangalia manunuzi
2.bei ni kwa running cost na manunuzi
Mfano , huwezi pata ajali ukataka mpaka Pini za kuunga mguu wako ambao umevunjika serekali ikulipie , serekali imesha somesha orthopedic surgeons na imeshaweka vitendea kazi ,
Sasa wewe unataka kila kitu wakupe Bure mbaya ufanyi Chochote na Kodi hulipi

Tunaibiwa sana kupitia hospitali hizi. Cha kusikitisha zaidi ni watu kama wewe mnaokenua wizi ukiendelea.

Kodi ninalipa na si ajabu kuliko wewe.

Kwa mentally za watu kama wewe ndiyo maana nchi hii Iko tulipo.

Watu kama wewe mna mchango mdogo sana kwa taifa hili.
 
Mimi ndio nimetoka kumtoa mtu kwa hospital masaa machache yalopita habari za huduma za bure kusema za ukweli ni hakuna zaidi ya ile ya ushauri nasaha

ILa bajeti tokea kwenye kodi na tozo hazipungui trillion zinazokwenda huko
 
Zingekuwa namba ingependeza zaidi. Bila hivyo tunaendelea na mbuzi ndani ya gunia.

Hospitali hizi ingekuwa sahihi zisipewe mgawo wowote tokea kwenye tozo na kodi.

Pia zirejeshe gharama zote umma uliwekeza huko.

Vinginevyo tunaibiwa Kodi na tozo kwamba zinaenda mahospitalini ambako hazipo.
Mfano:

- Kwa Kituo nilichopo Mimi, Kama huna Bima:

-Kumuona Daktari, 5000.
  • Vipimo ( stool, urinalysis)=2000
  • Full blood picture = 5000

Bei ya Dawa inategemeana na aina ya Dawa.

Kitanda kwa siku = 3000.

Wound dressing na kushona = 2000
 
Hili blanket la kusema tu kuhusu bodi haitoshi maana tunaolipa ni sisi iwe moja Kwa moja au kupitia bima.

Ipo hatari kubwa ya kuwa tunapigwa.

Tupewe wazi wazi vigezo hivi maana majengo ni ya umma na wafanyakazi ni wa umma pia.
Labda tutafute kiini cha umasikini wetu ni nini hasa. Sio huduma za afya pekee ndizo ghali kiasi cha raia wengi kushindwa kumudu. Elimu pia ni ghali sana. Nyumba ghali. Chakula ghali. Usafiri ghali n.k. Kwenye afya tunajua wazi sehemu kubwa ya dawa tunaagiza nje. Kuzihifadhi ni gharama. Vifaa tiba ghali. Mishahara ya wataalam wa afya ni ghali. Vipato vyeti ni vidogo. Kwa hiyo tujaribu kutafuta namna ya kuinua vipato vya wananchi na sio kudai gharama za huduma zishuke. Hii nchi ina rasilimali nyingi ambazo bado hatujaweza kuzifaidi. Tumekosa uongozi. Viongozi tulionao wanapambana kuhifadhi nafasi zao na ndugu zao na sio kuliinua taifa. Wizi wa mali ya umma kila sehemu. Viongozi wanaishi kama wafalme kati ya wananchi masikini wa kutupwa.
 
Mfano:

- Kwa Kituo nilichopo Mimi, Kama huna Bima:

-Kumuona Daktari, 5000.
  • Vipimo ( stool, urinalysis)=2000
  • Full blood picture = 5000

Bei ya Dawa inategemeana na aina ya Dawa.

Kitanda kwa siku = 3000.

Wound dressing na kushona = 2000

Kama ilivyo sekta zingine pana haja ya hizi bei kuwa kuwa regulated. Watu hawawezi kujipangia tu kiholela hivi. Labda tu kama lengo ni kuwafilisi watu au hiyo mifuko kama inavyojili.
 
Tunaibiwa sana kupitia hospitali hizi. Cha kusikitisha zaidi ni watu kama wewe mnaokenua wizi ukiendelea.

Kodi ninalipa na si ajabu kuliko wewe.

Kwa mentally za watu kama wewe ndiyo maana nchi hii Iko tulipo.

Watu kama wewe mna mchango mdogo sana kwa taifa hili.
Nipo Kwenye field ya medical
Serekali inatoa pesa nyingi mno kusaidia makali na zinaonekana wazi kabisa

Wewe ulie nje ndie unarusha mate

Hakuna gharama Kali kama za afya kwenye maisha

Weka bima Yako ya afya au tafuta pesa , hospital za serekali pia zina social office unaenda wanakusikiliza kama wewe ni pimbi huwezi tafuta pesa wanakusaidia
 
Hospitali za serikali siku hizi hazina tofauti na private kwenye gharama ni mara 100 ukaenda private uta tumia pesa na huduma bora..kuliko kutumia pesa kiasi kile kile kwa huduma mbovu
 
Mfano:

- Kwa Kituo nilichopo Mimi, Kama huna Bima:

-Kumuona Daktari, 5000.
  • Vipimo ( stool, urinalysis)=2000
  • Full blood picture = 5000

Bei ya Dawa inategemeana na aina ya Dawa.

Kitanda kwa siku = 3000.

Wound dressing na kushona = 2000
Kitanda umelipa 3000 it's so cheap wakati sehemu zengine hospital za serekali tunalipa per day tsh 25000/ hiyo ni private room sio icu lakini unajiuliza mwanachi wa kawaida alotakiwa aienjoy huduma hizi ndani ya hospital za serekali analipishwaje tsh 25000 na tozo lukuki zinazomsubiria huko nje kwenye ukamuaji mwengine alosema tuamamie Burundi kweli alimaanisha
 
Kama ilivyo sekta zingine pana haja ya hizi bei kuwa kuwa regulated. Watu hawawezi kujipangia tu kiholela hivi. Labda tu kama lengo ni kuwafilisi watu au hiyo mifuko kama inavyojili.
Hizo bei hazijapangwa kiholela, Mara nyingi ni wataalam kwa kushirikiana na baraza la madiwani.
 
Labda tutafute kiini cha umasikini wetu ni nini hasa. Sio huduma za afya pekee ndizo ghali kiasi cha raia wengi kushindwa kumudu. Elimu pia ni ghali sana. Nyumba ghali. Chakula ghali. Usafiri ghali n.k. Kwenye afya tunajua wazi sehemu kubwa ya dawa tunaagiza nje. Kuzihifadhi ni gharama. Vifaa tiba ghali. Mishahara ya wataalam wa afya ni ghali. Vipato vyeti ni vidogo. Kwa hiyo tujaribu kutafuta namna ya kuinua vipato vya wananchi na sio kudai gharama za huduma zishuke. Hii nchi ina rasilimali nyingi ambazo bado hatujaweza kuzifaidi. Tumekosa uongozi. Viongozi tulionao wanapambana kuhifadhi nafasi zao na ndugu zao na sio kuliinua taifa. Wizi wa mali ya umma kila sehemu. Viongozi wanaishi kama wafalme kati ya wananchi masikini wa kutupwa.
Ninadhani wanaoishi kifalme wanatumbua pia pesa kupitia afya.

Ninadhani afya ni ka soft target ka mavuno bila ukakasi.

Muhimbili Kuna wagonjwa wangapi? Kama ICU ni 450,000/- siku. Mgonjwa mmoja anaweza kupewa ankara ya 10m/- plus. Nk nk.

Wakati huo huo majengo, vifaa, mishahara, wafanyakazi na vyote vilivyomo ni Mali ya umma kupitia Kodi na tozo?

Bado ungependa tusipa mulike huku afya?

Siyo kuwa inafahamika kuwa panga pangua watamleta tu mdhungu na tutajipigia zao zote hapa hapa?
 
Kitanda umelipa 3000 it's so cheap wakati sehemu zengine hospital za serekali tunalipa per day tsh 25000/ hiyo ni private room lakini unajiuliza mwanachi wa kawaida alotakiwa aienjoy huduma hizi ndani ya hospital za serekali analipishwaje tsh 25000 na tozo lukuki zinazomsubiria huko nje kwenye ukamuaji mwengine alosema tumamie Burundi kweli alimaanisha
Kuweni seriously kwenye maisha afya Yako unatakiwa upambane kuilipia
Kuna gharama kubwa Sana kwenye vifaa tiba
La sivyo kubali kufa

Ila anetaka Kodi yangu imlipie matibabu yeye na mke wake na familia haiwezekani , afanye kazi atunze familia yake

Kodi yangu imuwekee infrastructure tu
 
Imekuwa si nadra kusikia ankara za mamilioni ya pesa kwa ajili ya tiba kwenye hospitali za umma.

Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kwamba kama bei ni kubwa basi kila mtu akaanzishe hospitali yake?

Kama taifa tunakoelekea yaweza kuwa siyo kwema sana.
Kakate Bima ya Afya dogo. Hayo mengine utayasikia tu.
 
Hizo bei hazijapangwa kiholela, Mara nyingi ni wataalam kwa kushirikiana na baraza la madiwani.
Uholela unakuja kwa kutojua kinachopelekea gharama za MRI, CT scan, Dialysis nk kuwa bei tunazoambiwa:

IMG_20230215_122840.jpg

Uholela mwingi ndiyo unayopelekea haya.

Haijali nani analipa iwe bima au binafsi kwa mtu mmoja kufilisika ni lazima.

Wewe huoni hivyo ndugu?

Au unasema kwa vile hayajakukuta?
 
Kuweni seriously kwenye maisha afya Yako unatakiwa upambane kuilipia
Kuna gharama kubwa Sana kwenye vifaa tiba
La sivyo kubali kufa

Ila anetaka Kodi yangu imlipie matibabu yeye na mke wake na familia haiwezekani , afanye kazi atunze familia yake

Kodi yangu imuwekee infrastructure twewe

Kuweni seriously kwenye maisha afya Yako unatakiwa upambane kuilipia
Kuna gharama kubwa Sana kwenye vifaa tiba
La sivyo kubali kufa

Ila anetaka Kodi yangu imlipie matibabu yeye na mke wake na familia haiwezekani , afanye kazi atunze familia yake

Kodi yangu imuwekee infrastructure tu
Mkuu utakuwa una kulaga meza kuu unajua kazi ya kodi zetu zinatakiwa zifanyie nini kwetu wananchi mojawapo ni kuleta haya madawa na vifaa tiba serekali inalijua hilo ila mtu kama we ukiongea inaonekana wazi hata bima ya afya unalipiwa na serekali ukiagiza gari pengine utozwi hata kodi bandarini
 
Kakate Bima ya Afya dogo. Hayo mengine utayasikia tu.
Umeshindwa kujua kinachoongelewa:

"Haijali nani analipa iwe bima au binafsi kwa mtu mmoja kufilisika ni lazima."

Zingatia NHIF tayari inapumulia mashine.

Siyo wewe peke yako ila uko na wale mburula wote wenye kuwadhania wengine ni madogo na tena kama wao, ni mabinafsi wenye kujiongelea wao na jamaa zao tu.

Watu kama nyie alisema shujaa mmoja, mnao mchango mdogo sana kwenye taifa hili.

Bure kabisa!
 
Kama ilivyo sekta zingine pana haja ya hizi bei kuwa kuwa regulated. Watu hawawezi kujipangia tu kiholela hivi. Labda tu kama lengo ni kuwafilisi watu au hiyo mifuko kama inavyojili.
Unatania au[emoji23][emoji23][emoji23], hivi boss unajuwa hospitali kama hospitali inajiendeshaje. Hapa sisemei kituo cha afya. Natumai unajua tofauti kati ya hospitali, kituo cha afya na zahanati. Naunavyoambiwa kuwa bajeti ya wizara ya afya imetengwa kiasi kadhaa nategemea unajua ile bajeti inatumika kwaajili ya nini, maana ile pesa sio inayotumika kuendeshea hospitali kama hospitali. Kama kweli unadhumuni la kutaka breakdown cost ya kila kitu hospitali, anza wewe mwenyewe kutafuta bei ya kila mashine, reagent zinazotumika kufanyia vipimo, vitendea kazi vya ziada vinavyotumika kufanyia hivyo vipimo, actual cost ya kila dawa kabla haijanunuliwa na msd kutoka nje. Na maintainance cost ya kila mashine inayotumika kutunza mashine, ikiwemo na mazingira safi ya hospitali ili kutosababisha contamination. Hivyo vyote unaweza kuvitafuta mtandaoni ukavipata. Mind you kodi yako sio inayoendesha hospitali, kodi yako inasimamia ujenzi na hatua za mwanzo wa ufunguzi wa hospitali baada ya muda hospitali inatakiwa ijiendeshe maana bajeti ya wizara ya afya inamatumizi makubwa na mengi zaidi ya kuendesha hospitali, ambazo hizo huduma zinakuwa nje ya hospitali na siyo ndani ya hospitali, kwaakili akili unaweza ukaifikiria moja na ukaipata. Principle ni kwamba, kila hospitali baada ya kufunguliwa inatakiwa iendelee kujiendesha yenyewe. Basketfunds huja mara 2 au 3 kwa mwaka. Sasa anza kuzitafuta hizo prices, kama kweli unania!
 
Back
Top Bottom