Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Umeshindwa kujua kinachoongelewa:

"Haijali nani analipa iwe bima au binafsi kwa mtu mmoja kufilisika ni lazima."

Zingatia NHIF tayari inapumulia mashine.

Siyo wewe peke yako ila uko na wale mburula wote wenye kuwadhania wengine ni madogo na tena kama wao, ni mabinafsi tu wenye kujiongelea wao na jamaa zao tu.

Watu kama nyie alisema shujaa mmoja, mnao mchango mdogo sana kwenye taifa hili.

Bure kabisa!
Acha porojo dogo. Kakate Bima ya Afya. Dunia nzima bei za matibau ziko juu. Nitajie nchi ambayo ukifanyiwa oparesheni kubwa unalipa buku au buku ten. Unafikiri Wazungu walikuwa wajinga kutumia Bima za Afya? Wanajua!!
Kaa na mburura wenzako akina babaako na mamaako waendelee kukudanganya eti bei ziko juu, bei ziku juu! Nenda kwa waganga wa kienyeji! PUMBAVU!!!!
 
Nikusaidie kitu rafiki!

Hospitali sio mambo ya CCM Vs CDM or CUF.

Kama unafikiri matibabu ni rahisi fungua hospitali yako kama una uwezo huo alafu utuletee mrejesho...
Mwambie matibabu ni gharama watu waache porojo .amna matibabu ya maana anyoweza kumoatia mtu bure .ukitaka matibabu ya bure utaishia kupewa vipanadol viwili vitatu kuridhisha wanasiasa
 
mtu kama we ukiongea inaonekana wazi hata bima ya afya unalipiwa na serekali ukiagiza gari pengine utozwi hata kodi bandarini
Nakatwa pesa kwenye mshahara wangu napata bima ya family yangu .
Uku duniani haupo ili mtu mwingine akuhudumie
 
Kitanda umelipa 3000 it's so cheap wakati sehemu zengine hospital za serekali tunalipa per day tsh 25000/ hiyo ni private room sio icu lakini unajiuliza mwanachi wa kawaida alotakiwa aienjoy huduma hizi ndani ya hospital za serekali analipishwaje tsh 25000 na tozo lukuki zinazomsubiria huko nje kwenye ukamuaji mwengine alosema tuamamie Burundi kweli alimaanisha
Mind you tofautisha level za health facility. Kuanzia, zahanati, kituo cha afya, hospitali ya wilaya, hospitali ya rufaa ya mkoa, hospitali ya kanda na hospitali ya taifa. Pili tofautisha huduma muhimu na huduma za ziada, mfano huduma ya muhimu ni wodi ya wagonjwa ila wodi ya private ni ya ziada. Kulazwa wodi ya private sio kwamba itakufanya upone haraka lahasha ulitaka wewe utulivu wako kujitenga na wagonjwa wengine. Running cost ya kila level ya health facility ni tofauti, kwakuwa kila level ya health facility kuna huduma zinaongezeka au kuboreshwa kadri unavyopanda juu ikiwemo huduma zipatikanazo na hata level ya ujuzi ikiwemo huduma za kibingwa. Sasa hapo ni actuaries ndio huingia kufanya kazi.
 
Imekuwa si nadra kusikia ankara za mamilioni ya pesa kwa ajili ya tiba kwenye hospitali za umma.

Nani anayepanga bei hIzi na kwa vigezo gani?

Je, ni bei kwa ugonjwa, dawa, ujuzi, vifaa au majengo?

Au ni yale ya Bashe na wakulima na bei zao za vyakula?

Kwamba kama bei ni kubwa basi kila mtu akaanzishe hospitali yake?

Kama taifa tunakoelekea yaweza kuwa siyo kwema sana.
Ni mbinu ya kuwalazimisha watu wajiunge na bima fake na ya kibaguzi nhif
 
Bro! Ni sawa na kwenda kwenye duka ukakuta watu kadhaa wanalipa laki moja ili kununua kitu fulani. Kwa akili ya kawaida, zile laki moja zinazoingizwa na kila mteja, mimi nitaona kama ni faida ya mwenye duka, kitu ambacho sicho. Lakini kurupuka kufungua biashara hiyo hiyo uone kama inalipa. Faida za huduma za afya zikiwa kubwa sana basi ni asilima 25%, sasa serikalini ukweli huduma wanazotoa mara nyingi zinatozwa kwa pesa, ambayo ukifanya costing utajua ni hasara.

Gharama za matibabu nchini Tanzania ni ndogo sana, ukilinganisha na kilichostahili kutozwa. Udogo wa gharama za matibabu unachangia kutoboresha huduma za afya, kwa sababu hospitali husika, zinashindwa kuendesha huduma za kawaida kama usafi, lakini pia kuanzisha huduma au kutanua za zamani kwa manunuzi ya vifaa vipya n.k.

Maumivu yote wayapata kwa sababu huna bima ya afya. Afya si bei rahisi kama unavyodhani.
 
Ni mbinu ya kuwalazimisha watu wajiunge na bima fake na ya kibaguzi nhif
Kama unafamilia udumuia familia Yako , achana na kusubiria watu wengine watoe Kodi ili ikuhudumie
 
Kama unafamilia udumuia familia Yako , achana na kusubiria watu wengine watoe Kodi ili ikuhudumie
Zingatia:

"Haijali nani analipa iwe bima au binafsi kwa mtu mmoja kama bei ni hizo, kufilisika ni lazima."

IMG_20230215_122840.jpg

Ama kwa hakika umeandika kama mlamba asali au mtu usiyejitambua.
 
Bro! Ni sawa na kwenda kwenye duka ukakuta watu kadhaa wanalipa laki moja ili kununua kitu fulani. Kwa akili ya kawaida, zile laki moja zinazoingizwa na kila mteja, mimi nitaona kama ni faida ya mwenye duka, kitu ambacho sicho. Lakini kurupuka kufungua biashara hiyo hiyo uone kama inalipa. Faida za huduma za afya zikiwa kubwa sana basi ni asilima 25%, sasa serikalini ukweli huduma wanazotoa mara nyingi zinatozwa kwa pesa, ambayo ukifanya costing utajua ni hasara.

Gharama za matibabu nchini Tanzania ni ndogo sana, ukilinganisha na kilichostahili kutozwa. Udogo wa gharama za matibabu unachangia kutoboresha huduma za afya, kwa sababu hospitali husika, zinashindwa kuendesha huduma za kawaida kama usafi, lakini pia kuanzisha huduma au kutanua za zamani kwa manunuzi ya vifaa vipya n.k.

Maumivu yote wayapata kwa sababu huna bima ya afya. Afya si bei rahisi kama unavyodhani.
Tatizo lako kuiangalia hoja hii kama suala binafsi.

Uhalali upi MRI kuwa 450,000/-? Ni umeme, ujuzi, machela, ugonjwa au kitu gani?

Itapendeza zaidi ukizingatia anayelipa ndiye mnunuzi wa mashine hiyo moja kwa moja au kupitia bima.

Zingatia maumivu ni pale pale iwe mlipaji ni bima au mtu binafsi kwani mifuko hii inauliwa na watu tunaowaona wakiifilisi kama hivi ilivyo hapa kwenye madai.
 
Weka misingi ya familia Yako ikiwemo afya , acha na mawazo kwamba watu wengine wapigike wakulipie wewe matibabu
Kwa hiyo mifuko hii inapofilisika haikuhusu siyo?
 
Zingatia:

"Haijali nani analipa iwe bima au binafsi kwa mtu mmoja kama bei ni hizo, kufilisika ni lazima."

View attachment 2518452

Ama kwa hakika umeandika kama mlamba asali au mtu usiyejitambua.
Kwa hiyo unataka walipa Kodi wote tukalipe iyo bill , kumbuka bill sio ya muhimbili tu muhimbili nao wanatakiwa wakalipe bill za watu kama oxygen, watoa huduma na n.k
 
Ukiona unapewa huduma ya Bure juwa wazi umelipiwa,
Na ukiona kuna majengo ya hospitali, vifaa, majengo, dawa nk huku ukichagizwa ulipe Kodi na tozo maana yake nini?
 
Kwa hiyo unataka walipa Kodi wote tukalipe iyo bill , kumbuka bill sio ya muhimbili tu muhimbili nao wanatakiwa wakalipe bill za watu kama oxygen, watoa huduma na n.k

Kwa hiyo kwenye MRI ya 450,000/- hao wa huduma nyingine ni pesa ngapi? Wewe hujui kuwa oxygen tuliambiwa vifaa vya kuzalisha wenyewe mahospitalini vilinunuliwa Kwa pesa zetu za ndani?

Kwanini hizi break down zisiwe wazi? Au wewe ni mnufaika wa hii biashara yA mbuzi ndani ya magunia?
 
Na ukiona kuna majengo ya hospitali, vifaa, majengo, dawa nk huku ukichagizwa ulipe Kodi na tozo maana yake nini?
Kodi Yako haitoshi

Serekali imekuwekea majengo, na watoa huduma na vifaa

Running cost kama umeme, maji , stationary, mawasiliano, kununua vifaa tiba , dawa, ulinzi , usafi
N.k

Labda kama nchi tupitishe kama laki 5 kila familia kwa mwaka only kwa afya
 
Kwa hiyo kwenye MRI ya 450,000/- hao wa huduma nyingine ni pesa ngapi? Wewe hujui kuwa oxygen tuliambiwa vifaa vya kuzalisha wenyewe mahospitalini vilinunuliwa Kwa pesa zetu za ndani?

Kwanini hizi break down zisiwe wazi? Au wewe ni mnufaika wa hii biashara yA mbuzi ndani ya magunia?
Ukiwa nje ya medical field ndio unapiga kelele ingia ndani uone mziki

Kama sio wafadhili mngekufa asilimia kubwa

Wamerekani ukiwaona wasalimie kwa heshima
 
Kodi Yako haitoshi

Serekali imekuwekea majengo, na watoa huduma na vifaa

Running cost kama umeme, maji , stationary, mawasiliano, kununua vifaa tiba , dawa, ulinzi , usafi
N.k

Labda kama nchi tupitishe kama laki 5 kila familia kwa mwaka only kwa afya

Kodi yangu isingekuwa haitoshi ma V8 yasingekuwapo.

Hizi general statements ni Kwa ajili ya kuhalalisha nini?

Nani ana panga bei hIzi? Tunashirikishwaje kwenye kupanga bei hizo? Au ni ki Bashe Bashe tu na wakulima?

Kwanini tusipewe break down ya bei hizi tukajiridhisha?

Unadhani tukubaliane tu na hIzi sweeping statements zako kuwa gharama za afya ni juu sana na kodi zetu pamoja na raslimali zetu za nchi kuwa hazitoshi huku pesa zinaishia China?
 
Ikiacha kutenga Bajeti Wananchi mtaweza kuchagia ili kulipa mishahara ya Madaktari na wahudumu wa afya? na kununua Vifaa Tiba? pamoja na kujenga Majengo ya kutolea Huduma?
Gharama tinazotozwa hivi sasa hazina tofauti sana na hospitali binafsi ambazo kwa kutumia tozo tunazotoa zinalipa mishahara mizuri zaidi madaktari na wahudumu wa afya pamoja na kununua vifaa tiba na pia kujenga majengo yao!
 
Ukiwa nje ya medical field ndio unapiga kelele ingia ndani uone mziki

Kama sio wafadhili mngekufa asilimia kubwa

Wamerekani ukiwaona wasalimie kwa heshima
Ukawasalimie wamarekani badala ya kuwawajibisha wezi wanaojulikana?

FnzAtagX0AIXEAW.jpeg

Na hata hizi muziki utakuwa huo huo.
 
Back
Top Bottom