Mjadara mzuri huu.
Tips.
1.Wananchi/clients wanahitaji mchanganuo wa huduma na gharama zake.
2.Kuna concept kwa wananchi kuwa hospital na vituo vya Afya vya umma vinaendeshwa na Govt 100%..... kwa hili inabidi watu waelewe kuwa si kweli kuwa Govt inagharimia 100% cost za uendeshaji ... kuna percentage imeachwa kwa mtumiaji kuchangia. Na jukumu la kupanga bei limekaimishwa kwa bodi za uendeshaji wa vituo/hospital so wao ndio wanapanga bei ya hudumu ambazo mgonjwa atachajiwa ili ku-compliment kiasi kilichotolewa na serikali ili kukamilisha mzunguko mzima wa matibabu... hapa utakutana na pesa ya kufungua file, kitanda n. k
3.kuna baadhi ya gharama za uendeshaji zinategemea mapato ya kituo/hospital chenyewe eg. umeme, maji, posho za overtime na extra duty, on call allowances , Ulinzi, Usafi ...hapa si ajabu kituo cha kawaida kabisa kinahitaji 60M ku-cover hizo cost, so watu waelewe tanesco na mamlaka za maji zinatoza pesa as usual.
4.kuhusu itemization.. hili liko kwenye miongozo/maandishi kama wao wanavyopenda kusema .. BUT nani ana muda wa kuanza kumfafanulia clients item moja moja ...so huduma zimekuwa fixed kwenye mfumo wa package ... na kila package na bei yake(boards za uendeshaji ndo wazee wa shoo hizi).
5.Kuhusu Gharama kuwa juu ... inabidi tufanye comperative ... unasema gharama iko juu ukilinganisha na wapi? kwa ukanda wetu sisi ndio tunatoa huduma cheap sana.... kama refference point ni uchumi wa watumiaji (mimi nikiwemo) hapo huwezi kuturidhisha wotee.
WHO IS RESPONSIBLE.
again .. mwananchi eg mwanzilishi wa maada anatakiwa aihoji mamlaka(mhimili uliojichimbia zaidi) kuhusu gharama hizi na itemazation.
CRAZY OPINION FROM MY COLLEGUE.
Turudi sera ya nyuma kidogo ... huduma za Afya na Elimu ziachiwe Govt tuuu na ziwe buree ... private sector abakie huko kwingine ... hii haitatuhitaji BIMA wala mbwembwe nyiingi .. kwanza wahudumu hawatakuwa na choices za kukimbia kimbia mara yuko kituoni kwake muda kidogo yuko private ... hakutakuwa na upotevu wa bidhaa za Afya .. hata akiiba cormodity atapeleka wapi?
Kongole mleta mada .. but kuwa flexible wa Tz hatuko serious hivyo .. tunasubir Afe tukachange msibani at the time hatukuweza kuchangia gharama ya Tiba.
Bila shaka mjadala kuwa mzuri una maana hoja ni ya msingi na so Kwa maslahi binafsi.
Kama ulivyomalizia inafahamika kuwa watanzania huwa hawako serious na mambo ya msingi. Kabla ya jambo mtu kumkuta, ubinafsi uliopitiliza ndiyo kwao.
Jambo jingine la kutambua ni uvivu wao wa kuchambua mambo na utayari wao kuhoji mambo
Pamoja na yote niweke hapa wazi kuwa hakuna kurudi nyuma na neno
flexibility litazingatiwa.
Yafuatayo ni maoni zaidi kuhusiana na bandiko lako, kifungu kwa kifungu kwa mlolongo ule ule kama ulivyokuja nao:
Tips:
1. Wananchi/clients wanahitaji mchanganuo wa huduma na gharama zake.
2. Concept iliyopo ni kuwa inawezekana bajeti ya serikali kuziendesha hospitali hizi haitoshi. Kwa kiasi gani haijulikani. Hapa ni muhimu kukafanyika audit ya kuaminika ili ijulikane bayana.
Kwa hili inajulikana kuwa bajeti kutoka serikalini inaweza kuwa haigharimii 100%. Gharama za uendeshaji ziko je?
"Audit ya kuaminika itatoa jibu hapa."
... Kwamba kuna percentage imeachwa kwa mtumiaji kuchangia. Hili lina ukakasi.
"Kiasi gani kimeachwa na kwa kigezo?" Hilo litakuwa swali #1 niliache pending kwanza.
Kwamba kuna % imeachwa na jukumu la kupanga bei limekaimishwa kwa bodi za uendeshaji wa vituo/hospital so wao ndio wanapanga bei ya hudumu ambazo mgonjwa atachajiwa ili ku-compliment kiasi kilichotolewa na serikali ili kukamilisha mzunguko mzima wa matibabu... hapa utakutana na pesa ya kufungua file, kitanda n. k.
-------
Niseme kuwa hapo unasomeka kigezo kikiwa swali #1 pending limejibiwa.
3. Kwamba kuna baadhi ya gharama za uendeshaji zinategemea mapato ya kituo/hospital chenyewe eg. umeme, maji, posho za overtime na extra duty, on call allowances , Ulinzi, Usafi ...hapa si ajabu kituo cha kawaida kabisa kinahitaji 60M ku-cover hizo cost, so watu waelewe tanesco na mamlaka za maji zinatoza pesa as usual.
------
Haya hayana tatizo kutegemea na majibu ya swali #1 lililo pending.
4. Kuhusu itemization, haina tatizo kuwa iko miongozo/maandishi kama wao wanavyopenda kusema .. kwamba nani ana muda wa kuanza kumfafanulia clients item moja moja ...kwamba huduma zimekuwa fixed kwenye mfumo wa package ... na kila package na bei yake(boards za uendeshaji ndo wazee wa shoo hizi).
--------
Hili Kwa setup iliyopo inafahamika ambako ndiko tunakoita kuuziana mbuzi kwenye gunia.
Tunamjua mwenye lake jambo. Hapa siyo hospitali (kwa maana ya madaktari au wahudumu).
Ni kweli kuwa wao wanatumia tu hizi packages zenye bei zote za huduma programed ndani.
Mwenye package ndiye mwenye majibu na huyo ndiye anayemhitajika awafafwnulie wadau wake zaidi ya bei za huduma. Yaani kwenye gharama, item kwa item kwa kila huduma.
Kwa vile bila shaka ni Kwa maslahi yake kuonyesha kuwa tuko fair, bila shaka atakuwa forthcoming kutoa ushirikiano wenye kujua alizifikia je bei hIzi zinazolalamikiwa.
(boards za uendeshaji ndo wazee wa shoo hizi).
Bila shaka hapo una maana hao ndiyo wenye hizo packages.
5. Kuhusu Gharama kuwa juu hili ni kuhusiana na uchumi wa watumiaji. Kwamba ni chini kuliko wa ukanda huu? Hilo sisi halituhusu kwa sababu kodi, tozo, uchumi, mipango, sera nk za nchi hizi tofauti.
"Wasiwasi wetu ni kuwa bei zinazotozwa ni kubwa mno kwa watu au mfuko wowote wa bima kutokufilisika."
Kwamba kama reference point ni uchumi wa watumiaji hapo hatuwezi kuwaridhisha wote? Hapana. Kujua gharama halisi kwa uwazi zitamridhisha kila mtu.
Izingatiwe hakunaombwi msaada, bali kinachogomba ni dalili za kukosekana kwa haki bin haki.
Zaidi sana kuwekwa mipango jumuishi yenye kuwaridhisha wote ni jambo linalowezekana. Hii ninaitunza kama swali #2 pending.
WHO IS RESPONSIBLE.
Ni wajibu wa wananchi kuihoji mamlaka(mhimili uliojichimbia zaidi) kuhusu gharama hizi na itemization.
Zingatia post #375 kwenye Uzi huu ina hadidu za rejea ya nini kifuate.
Mawazo, maoni au mapendekezo yoyote kuyaboresha yaliyomo kwenye post #375 litakuwa jambo jema.
Ni muhimu tukawa wageni rasmu Kwa Mh. Waziri Ummy Mwalimu kuziona ni mbivu au mbichi, na kulikoni.
CRAZY OPINION FROM YOUR COLLEGUE.
Turudi sera ya nyuma kidogo ... huduma za Afya na Elimu ziachiwe Govt tuuu na ziwe buree ... private sector abakie huko kwingine ... hii haitatuhitaji BIMA wala mbwembwe nyiingi .. kwanza wahudumu hawatakuwa na choices za kukimbia kimbia mara yuko kituoni kwake muda kidogo yuko private ... hakutakuwa na upotevu wa bidhaa za Afya .. hata akiiba cormodity atapeleka wapi?
Hili ni muafaka kama maswali yale pending mawili pale juu yatakuwa yamejibiwa, kwa mfano:
1. Kwa nini Kuna percentage imeachwa kwenye gharama za uendeshaji na serikali?
Kwamba serikali itoe 100% ya gharama za uendeshaji. Ambapo kupitia bima, tozo au kodi ihakikishe hospitali zinapata mahitaji yake 100%.
2. Serikali inaweza kulenga certain percentage e.g. 90% ya population kuona kuwa inaridhika. Halafu ikawa na maalum kwa wanaobakia.
Pamoja na yote tuko kwenye njia sahihi, kwamba yote yajengwe katika msingi wa bei zilizo halali.
Kila bei ya huduma kwenye hospitali ya umma ni lazima ijulikane item kwa item.
"Asiibiwe mtu moja kwa moja au mtu kupitia bima."
Nisiache kushukuru kwa kufuatilia na kutambua kuwa kuna hoja ya msingi yenye kuhitaji majibu kutoka kwa wahusika.
Haifurahishi kusikia aana wapendwa marehemu wanashikiliwa kwa kushindwa kulipa gharama zaa matibabu za matibabu zisizo mchanganuo.
Haifurahishi kusikia watu wameshindwa kulipa, watu au mifuko ya bima imefilisika. Kisa na mkasa ikiwa ni kukosekana kwa uwazi katika bei hIzi.
Yote ni mapambano.
Aluta Continua.