Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12

Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12

Matokeo yake alivyorudi Tanzania akasema ametumia Dola za kimarekani milioni 12. Maradhi gani hayo? Kafanya operesheni ngapi? Alikwenda hospitali ya aina gani mpaka alipe dola milioni 12. Hakuna duniani, huo ni ufisadi.
Duuh. Wacha waombe msamaha wanajua maana yake.
 
BARAZA la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamedai wamemwibukia spika wa Bunge, Job Ndugai, huku wakitaka ripoti ya gharama za matibabu ya kiongozi huyo wa chombo cha kutunga sheria alipokuwa India, iwasilishwe bungeni.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Issa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ndani ya matibabu hayo kuna harufu ya ufisadi.

Issa alidai kuwa matibabu ya Spika Ndugai yalitumia dola za kimarekani milioni 12 na kwamba huo ni ufisadi uliolenga kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania.
“Tunataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni, vikiwamo vyeti vya matibabu na madaktari walifanya operesheni,” alisema.


Alidai kuwa Spika Ndugai alikwenda nchini India kutibiwa ingawa hawajui alikuwa anasumbuliwa na nini.

“Matokeo yake alivyorudi Tanzania akasema ametumia Dola za kimarekani milioni 12. Maradhi gani hayo? Kafanya operesheni ngapi? Alikwenda hospitali ya aina gani mpaka alipe dola milioni 12. Hakuna duniani, huo ni ufisadi.

“Hiyo ilikuwa njia ya kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania kutumia kisingizio cha maradhi kwenda hospitali, kumbe kavusha fedha,” alidai huku akisisitiza Baraza la Wazee Chadema, linataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni.

“Ripoti ya Spika Ndugai, tunataka vyeti vyote vya hospitali, hesabu ya madaktari, alifanyiwa operesheni ngapi. Tunataka hesabu kamili ya miezi yote ya matibabu kama zimefika Dola za kimarekani milioni 12,” alisema.

Aprili 14, mwaka huu, Spika Ndugai akijibu swali la gharama ya matibabu yake nje ya nchi wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuugua kwake kumelisababishia taifa fedha nyingi, hawezi kujua.

“Labda ningekufa watu wangefurahi. Katika matibabu yoyote yale, tunawatibu watu hatuangalii thamani ya mtu na kiwango cha fedha kilichotumika. Kinachoangaliwa kama kuna matumizi mabaya ndani ya matumizi hayo,” alisema.

“Nilitibiwa mwaka 2015/16 na hesabu hizo ni za 2017/18. Unajua tena mtu akibanwa anatafuta sababu huku na kule. Wanaotibiwa ni wengi na hospitali niliyokwenda kutibiwa ni ya kawaida. Nilikutana na Watanzania wa kila aina, wa aina zote, tunapishana huyu anakwenda kwa daktari huyu, mwingine huyu, sijawahi kwenda hospitali ya New York (Marekani), Ujerumani, naenda India ambako ndiko Watanzania wanakotibiwa,” aliongeza.

Aprili, mwaka jana, Spika Ndugai alirejea nchini akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa miezi kadhaa.
 

Attachments

  • IMG_1415.MP4
    1.3 MB
Duuh. Wacha waombe msamaha wanajua maana yake.
Hayo ni matokeo ya karma, kila kitu utakilipa hapa hapa Duniani.

Wakati wananchi wake anaowawakilisha wa Jimbo la Kongwa, baadhi yao wanakufa kwa ugonjwa wa malaria, kwa kukosa dawa za kujitibia, yeye anafuja mamilioni ya Dollar za kimarekani, kwa matibabu yake binafsi🥺
 
Hayo ni matokeo ya karma, kila kitu utakilipa hapa hapa Duniani.

Wakati wananchi wake anaowawakilisha wa Jimbo la Kongwa, baadhi yao wanakufa kwa ugonjwa wa malaria, kwa kukosa dawa za kujitibia, yeye anafuja mamilioni ya Dollar za kimarekani, kwa matibabu yake binafsi🥺
Uliwapima ukajua wamekufa kwa sababu ya Malaria?
 
Nadhani ilimaliza bajeti ya matibabu kwa vigogo wa serikali wakakia kutibiwa Mzena.
Hata bima ya afya haitoshi.So sad.
 
Ndugai amesemwa sana vibaya, SASA katangulia mbele za haki endeleeni na li nchi lenu.
 
India huko ukienda kichwa kichwa wanakukunguta tu!
Ndugai kumbuka alupokuwa huko alikaa 5 🌟 hotel
Alitaka special treatment

Ova
 
Mungu fundi, hata ukatibiwe hosp gani kwa gharama ipi kama wewe zamu ishafika ya kuondoka UTAONDOKA.
Cha ajabu katuacha sisi wa Mwananyamala tunadunda.
 
Back
Top Bottom