Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12

Ndio maana alikuwa anamchukia cag kumbe alikuwa anaogopa kuumbuliwa na taarifa ya cag kuhusu ufisadi wake .shetani ,Ndugai na prince makalio wanaimaliza hii nchi .
 
Umesoma vizuri ni karibu bilioni 28 imetumika kumtibu mgonjwa mmoja. Hatuna viongozi bali wahuni waliojivisha ngozi ya uongozi kumbe ni majibu makubwa usiku na mchana yako busy kuifilisi Tanzania yetu.

😂😂😂😂😂
Nimesoma vizuri au? Kama kweli imetumika hiyo hela, hatuna viongozi.
 
Yule mzee ana miaka mingi aliyoishi ilikuwa inamtosha. Kulikuwa hakuna haja ya kufuja hela zote zile.
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji15][emoji15] USD million 12 ni sawa karibia kabisa na BILLION 30[emoji19][emoji19][emoji19] kweli kuna roho zina thamani kubwa sana
Hawa ndio wana CCM sasa waliojificha kwenye mwamvuli wa kutetea wanyonge
 
Awamu iliyoamua kuvunja rekodi ya wizi na ufisadi wa awamu zote zilizopita bila woga wala aibu. Chama kimeshika UTAMU.
Wengine waliogopa sheria na waliiba kwa kujificha, hawa hawajali sheria wanaiba kwa ubabe waziwazi. Washamba na limbukeni...kweli masikini akipata matako hulia mbwata!
 
Cha kushangaza zaidi Mkuu ni hawa wahuni wenzie kutaka kumpa huyo nduli miaka mingine mitano pamoja na maovu ya kutisha kila kona.

Waliomsukumizia Ikulu huyo dikteta, Mkapa na Kikwete, wameuchuna kimyaaaa kama hawahusiki na haya majanga na wizi wa kutisha unaofanywa awamu hii.

Wengine waliogopa sheria na waliiba kwa kujificha, hawa hawajali sheria wanaiba kwa ubabe waziwazi. Washamba na limbukeni, kweli masikini akipata matako hulia mbwata!
 
Gharama matibabu Ndugai yazua jambo
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Issa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ndani ya matibabu hayo kuna harufu ya ufisadi.

Issa alidai kuwa matibabu ya Spika Ndugai yalitumia dola za kimarekani milioni 12 na kwamba huo ni ufisadi uliolenga kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania.
“Tunataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni, vikiwamo vyeti vya matibabu na madaktari walifanya operesheni,” alisema.

Alidai kuwa Spika Ndugai alikwenda nchini India kutibiwa ingawa hawajui alikuwa anasumbuliwa na nini.
“Matokeo yake alivyorudi Tanzania akasema ametumia Dola za kimarekani milioni 12. Maradhi gani hayo? Kafanya operesheni ngapi? Alikwenda hospitali ya aina gani mpaka alipe dola milioni 12. Hakuna duniani, huo ni ufisadi.

“Hiyo ilikuwa njia ya kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania kutumia kisingizio cha maradhi kwenda hospitali, kumbe kavusha fedha,” alidai huku akisisitiza Baraza la Wazee Chadema, linataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni.

“Ripoti ya Spika Ndugai, tunataka vyeti vyote vya hospitali, hesabu ya madaktari, alifanyiwa operesheni ngapi. Tunataka hesabu kamili ya miezi yote ya matibabu kama zimefika Dola za kimarekani milioni 12,” alisema.

Aprili 14, mwaka huu, Spika Ndugai akijibu swali la gharama ya matibabu yake nje ya nchi wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuugua kwake kumelisababishia taifa fedha nyingi, hawezi kujua.
“Labda ningekufa watu wangefurahi. Katika matibabu yoyote yale, tunawatibu watu hatuangalii thamani ya mtu na kiwango cha fedha kilichotumika. Kinachoangaliwa kama kuna matumizi mabaya ndani ya matumizi hayo,” alisema.
“Nilitibiwa mwaka 2015/16 na hesabu hizo ni za 2017/18. Unajua tena mtu akibanwa anatafuta sababu huku na kule. Wanaotibiwa ni wengi na hospitali niliyokwenda kutibiwa ni ya kawaida. Nilikutana na Watanzania wa kila aina, wa aina zote, tunapishana huyu anakwenda kwa daktari huyu, mwingine huyu, sijawahi kwenda hospitali ya New York (Marekani), Ujerumani, naenda India ambako ndiko Watanzania wanakotibiwa,” aliongeza.

Aprili, mwaka jana, Spika Ndugai alirejea nchini akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa miezi kadhaa.
Yaleyale ya HASSY KITINE.....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Spika Ndugai atuambie tu ukweli ni nini hicho alichotibiwa kwa Billion 30?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Uwiiii 30bil ndugai onea huruma kodi zetu tafadhali
 
Ni hiviiii

Huyo Ndugai sidhani kama ana uwezo wa kuchota hela zote hizo, yeye ni receiver tu,huyo aliyeidhinisha kiwango chote hicho kiende kwa matibabu ya mtu mmoja ndio TUNAMTAKA😏😏😏
 
Gharama matibabu Ndugai yazua jambo
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Issa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ndani ya matibabu hayo kuna harufu ya ufisadi.

Issa alidai kuwa matibabu ya Spika Ndugai yalitumia dola za kimarekani milioni 12 na kwamba huo ni ufisadi uliolenga kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania.
“Tunataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni, vikiwamo vyeti vya matibabu na madaktari walifanya operesheni,” alisema.

Alidai kuwa Spika Ndugai alikwenda nchini India kutibiwa ingawa hawajui alikuwa anasumbuliwa na nini.
“Matokeo yake alivyorudi Tanzania akasema ametumia Dola za kimarekani milioni 12. Maradhi gani hayo? Kafanya operesheni ngapi? Alikwenda hospitali ya aina gani mpaka alipe dola milioni 12. Hakuna duniani, huo ni ufisadi.

“Hiyo ilikuwa njia ya kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania kutumia kisingizio cha maradhi kwenda hospitali, kumbe kavusha fedha,” alidai huku akisisitiza Baraza la Wazee Chadema, linataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni.

“Ripoti ya Spika Ndugai, tunataka vyeti vyote vya hospitali, hesabu ya madaktari, alifanyiwa operesheni ngapi. Tunataka hesabu kamili ya miezi yote ya matibabu kama zimefika Dola za kimarekani milioni 12,” alisema.

Aprili 14, mwaka huu, Spika Ndugai akijibu swali la gharama ya matibabu yake nje ya nchi wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuugua kwake kumelisababishia taifa fedha nyingi, hawezi kujua.
“Labda ningekufa watu wangefurahi. Katika matibabu yoyote yale, tunawatibu watu hatuangalii thamani ya mtu na kiwango cha fedha kilichotumika. Kinachoangaliwa kama kuna matumizi mabaya ndani ya matumizi hayo,” alisema.
“Nilitibiwa mwaka 2015/16 na hesabu hizo ni za 2017/18. Unajua tena mtu akibanwa anatafuta sababu huku na kule. Wanaotibiwa ni wengi na hospitali niliyokwenda kutibiwa ni ya kawaida. Nilikutana na Watanzania wa kila aina, wa aina zote, tunapishana huyu anakwenda kwa daktari huyu, mwingine huyu, sijawahi kwenda hospitali ya New York (Marekani), Ujerumani, naenda India ambako ndiko Watanzania wanakotibiwa,” aliongeza.

Aprili, mwaka jana, Spika Ndugai alirejea nchini akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa miezi kadhaa.
Gharama ya matibabu ya Tundu Lisu kuanzia Kenya hadi Ubelgiji itakuwa imefikia USD 12 M ?
 
e bwanaeee awamu hii ina UOZO MKUBWA SANA unafunikwa kwa vitisho vya kila aina ila siku ukifumuka wanyonge watabaki mdomo wazi
 
Back
Top Bottom