Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12

Gharama matibabu Ndugai yazua jambo. Alitumia zaidi ya Dola Milioni 12

Hizo bilioni 30 alikuwa anatibiwa kitu gani? Hapa kuna ufisadi mkubwa umefanyika
 
Huu uzi umekosa hata support ya bavicha wenyewe kwa sababu hata akili zao wenyewe pamoja na kuwa za kinyumbu lkn zimeshindwa kuamini kwamba mtu anaweza kutumia billion 30 kwa matibabu tu
Hiyo bilioni 30 huyo ndugai alikuwa anakwenda kubadilishiwa roho?
 
Alafu leo anasema hajui alipo lissu!!??
Anatafuta laana kwanguvu huyu. Lakini nahisi hizi hela zimetoroshwa na CCM kiujanja kwaajili ya uchaguzi mkuu ujao kwaajili ya kutoa rushwa ili washinde uchaguzi.
 
Gharama matibabu Ndugai yazua jambo
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Issa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ndani ya matibabu hayo kuna harufu ya ufisadi.

Issa alidai kuwa matibabu ya Spika Ndugai yalitumia dola za kimarekani milioni 12 na kwamba huo ni ufisadi uliolenga kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania.
“Tunataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni, vikiwamo vyeti vya matibabu na madaktari walifanya operesheni,” alisema.


Alidai kuwa Spika Ndugai alikwenda nchini India kutibiwa ingawa hawajui alikuwa anasumbuliwa na nini.
“Matokeo yake alivyorudi Tanzania akasema ametumia Dola za kimarekani milioni 12. Maradhi gani hayo? Kafanya operesheni ngapi? Alikwenda hospitali ya aina gani mpaka alipe dola milioni 12. Hakuna duniani, huo ni ufisadi.

“Hiyo ilikuwa njia ya kuvusha fedha ambazo ni kodi za Watanzania kutumia kisingizio cha maradhi kwenda hospitali, kumbe kavusha fedha,” alidai huku akisisitiza Baraza la Wazee Chadema, linataka kuona ripoti zote zinawasilishwa bungeni.

“Ripoti ya Spika Ndugai, tunataka vyeti vyote vya hospitali, hesabu ya madaktari, alifanyiwa operesheni ngapi. Tunataka hesabu kamili ya miezi yote ya matibabu kama zimefika Dola za kimarekani milioni 12,” alisema.

Aprili 14, mwaka huu, Spika Ndugai akijibu swali la gharama ya matibabu yake nje ya nchi wakati akizungumza na waandishi wa habari, alisema kuugua kwake kumelisababishia taifa fedha nyingi, hawezi kujua.
“Labda ningekufa watu wangefurahi. Katika matibabu yoyote yale, tunawatibu watu hatuangalii thamani ya mtu na kiwango cha fedha kilichotumika. Kinachoangaliwa kama kuna matumizi mabaya ndani ya matumizi hayo,” alisema.
“Nilitibiwa mwaka 2015/16 na hesabu hizo ni za 2017/18. Unajua tena mtu akibanwa anatafuta sababu huku na kule. Wanaotibiwa ni wengi na hospitali niliyokwenda kutibiwa ni ya kawaida. Nilikutana na Watanzania wa kila aina, wa aina zote, tunapishana huyu anakwenda kwa daktari huyu, mwingine huyu, sijawahi kwenda hospitali ya New York (Marekani), Ujerumani, naenda India ambako ndiko Watanzania wanakotibiwa,” aliongeza.

Aprili, mwaka jana, Spika Ndugai alirejea nchini akitokea India alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa miezi kadhaa.
Kama kweli zilitumika US$ 12 mil, hilo ni tatizo kubwa! Lazima tuwe na kiwango cha kumuhudumia mtu. Huwezi kuokoa roho ya mtu mmoja kwa kiasi hicho cha pesa kwa kisingizio kwamba roho ya mtu haina gharama. NO! NO! Taifa haliwezi kufilisika kwa sababu tu kuna mtu asnaitwa spika. Spika hana thamani kiasi hicho.

Spika lazima aelewe kwamba yeye kufa au kupona siyo vibaya kama ilivyo kwa m-TZ yeyote kufa au kupona. Tusiogope kifo kiasi hicho! Mimi nikifa ni sawa na spika akifa. Kwa wenye akili tunaelewa hata atumie bilioni zetu atakufa tu! Nami nitakufa! Pesa hizo zirudishwe, zichunguzwe.
 
Ndugai aweke risiti hadharani ili Bunge lichunguze kwa kina kuhusu huu ubadhirifu wa kutisha wa pesa za walipa kodi.

Kama ni kweli matumizi yalifikia kiwango hicho, kwa kiwango chochote kile na kwa nchi yoyote ile, huo ni wizi wa hali ya juu. Kuna wengi watakuwa walitajirika kutokana na hayo matibabu.

Kwa wizi huu, Spika ni lazima awe mnyonge sana dhidi ya yeyote mwenye mamlaka ya kiserikali.
 
Hizi hela zinatosha kununua club ya Simba na zikabaki kudadeki
 
Najiuliza tuu hio hela ingeokoa Maisha mangapi huko kijijini kwa wale wasio na access ya huduma ya afya...Kama madawa
 
Hizo hela zimemfanya awe mtumwa wa Jiwe. Ndiyo maana Mhimili anaosimamia kaukasimu kwa Jiwe afanye atakalo.
Kila akijaribu kujiinua, anakumbushwa hizo hela. Atakuwa mtumwa milele.
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji15][emoji15] USD million 12 ni sawa karibia kabisa na BILLION 30[emoji19][emoji19][emoji19] kweli kuna roho zina thamani kubwa sana
Ila zitakufa tu nazo
 
Ndugai aweke risiti hadharani ili Bunge lichunguze kwa kina kuhusu huu ubadhirifu wa kutisha wa pesa za walipa kodi.

Hawa ndio wazalendo wenyewe wa hapa kwetu.
 
😂😂😂😂😂
Nimesoma vizuri au? Kama kweli imetumika hiyo hela, hatuna viongozi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni haki yake hata akipewa 1trion ni sawa tu amepigania sana nchi hii. Amepigana kufa na kupona mpaka CAG amepunguziwa bajeti karibu 7b kwanini tusimpongeze! Kwanini asipewe 30 b kama motivation! Hongera sana supika kwa kupigania maislai ya Taifa, Mungu akuzidishie maisha uishi milele na milele!
 
Hajajiuzulu tu kwa kadhia hii? Mbona kuna taarifa za kufikia five star hotel yeye na katibu myeka wake na nesi na daktari wake na house girl wake ambazo hajazikataa wala kuzikanusha?
Ati kajiongezea na zile milioni 350 za taifa star! Kweli, alikuwa na kila sababu ya kumharass cag lakini karma haitamwacha hata kidogo! Hebu ajipeleke mahakama ya mafiasadi kabla hajalazimishwa kwa kuvishwa pingu!
 
Back
Top Bottom