Gharama na taratibu za kufungua sanduku la posta

khaliciouz

Ushauri ambao naona utapata sanduku bila kuhangaika tena miezi hii ndo watu wengi wanakua wamenyang'anywa masanduku kwa kushindwa kulipia.

Priority ya kugawa masanduku kubwa ipo kwa makampuni na hawaitaji attachment kama TIN number, cjui business licence wala nini zaidi ya kujaza tu fomu yao tena wanakusaidia, wewe tumia hata jina la kampuni la mtu unayemfahamu na ni vizuri awe na physical address, uwe na picha mbili na mwenzako awe na picha mbili ili mpewe kadi ya sanduku.

Kwa uhakika zaidi uwe na 150,000/= pamoja na kuhonga marketing manager wa posta sababu ndiye anayegawa masanduku kwa makampuni na ujifanye una expectations kubwa sana za kutumia huduma za posta kama CITY DELIVERY nk.

Kwenye 150,000 kuna gharama za awali za kulipia sanduku zinaweza kufika hata 90,000/= ikiwa ni pamoja na kuchongewa funguo. halafu uwe na kama elfu 30 hivi inatosha kabisa kwa soda/rushwa ya mtu wa marketing wa posta.

Pia urahisi na unafuu wa kupata sanduku upo kwenye branch za nje za posta mpya kama Pugu Road karibu na Sigara na nyinginezo hata za nje ya Mji. Ila gharama ya laki na nusu ni ya kupata sanduku posta mpya au ya zamani ukizingatia trick niliyokupa ya malengo makubwa ya kikampuni na ada ya box la kampuni kwa mwaka ni elfu 52.

Kuna upotevu na ucheleweshwaji sana na mizigo au barua ambazo hazipo registered kwa branch za nje ya mji within Dar kuliko posta mpya.

Kama ni muagizaji wa vitu vya nje ya nchi sana fungua box branch tofauti na ya posta mpya ili kuepukana na watu wa TRA coz ni wasumbufu sababu hata kama umetumiwa soksi watataka kufungua ili wakague. Wakihisi ina kitu chenye value kubwa sana.
 
Kufungua sanduku kwaajili ya kampuni ni shilingi laki moja ila kwaajili ya mtu binafsi ni elfu hamsini tu za kitanzania.

Mkuu your right ila sio kila eneo unalohitaji utakuta yako wazi utaambiwa andika barua ya maombi na subiri nafasi ikipatika utajulishwa.
 
Hii itakua ngumu kukodishiwa! Nenda posta gharama za mwanzo ni kama laki na nusu ila kulipia kila mwaka ni 13,000 kwa dsm

Mkuu mimi ninalo pale Posta mpya nenda na hiyo 11,800 uone kama utapata, hiyo laki na nusu nimesema ni gharama za mwanzo na sio official. Sipendi Rushwa ila siwezi kukosa nachohitaji kwa sababu ya misimamo yangu.

Unachoongea ni kweli ila watu wanachukulia mambo kirahisi rahisi tu, hata huko nje mji ni sawa tu na ni rahisi kupata sababu usipojiongeza na pesa ya maji utakuwa unaambia subiri tutakupigia we jaza fomu uingie kwenye waiting list.
 
Mkuu mimi ninalo pale Posta mpya nenda na hiyo 11,800 uone kama utapata, hiyo laki na nusu nimesema ni gharama za mwanzo na sio official. Sipendi Rushwa ila siwezi kukosa nachohitaji kwa sababu ya misimamo yangu.

Mhhhh basi ghalama zinatofautiana sehemu na sehemu, I am telling you from deep down kwamba mimi ninalo Kijitonyama maeneo ya pale Bamaga karibia na TBC ninalipia kwa mwaka TSH 11,800/=
 
Unachoongea ni kweli ila watu wanachukulia mambo kirahisi rahisi tu, hata huko nje mji ni sawa tu na ni rahisi kupata sababu usipojiongeza na pesa ya maji utakuwa unaambia subiri tutakupigia we jaza fomu uingie kwenye waiting list.

Aise mkuu basi mimi nilipata box kwa urahisi sana, du inabidi nilishikilie sana sikuwa najua kama ni deal kiasi hiki
 
We lishikilie haswa hapa mjini bhana.

Asante sana aise sintolichezea tena walah, huweziamini kila mwaka huwa nalilipia mwezi wa kwanza ila naweza extend mpaka mwezi wa pili nikalikuta lipo tu, du asante sana maana sikuwa najua kama ni kitu adimu, next year ntalipia tarehe mbili mwezi wa kwanza kabisa du ebwana ee
 
Ningeomba kwa anayejua anifahamishe namna ya kufanya ili na mimi niwe na sanduku la posta. Kuanzia kwenye procedure za kufuata mpaka na gharama zote. Maana mpaka leo nikitumiwa barua sina njia ya kuipata sababu sandaku ninalotumia sijui kama lipo active na lipo mkoani.

Naomba kuwasilisha
 
tembelea ofisi ya posta tawi lolote karibu na wewe, utapata maelezo. au jaribu kusoma chchote hapa www.posta.co.tz kama wana maelezo
 
Karne hii bado unategemea p.obox? Labda kama unamiliki gazeti
.
 
Hvi bado mnaandikianaga barua mpaka karne hii ya 21?
 
Ukienda posta tafuta picha mbili yako na ya mtu wa karibu yako ili ukiwa haupo yeye atahusika so ziwe nne yaani zako mbili na huyo jamaa mbili baada ya hapo utajaza form utalipia mm nakumbuka nililipa 24,000 kufungua kitu km hicho ila kuepuka usumbufu uwe 30,000 haivuki hapo unakuwa ushamaliza process watakupa id yao ikiwemo na sanduku lako la posta baada ya week mbili au tatu utapewa ufunguo wako wa sanduku la posta inamaanisha km utaitumia kabla ya kupewa ufunguo barua utakazo tumiwa utaenda kuchukua dirishani kwa id yako.
 

Nenda posta kuu watakupa utaratibu na posta zenye nafasi.
 
tembelea ofisi ya posta tawi lolote karibu na wewe, utapata maelezo. au jaribu kusoma chchote hapa www.posta.co.tz kama wana maelezo

Nyie mnaohoji kuhusu barua wote ni watoto wa mama, hamjajua maisha bado. Ndugu muuliza swali nenda posta iliyokaribu nawe watakupa maelekezo, kuhusu garama si kubwa kwa mwaka unalipia haizidi elfu 15, kwa hiyo ni wewe jipange tu


Nenda posta kuu watakupa utaratibu na posta zenye nafasi.
Asanteni sana kwa msaada wakuu wa kazi. Nawatunuku degree ya heshima daraja la pili " Honoris Causa Magna Cum Laude"
 
Jamani humu ndani mna mijitu mijinga na isiyojitambua, hivi mtu kuja humu akauliza swali lake kutaka kupata ufumbuzi likajitokeza jitu likajibu utumbo linamaanisha kitu gani ama kweli kuwa mstaarabu unahitaji ujitume kweli kweli. Mwisho ukiona hauna msaada pita tu silazima ujibu.
 
Afadhali uwajibu mkuu mi nimewashindwa.
 
Sanduku la posta la mtu binafsi linagharimu jumla TShs 54,400 hyo ni gharama imecontain gharama ya ada ya mwaka shs 35400 ufunguo Shs 17000 pamoja na authority card shs 2000 ukifika posta yoyote utajaza fomu then utaambiwa uwe na picha pasport size stamp size yakoymoja na ya mtu wakowwa karibu incase ukipata tatizo yeye ataenda posta na authority card kuchukua mzigo wako
 


Ni kweli dada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…