Gharama ya Bima ya Afya kwa wote ni Tsh. 150, 000 kwa kaya, wasio na uwezo kugharamiwa na serikali

Gharama ya Bima ya Afya kwa wote ni Tsh. 150, 000 kwa kaya, wasio na uwezo kugharamiwa na serikali

Huna akili
Ambao hawana akili ni hawa wanaokuja na program kila muda ambazo hawana akili yoyote ya kuzifanikisha

Ipo wapi bima ya CHF? Walifeli kipi? Waliizindua kwa nguvu kubwa, sasa hivi ipo chali.

Ukashindwe kuhudumia Watoto kwa toto afya ya 50k, alafu uje uweze kuhudumia bure karibu nusu ya watanzania ambao ni maskini wa kutupwa. Machawa kama wewe ndio huwa mnasikiliza huu ujinga
 
Serikali imetangaza rasmi kuanza utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote katika awamu ya kwanza. Katika awamu hiyo, kitita cha huduma muhimu za afya kitatolewa na skimu za Bima ya Afya kwa gharama ya shilingi 150,000 kwa kaya yenye watu wasiozidi sita.

Akizungumza kuhusu mpango huo, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema wananchi wasio na uwezo, wakiwemo wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu, watagharamiwa na Serikali.

Aidha, amesema kwa gharama ya 150,000, watu sita walio kwenye kaya moja watajiunga na Bima ya Afya kwa Wote itakayojumuisha mwanachama mchangiaji, mwenza wa mwanachama na wategemezi wanne.

“Wategemezi hao wanne wanaweza kuwa ni mzazi wa mwanachama au mzazi wa mwenza wa mwanachama; mtoto wa mwanachama wa kuzaa, kuasili au wa kambo aliye na umri chini ya miaka 21 au ndugu wa damu wa mwanachama aliye na umri wa chini ya miaka ishirini na moja” amefafanua.
KAYA MLIOZAA WATOTO 5 MJUE LAK 3 INAWAHUSU WAWEKE SAWA

BAADA YA SITA

YULE MMOJA ANAINGIA KWENYE KAYA NYINGINE

USINIULIZE WALIOZA 11
450K INAWAHUSU

AAHSANTENTUNANZA LINI KU APPLY
 
Pingapinga kazini,msio na jema,msiopendeka,subirini wakenya wajisajili mkie delea kupiga kelele

mathematics haidanganyi, hiyo bima kwa wote serikali haina uwezo wa kui-finance, kwa tanzagiza unatumia kigezo gani kwanza kubaini mwenye uwezo na asiye na uwezo? boda boda ana uwezo au hana? dada muuza mchicha, utingo, fundi gereji bubu, shehe msikitini? i mean, unapima vipi nchi ambayo >85% ya uchumi wake ni informal i.e hakuna records zozote popote za kodi au michango mingine ya kiuchumi, how do you finance that? kwa fedha zipi?
btw >68% ya watanzagiza wana kipato cha chini ya dola 1/siku usd, hiyo hela extra ya kuchangia matibabu wataitoa wapi? …
 
Ngoja tuone, ila isijekutokea ninabima na nadaiwa pesa kwa ajili ya matibabu, tutatifuata mno.
 
1. CHF ilifeli kwa sababu zipi???
2. Afya toto card ilifeli vip ?? Serikali inaona nigarama kumhudumua mtoto wakaona wafute bima ya afya ya watoto ila cha kushangaza NHIF wanakopesha taasisi za afya pesa wanunue vifaa,wajenge majengo mfano MOI na kuboresha miundombinu hii siyo kazi ya NHIF nikazi ya serikali kujenga hospitali kununua vifaa tiba na dawa.
Pesa zinzochangiwa na wanachama wa NHIF nikwaajili ya matibabu ya wanufaika si kwaajili ya kukopesha taasisi za afya.
3. Huduma ya mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano imewashinda wazee kupata huduma bure imeshindikana mtaweza bima kwa wote
 
Wakuu,waliojisajili na hii bima vipi?
Inafanya kazi ?tujilipue
 
Back
Top Bottom