Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Mkuu inategemea na ww unataka kukamua alizeti kiasi gani kwa siku. Lakini mwa sababu umeomba tu shauri nitakupa gharama za kiwanda cha size ya kati ambayo inatumia mashine ya kukamua no 95.habarini ndugu zangu,
Naomba kufaham garama halisi endapo mtu anataka kuanzisha kiwanda kidogo kwa ajir ya kukamua mafuta ya alizeti hususan garama ya mashine zote zinazohitajika
Aina hii ya mashine ukipaya ya kichina bei ni 5.5 mil kwa dar.
Mashine hii itahitaji uwe pia na filter yake ambayo bei ni 3.5mil kwa dar.
Kama utataka kurefine mafuta yawe kama ya sunblet kwa mfano itabidi uwe na mini refinery ambayo itakughramu 9.5mil
Kwa hiyo hapo utaona utahitaji 5.5+3.5+9.5= 18.5mil
Lakini refinery siyo lazima uwe nayo unapoaanza kwa hiyo kwa kuanza utahitaji hizo mbili ya kukamua na ku filter ambazo bei yake jumla ni 9mil
Hizo bei ni bila gharama za nyuma ya kuzifunga pamojana na material ya kuanzia.
Kama unahitaji uelewa zaidi unaweza kuuliza
Nimeona post ni ya zamani ila jibu langu linaweza saidia wengine