Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Gazeti la Financial Times la Marekani, imenukuu utafiti uliofanywa na kampuni ya ushauri wa kimkakati duniani Ernst & Young-Brexit, ikisema kama Marekani, Umoja wa Ulaya, na Uingereza zinataka kuondoa kwa kiasi kikubwa utegemezi wao kwa viwanda vya China na minyororo ya ugavi ifikapo mwaka 2050, zitahitaji kuwekeza dola trilioni 23.6 za Kimarekani za ziada katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Marekani itahitaji dola trilioni 13.7 za ziada katika kipindi cha miaka 25 ijayo, Umoja wa Ulaya dola trilioni 9.1, na Uingereza takriban dola bilioni 800. Pesa hizo zitatumika kimsingi kujenga upya viwanda, mifumo ya utafiti, ukuzaji wa software, miundombinu, na minyororo ya ugavi ya juu na chini ambayo kwa sasa inategemea China.
Hata hivyo, pesa hizo haziwezi kuhakikisha nchi za Magharibi kutimiza lengo lao. Inamaanisha kwamba ili kuondoa utegemezi kwa minyororo ya ugavi ya China ifikapo mwaka 2050, nchi za Magharibi zitalazimika kutumia utajiri wao mkubwa, wakikabiliwa na nakisi ya bajeti katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, maendeleo ya teknolojia, na ujenzi wa ulinzi. Hata kama nchi hizo zingetumia rasilimali zake zote, ikiwa ni pamoja na dola trilioni 23.6, itakuwa vigumu kwao kujenga mfumo kamili wa viwanda ambao China imeujenga kwa miongo kadhaa.
Kulingana na utabiri wa Shirika la Nishati la Kimataifa, ifikapo mwaka 2035, China bado itachukua zaidi ya asilimia 60 ya uzalishaji wa lithiamu na kobalti iliyosafishwa duniani, na takriban asilimia 80 ya grafiti ya kiwango cha betri na vifaa adimu vinavyohitajika duniani. Hii inamaanisha kwamba ifikapo wakati huo, tasnia za viwanda vya nchi za Magharibi bado vitategemea China.
Wanasiasa wa nchi za Magharibi hudai kuamini nguvu ya kanuni ya kisoko. Lakini wakati utengenezaji wa China una uwezo zaidi, wanaanza kusema “usahihi wa kisiasa” unachukua nafasi ya kwanza badala ya kanuni ya kisoko. Vipimo hivi viwili vyenyewe ni unajisi mkubwa zaidi kwa uchumi wa kisoko.
Hatimaye, sababu ya kimsingi ya mchezo huu wa “kuondoa utegemezi wa China” ni kwamba nchi za Magharibi haziwezi kukubali maendeleo ya kasi ya China, na kukataa dunia yenye ncha nyingi. Wanataka kurekebisha upya mnyororo wa viwanda wa kimataifa kupitia njia ya kisiasa, wakisahau kwamba utaratibu wa uchumi haubadiliki kutokana na matakwa yao. Dola trilioni 23.6 za kimarekani zitakuwa gharama ya kwanza tu, gharama kubwa zaidi zitakuwa ni kupoteza kabisa ushindani wa nchi za magharibi, mfumuko mkubwa wa bei kwa watu wa nchi hizo, na maumivu ya kudumu kwa uchumi wa dunia nzima.
Pia soma: Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika labadilisha mwelekeo wa bara la Afrika